11/04/2022
💦PUNYETO:
Hakuna dawa ya kutibu punyeto, walakini kuna njia zinazoweza kutibu tabia hiyo, nazo ni;
kuepuka vichochezi na upweke, kujishughulisha, kutumia muda mwingi na watu wengine, Kufanya mazoezi, kupata kikundi na msaada kwa mtaalamu. ~
📲Epuka vichochezi:
epuka tovuti/vitabu/picha/video za utupu kwani hivi vyote huchochea hamu ya kupiga punyeto hivyo viepuke kadri iwezekanavyo. Tumia vichungi/vichujio ili kuvizuia kukufikia. ~ 🤹Jishughulishe:
tafuta shughuli uzipendazo ambazo zitachukua muda wako k**a michezo na wengine, kucheza chombo cha muziki na zingine. Pia ufahamu ni muda gani ambao hamu huwa juu sana na upange shughuli nyingine wakati huo. ~
👨👩👧👦Tumia muda mwingi na watu wengine:
kwani watu wengine hupiga punyeto kwa sababu wanahisi upweke au hawana kitu/mtu wa kujaza wakati wao, hivyo jitahidi kuwa na wengine kwani unaweza jumuika na wanafamilia, ndugu, marafiki, wapwa au kikundi cha mazoezi. ~
🚵Mazoezi:
K**a kukimbia, kuogelea, kuruka kamba na mengine mengi yanaimarisha mwili wako na ni bora sana kwani hukuza hisia za ustawi, furaha na kuimarika zaidi na hivyo kupunguza hamu ya kupiga punyeto mara kwa mara. ~
👬Pata kikundi kinachosaidia na kutegemeza:
kwani kutakusaidia kupunguza hisia za hatia na aibu na kutoa nafasi unayohitaji ili kuelezea wasiwasi na kuzungumzia waziwazi juu ya changamoto unazozikabili na kukuza mikakati mizuri ya kukabiliana nayo. ~
👩⚕️Tafuta msaada wa kitaalamu:
Tafuta ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya ya akili/mwanasaikolojia ambaye ni mtaalamu wa afya ya jinsia kwani kuzungumza naye kutasaidia kujifunza mikakati ya kurekebisha tabia na kuizuia. Tuma neno Afya kwa WhatsApp namba +255 627 362 567 kupata elimu zaidi juu ya afya na SULUHISHO la kudumu