11/01/2023
HII NDIO NJIA RAHISI NA SALAMA YA KUPUNGUZA TUMBO
Wengi wa wagonjwa wa mifupa ambao nawahudumia wamemtumia meseji za kutaka kujua njia ya kupunguza tumbo na mafuta tumboni...
Na hii ni kutokana kwamba wengi wao sababu ya maumivu ya viungo imesababishwa na Uzito mkubwa unaombatana na kuwa na tumbo kubwa na manyama uzembe .
Njia nyepesi kabisa ya kupunguza tumbo kubwa ni ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.
Nilipata nafasi wiki hii ya kuzungumza na daktari mmoja katika hospitali ya Muhimbili ambaye sitamtaja kwa jina na alikuwa na mengi ya kuelezea jinsi hali hiyo inavyoanza na husababishwa na nini.
Alisema kuwa,k**a unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula vyakula vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa wingi.
Vyakula k**a viazi mviringo, wali mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku tatu, pia ulaji wa nyama nyekundu inasababisha kuongezeka uzito na pia huongeza ukubwa wa tumbo,vyakulahivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi kidogo sana.
"Kuna wakati tumbo linajitokeza na kuwa kubwa kuliko kawaida hali hiyo inasababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi, kutokunywa maji ya kutosha na pia kula bila ya mpangilio maalum" aliendelea kusema.
Alisema pia kuwa k**a mtu anataka kupunguza mafuta au kuondoa kitambi anatakiwa kula milo mitatu kwa siku na si kujinyima kula kwa kudhani kuwa unaweza kupungua uzito.
"Vyakula vya wanga na mafuta hufanya mtu kunenepa, acha au punguza kula vyakula vyenye wanga ili kupunguza mafuta yaliyozidi mwilini.
Mafuta yanaporundikana mwilini athari moja kubwa ni kuwa na tumbo kubwa." Alikazia Kwa kusema hivyo.
Na mwisho aliniambia kuwa ,tumbo kuwa kubwa ni dhahiri kuwa chakula unachokula hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na ziada mwilini na hii ziada inafanyika mafuta ambayo hujiwekesha akiba katika maeneo mbalimbali ya mwili.
Na Kwa kuwa Chakula hiki cha ziada huwa hakitakiwi, mwili hukibadilisha na kuweka akiba katika mfumo wa mafuta kitaalamu k**a glycogem.Unaweza kukabiliana na kuzidi kwa protini zinazoyeyushwa na kuwekwa katika akiba kwa mfumo huo wa mafuta.
TIBA NA USHAURI
K**a mtu mwenye tatizo hilo ni bora akapangilia mlo wake kwa siku k**a ifuatavyo👇🏼
"Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana k**a kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika hali inayotakiwa.
Watu wengi wanatumia wanga mwingi wakati wa usiku muda ambao unaenda kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi ya kujikusanya, kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa tumboni.
Je Mazoezi husaidia kupunguza uzito wa mwili na manyama uzembe?
Ni kweli Mazoezi ya viungo yamethibitishwa kusaidia kuchoma mafuta ya ziada katika mwili. Kutokana na hali ya ulaji unaweza kutengeneza manyama uzembe katika kifua, mapaja na maeneo fulani ya tumbo ambayo yametengenezwa kupokea maeneo ya ziada yanayotokana na mafuta yenyewe au sukari iliyobadilishwa kuwa mafuta. Nishati inayotokana na nafaka ambayo pia haiwezi kutumika muda huo hutengenezwa kuwa mafuta na kupelekwa eneo husika.
Wanaume huwa na asilimia 8 hadi 20 ya mafuta katika mwili na ni kawaida wakati kwa wanawake ni asilinia 13 hadi 25.
Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni kwa wingi katika mapafu yako na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu kwa mwili. Mafuta yanayounguzwa kwanza ni yale ya kawaida kabla ya kuingia katika akiba.
Lakini pia unashauri k**a mtu atakula kidogo kabla ya kuanza mazoezi ili kutoa nishati ya kutosha ya kufanyisha mazoezi. "Lakini k**a unaenda mwendo fulani mdogo tu au unatembea kwa dakika 30 huenda usiwe na haja kabisa ya kula hata hicho kidogo na hasa ikiwa uliweka kitu kidogo saa tatu/nne zilizopita.