Afya Ya Jamii Kwa Wote

Afya Ya Jamii Kwa Wote Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Afya Ya Jamii Kwa Wote, Medical and health, magomeni, Dar es Salaam.

Afya ya jamii kwa wote, is a page specifically for general health issue in all Fields of human health, including advice, consultation and health promotion topics

TUACHENI MAZOEA YA KUWAPA DAWA ZA MAJI ZA KIKOHOZI NA MAFUA WATOTO CHINI YA MIAKA 4Fatal Child Poisonings Linked to Comm...
05/11/2021

TUACHENI MAZOEA YA KUWAPA DAWA ZA MAJI ZA KIKOHOZI NA MAFUA WATOTO CHINI YA MIAKA 4

Fatal Child Poisonings Linked to Common Cough and Cold Meds
Laura Lillie

October 28, 2021

11
Add to Email Alerts
A number of fatal child poisonings have been linked to common cough and cold medications, according to a report.

The Pediatric Cough and Cold Safety Surveillance System, which tracks fatal child poisonings, has identified 40 such deaths in recent years and raised particular concern about medications containing diphenhydramine, a common antihistamine that can be sedating.

"There is little evidence that cough and cold medicines make children feel better or reduce their symptoms, but there is evidence they can suffer harm," says Kevin Osterhoudt, MD, medical director of the Poison Control Center at the Children's Hospital of Philadelphia.

In recent years, the FDA has advised labeling changes and recommended that cough and cold medications not be given to children younger than 2. Drugmakers also voluntarily relabeled these products to state "do not use in children under 4 years of age."

Compared to older children or adults, young children have a different physiology when they breathe, so any product containing antihistamines can be a danger to little kids, Osterhoudt says.

But a recent survey shows about half of American parents gave their child cough and cold medication the last time they were ill, Osterhoudt says. And the findings suggest that cough and cold medications are in homes where children might find them.

Using the new evidence from the national surveillance system, investigators set up an expert panel to review the results. They found that most of the deaths were in children under the age of 2. The results were reported in the October issue of Pediatrics.

In seven instances, death followed the intentional use of medication to sedate the child, reports lead investigator Laurie Seidel Halmo, MD, from Children's Hospital Colorado in Aurora.

"It's not uncommon for parents to use sedatives like diphenhydramine to make their child sleepy for activities like air travel," Osterhoudt says.

While antihistamines can be sedating, "an overdose of antihistamines like diphenhydramine can paradoxically become a stimulant," having the opposite effect, he explains.

Adults and teens who take overdoses will sometimes become delirious, hallucinate, and have a racing heart.

But in young children, "if not careful with your dosing, you could actually give too much and create this stimulant activity," Osterhoudt says.

In six other cases, the cough and cold medication was given to murder the child, the investigators reported.

The findings are "concerning," especially with "more than one-half of nontherapeutic intent cases determined to be malicious in nature," Michele Burns, MD, from Boston Children's Hospital, and Madeline Renny, MD, from the Grossman School of Medicine in New York City, wrote in a commentary with the report.

This important fatality review shows that despite safety efforts, young children remain at risk for death, they report.

The investigators point out that labeling changes do not seem to have protected vulnerable children, and they recommend that doctors educate parents and caregivers about the risk of cough and cold medications.

Halmo and her team also recommend that the medical community and child welfare advocates be on the lookout for medication use as a source of child abuse.

At home, preventing accidental ingestion could go along with other practices already engrained in the minds of many, Osterhoudt says

"We know to change the clocks in the spring and fall and make sure your smoke detector and carbon monoxide detector has fresh batteries, but maybe it's also a good time to look at medicines in the house."

In other words, after you change the clocks, it's time to take inventory of medications around the house, and if they're no longer in use, safely dispose of them.

The American Academy of Pediatrics offers guidelines on the safe home storage of medications to keep them out of reach of children and the use of protective caps on drugs.

Source
Pediatrics: "Pediatric Fatalities Associated With Over-the-Counter Cough and Cold Medications," "Pediatric Poisoning Fatalities: Beyond Cough and Cold Medications."

Akina mama k na baba k Habari za leo.Ukiangalia kwenye picha hiyo hapo chini kuna swali la msingi ambalo wengi hutamani ...
20/01/2021

Akina mama k na baba k Habari za leo.
Ukiangalia kwenye picha hiyo hapo chini kuna swali la msingi ambalo wengi hutamani kulifahamu. Aliliuliza mama k team march anaitwa Anne Bosko

SWALI: Je kuna ukweli wowote mama mjamzito akila kipolo siku ya kujifungua hutoa haja kubwa kwa wingi?

MAJIBU: Hii hoja ya kula kipolo haina ukweli wowote, bali ni maneno na sababu watu wanazoambiana tu mtaani. Na ni kweli yanasikilizwa sana kuliko sababu za kitaalamu.

SABABU YA KUTOA HAJA KUBWA: Iko hivi, mama anapokuwa kwenye uchungu yaani labor, unapofika wakati wa kusukuma mtoto, misuli inayotumika kufunga njia ya haja kubwa ndiyo hiyo hutumika pia kubana uke. Hivyo wakati wa kusukuma mtoto, misuli hii hulegea ili kuruhusu uke kutanuka na kuruhusu mtoto kupita.
Hivyo inapolegea uke na njia ya haja kubwa vyote hubaki bila kufungwa, yaani wazi. Kumbuka wakati wa kusukuma mtoto mama huhisi k**a anataka kusukuma haja kubwa. Na k**a mama hakwenda haja kubwa kabla ya uchungu kuchanganya, ndiyo chanzo cha mama kusukuma haja kubwa pamoja na mtoto kwa pamoja. Na hii ni baada ya kichwa cha mtoto kukandamiza njia ya haja kubwa na haja kutoka pia.

Hivyo majibu sahihi ni hayo. Mama yeyote anaweza kupatwa na jambo hili.

Kumbuka ku like na ku comment page hii kwa taarifa zaidi kila tukitoa elimu upate taarifa.

04/01/2021

Swali: je mama mjamzito akinywa chai ya moto sana humuunguza mtoto aliye tumboni?

Jibu: hapana

Hoja hii huja baada ya kuwa na maneno yanayosikiwa mtaani kwamba mama mjamzito akinywa chai ya moto sana humuunguza mtoto aliye tumboni, eti ndiyo maana mtoto hucheza, na kupelekea mtoto kuzaliwa na mabaka.

Hili jambo halina ukweli wowote ni maneno ya mtaani ambayo hayana ukweli wala uhusiano na uhalisia wa jambo husika. Hili jambo lingekuwa na ukweli basi hakuna mama ambaye angekuwa akiruhusiwa kunywa chai ndani ya chumba cha leba ( labor). Maana kwa kufanya hivyo mtoto huyo angezaliwa na vidonda balaa.
Hii hoja ni ya uongo kwa sababu zifuatazo.

1. Mfumo wa chakula ambapo chai hupita ni tofauti kabisa na mfumo wa uzazi ambapo mtoto anakaa. Hivyo hata chakula unachokula mtoto hali kwa mdomo chochote ulacho wewe. Kutokana na kwamba mfumo wa chakula joto lake haliwezi mfikia mtoto, hawezi kuunguzwa na chai ambayo hagusani nayo. Mtoto kuzaliwa na mabaka ni swala lingine la kitaalamu zaidi.

2. Swala la mtoto kuchangamka na kucheza unapokuwa ukila ni swala lingine na siyo kwamba huwa anaungua ndo maana huwa anarukaruka.
Iko hivi mtoto awapo tumboni mwa mamaye, huhisi mabadiliko ya hali ya furaha au ya huzuni anayoipata mama yake. Hivyo mama akifurahi mtoto naye huruka tumboni kwa furaha, na mama akihuzunika vile vile mtoto huhuzunika tumboni.
Mama akipata chakula nafsini mwake hufurahi na mtoto pia hufurahi na kurukaruka ama kucheza. Hii ndiyo sababu kuu.

Hilo lilikuwa swali la mmoja wetu.
Karibuni kwa maswali zaidi.

Like page hii kisha ingia kwenye page yetu na kuuliza maswali utajibiwa wakati wowote.

Usipite bila ku like page hii k**a imekupa ufahamu wa kitaalamu.

04/01/2021

Akina mama wajawazito pamoja na mlio na watoto wachanga, maswali mliyo nayo na maneno ya mtaani mnayoyasikia ulizeni kwa wataalamu mpate majibu yaliyo sahihi.

Mimi ni mtoa huduma wa Afya upande wa mama na mtoto. Nipo tayari kuwajibu maswali yenu mnayojiuliza na kuulizana mitandaoni maana naona kuna baadhi yenu wanawajibu kulingana na maneno yanayosikiwa mtaani ambayo hayana ukweli wala uhusiano na uhalisia.

Karibuni kwa maswali yoyote na wakati wowote.

Share page hii kwa akina mama wote wapate ufahamu.

11/11/2020

Afya ndiyo mtaji wa kwanza

MAISHA KATIKA KIPINDI CHA UGONJWA WA CORONAMaisha ni lazima yaendelee katika kipindi hiki cha ugonjwa huu wa Corona. COV...
26/05/2020

MAISHA KATIKA KIPINDI CHA UGONJWA WA CORONA

Maisha ni lazima yaendelee katika kipindi hiki cha ugonjwa huu wa Corona. COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi, hivyo sii ugonjwa wa kuisha leo wala kesho

Tumshukuru Mungu kwa kuwa nchini kwetu Tanzania maambukizi ya ugonjwa huu yamepungua kwa mujibu wa takwimu rasimi za serikali.
Zingatia maana ya maneno hayo, ni maambukizi ndiyo yamepungua lakini ugonjwa bado upo. K**a ugonjwa bado upo kumbuka tena ya kuwa huu ugonjwa ni sawa na vita ya kupambana na adui asiyeonekana.

Katika vita hii askari wa msitari wa mbele ni mimi na wewe, uliye kijana, uliye mzazi, uliye mzee na hata mtoto, na hii haina kumwangalia jirani wala rafiki. Kila mmoja yuko nafasi sawa ya kushambuliwa maadamu sote tuko msitari wa mbele katika kikosi cha mbele. Adui Corona atalipua kutokea upande wowote na yeyote kati yetu anaweza ambukizwa mda wowote.

Kwa kusema hayo nifupishe kwa kusema kuwa vaa siraha zako zote yaani tahadhari za afya kujikinga na ugonjwa huu wa Corona maadamu sote tuko hatarini kuripuliwa na maambukizi ya ugonjwa huu.
Hili ni Janga, MCHUMA JANGA HULA NA WA KWAO, yaani ukiambukizwa utawaambukiza ndugu, jamaa, marafiki, na mwisho wa siku utaigharimu familia yako kwenye matibabu.

Tuache tabia ya kuishi kwa msisimko au mhemuko. Tusiishi kwa kufuata upepo, ugonjwa uliposhamili kila mtu alikuwa makini kujikinga kwa kufuata tahadhari zote, baada ya taarifa za maambukizi kupungua watu tumeacha tahadhari zote na mikusanyiko na kujiachia mitaani k**a kawaida. Kwa mtindo huu sii wa maisha chanya, bali ni maisha ya mkumbo.
COVID-19 ni changamoto iliyokuja ili tuishi kwa usitaarabu unaofaa na wa kiafya zaidi. Kumbuka kwa kunawa na kujikinga na Corona imepelekea magonjwa ya mripuko k**a kipindupindu na kuharisha kupungua.
Hivyo kwa vile huu ni usitaarabu wa kiafya basi tuufuate, tusiuone k**a mzigo ndiyo uzima wetu na afya ya jamii yetu katika maisha haya.
Badili mtazamo na ujisikie huru kufanya jambo jema hata k**a ukiwa pekee yako katika maelfu ya watu. Vaa barakoa yako katika mikusanyiko hata k**a uko pekee yako, usiiweke mfukoni. Fika mahali nawa hata k**a wenyeji hawanawi mikono ijapo wameweka maji. Na mengine k**a hayo.

Mambo yafuatayo yataendelea katika maisha lakini tahadhari ni lazima.

1. KILA MMOJA WETU ANAENDELEA NA SHUGHULI ZAKE.
Tutakaribiana na mikusanyiko ilishaanza.
2. TULIOKUWA MASOMONI TUNAREJEA MASOMONI.
Tuliwamiss marafiki, utataka ujue atokako ilikuwaje
3. WANAMICHEZO TUNAREJEA KWENYE MASHINDANO NA USHAHABIKI.
Tutashangilia na kujaa kwenye vibanda vya kuonyesha matangazo ya michezo
4. WAFANYAKAZI TUNAREJEA OFISINI.
Kuna kujikusanya na wenzako kubadilisha mawazo hasa maeneo ya kupata vyakula na kupumzika
5. WANAFAMILIA TUNATAWANYIKA ASUBUHI KUANZIA WAZAZI HADI WATOTO NA TUTAKUTANA TENA JIONI AU USIKU.
Tutachangamana na watu toka familia mbalimbali ambazo hatujui hali zao kiafya.

Ni katika shughuli hizi ambapo tunapaswa tusisahau kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kutakasa mikono, kudumisha umbali angalau mita 1 kutoka kwako na mfanyakazi mwenzio au rafiki yako, epuka salamu za kushikana mikono na kukumbatiana, tumia kupunga mkono inapobidi.
MZAZI HAKIKISHA UNAAGANA NA MWANAO ANAPOTOKA KWENDA SHULE NA MKUMBUSHE KILA SIKU ACHUKUE TAHADHARI KUJIKINGA NA COVID-19.
Kumbuka yeyote kati yetu ni mhisiwa wa kuambukiza au kuambukizwa.

KARIBU KWA MAONI.

11/05/2020

UKIWA K**A MDAU WA UKURASA HUU TUNAKUPA NAFASI YA UPENDELEO:

UNGEPENDA KUJIFUNZA NINI KATIKA NYANJA YA AFYA?

COMMENT UKITAJA UNACHOHITAJI KUJIFUNZA KUPITIA UKURASA HUU. NASI TUTAANZA KUFUNDISHA KULINGANA NA HITAJI LAKO.

TAFADHARI TAJA TU UNACHOHITAJI KUJIFUNZA KWENYE AFYA.

ANDIKA HAPA
👇👇👇👇👇👇

03/05/2020

Ahsanteni sana wadau wetu wote katika page yetu hii.
Heshima kwenu.
Tuendelee kuitangaza page yetu kwa wengine marafiki zetu.
🤝🤝

23/04/2020

JINSI YA KUNAWA MIKONO.
Katika kipindi hiki cha gonjwa hili la COVID-19, kunawa mikono ni miongoni mwa silaha za kupambana na kujikinga na kuenea kwa ugonjwa huu kupitia mikono yetu. Hivyo kuna mambo ya msingi ya kuzingatia unaponawa mikono yako.

Kila mmoja wetu anaponawa mikono anahitaji uhakika ya kwamba mikono yake imekuwa safi kabisa bila uchafu wala mimelea vya magonjwa.

Kunawa mikono si kitendo cha haraka, bali ni kitendo kinachohitaji utulivu na uhakika ili kunufaika na mda ulioutumia kunawa mikono yako.

Katika video hii imeelezwa hatua kwa hatua ni kwa namna gani ujihakikishie kuwa umenawa mikono yako vizuri na ni safi kwa ajili ya kuendelea na shughuli zako.

ANGALIA VIDEO HII UJUE UNAKOSEA WAPI UNAPONAWA MIKONO AU NI SEHEMU GANI UNAZIACHA BILA KUZISAFISHA.

Kumbuka like, comment, share, au toa mapendekezo, Ili kila mafundisho yanapotolewa yakufikie kiurahisi

COVID-19 NI TAUNI HATARI SANA.SOMA MATHAYO 24:7-8 na luka 21:10-11Suruhisho katika vita hii dhidi ya COVID-19 ni kujiten...
13/04/2020

COVID-19 NI TAUNI HATARI SANA.
SOMA MATHAYO 24:7-8 na luka 21:10-11

Suruhisho katika vita hii dhidi ya COVID-19 ni kujitenga mbali na muingiliano au mkusanyiko wa watu. Kwa kila sababu uliyonayo ya kutaka kutoka nyumbani, itarejea kwenye jibu kwamba baki nyumbani.

BAKI NYUMBANI, UWE SALAMA.

Ama hakika tuwe waaminifu na kuwasaidia hawa watoa huduma za Afya, hakikisha ufikapo maeneo ya hospital FUATA TAHADHARI ...
12/04/2020

Ama hakika tuwe waaminifu na kuwasaidia hawa watoa huduma za Afya, hakikisha ufikapo maeneo ya hospital FUATA TAHADHARI ZOTE ILI USIWAAMBUKIZE WAHUDUMU WETU HAWA.

COVID-19Hiki ni kifupi cha maneno haya CORONA VIRUS DISEASE, Erupted IN 2019.KINGA DHIDI YA UGONJWA UNAOSABABISHWA NA VI...
23/03/2020

COVID-19
Hiki ni kifupi cha maneno haya CORONA VIRUS DISEASE, Erupted IN 2019.

KINGA DHIDI YA UGONJWA UNAOSABABISHWA NA VIRUSI JAMII YA CORONA.

Dumisha haya yafuatayo ili kujikinga katika ngazi kuu 3; wewe mwenyewe, familia yako na jamii yako.

KWANZA; JILINDE WEWE MWENYEWE
Fanya yafuatayo ili kujikinga dhidi ya hii homa ya njia ya upumuaji inayosababishwa na kirusi jamii ya Corona:

1. Nawa mikono yako kwa maji tiririka na sabuni kiuhakika mara kwa mara.
- Utaniuliza, kunawa mikono kiuhakika ni namna gani?
- Jibu, ni kunawa kwa kusugua viganja vya mikono, kisha nyuma ya viganja, kisha kati kati ya vidole yaani k**a unasugua kidole kimoja baada ya kingine, kisha safisha kucha zako yaani ncha za vidole vyako.
Nawa nikono yako hadi juu karibia na kiwiko.

2. Nawa kwa kutakasa mikono, ukitumia dawa maalumu ya kuua vimelea vya mikononi, tumia vitakasa mikono (sanitizer).
K**a hujanawa kwa maji na sabuni, ndipo tumia sanitizer, ila usitumie maji na sabuni hapo hapo tena ukatumia sanitizer. Tumia kimojawapo ulichonacho wewe.

3. Usijiguse usoni, mdomo, pua wala macho kwa mikono ambayo sii safi, jitahidi kwa kadiri iwezekanavyo. Ukihitaji kufanya hivyo hakikisha umenawa mikono kwanza ndipo ujiguse uso au ujikune usoni. Hivyo utamaduni wetu wa kukuna uso, pua, mdomo, kidevu nk tuuepuke kwa kipindi hiki cha mripuko.

4. Kaa mbali na mtu anayekohoa au anayepiga chafya angalau umbali wa mita 2 yaani hatua zako 2. Hii itaepusha kugusana nae na hata akikohoa au kupiga chafya, basi matone ya maji maji toka mdomoni au puani mwake hayataweza kukufikia.

5. Epuka salamu za kugusana kwa kushikana mikono au kukumbatiana. Virusi hawa wa Corona huenea kwa njia ya kugusa zaidi ya njia ya hewa, hivyo unaposisitizwa kunawa mikono siyo mtindo bali ndiyo kinga kuu ili kuzui kuwasafirisha kutoka mtu mmoja hadi mwingine na kutoka eneo moja hadi lingine. Unaeshikana nae mkono hujui kaanzia kwa nani, pengine ameshasalimiana na mgonjwa wa Corona, atakuambukiza wewe, nawe utawachua mikononi mwako na kuwaambukiza wengine utakao salimiana nao kabla hujanawa. Hivyo kunawa mikono hupunguza mzunguko huo.

PILI; LINDA FAMILIA YAKO
Baada ya kuangalia wajibu wako ili kujilinda binafsi, sasa tuangalie wajibu wako ili kuilinda familia yako na wote uwapendao. Fanya yafuatayo;

1. Usikohoe au kupigia chafya kwenye viganja vya mikono yako.
Tumia karatasi maalumu yaani tishu (tissue papers) kufunika mdomo na pua, unapopiga chafya au kukohoa. Kisha tupa hiyo tishu kwenye chombo cha taka (dustbin).
Hii itazuia kuwabeba wale virusi vya Corona mikononi mwako, hivyo mikono yako itabaki salama, na mwanafamilia wako akigusa vitu, vifaa au vyombo ulivyovigusa wewe hawezi pata maambukizi. Kwa kufanya hivyo umeilinda familia yako.

2. Usikae wala kutembelea maeneo yenye msongamano wa watu. Ni heri kubaki nyumbani k**a huna sababu ya lazima ya kukufanya utoke nyumbani. Katika msongamano hujui ni nani aliyeambukizwa ugonjwa huu,wala hujui ni nani amekuwa na hayo maambukizi. Maana anaweza kuwa ameambukizwa ingawaje bado hajawa na dalili za wazi wazi.
K**a ulitoka nyumbani ukaenda nje ya makazi yenu, basi ukirudi nawa mikono yako kabla hujaingia ndani.

3. Vaa balakoa (face mask) k**a unaumwa, au unasikia dalili za ugonjwa huo, au k**a unamhudumia mgonjwa wa aina hiyo hasa kwa wale watoa huduma za Afya. Usivae mask kiholela k**a huumwi, na k**a unaumwa vaa mask yako nenda kituo cha afya karibu yako au piga namba elekezi zilizotolewa na wizara ya Afya.

TATU; LINDA JAMII YAKO
Baada ya kuangalia wajibu wako ili kuilinda familia yako, sasa tuangalie wajibu wako ili kuilinda jamii yako pia. Fanya yafuatayo;

1. K**a unaumwa magonjwa mengineyo tafadhari tafuta huduma ya afya ukatibiwe. Tibiwa mafua na kikohozi k**a kawaida ikiwa haviambatani na shida ya upumuaji.
Kumbuka kuna mafua na kikohozi cha kawaida k**a ulivyowahi kuugua ni tofauti na dalili za Corona.

2. K**a unajisikia kuumwa, na dalili zako ni sawa na za ugonjwa wa Corona k**a homa, kukohoa, mafua yanayoambatana na shida ya kupumua na kifua kuuma au kubana, baki nyumbani usitoke kutembea tembea nje, piga simu kwa huduma za afya na fuata ushauri utakaopewa. Kumbuka kuvaa balakoa yako na jiepushe kugusana na watu kadiri iwezekanavyo.

3. Usipagawe wala kupagawisha wenzako kwa ujumbe uliotumiwa kiholela. Hakikisha unatilia maanani taarifa rasmi tu zinazotolewa na wizara ya Afya au watoa huduma za Afya pekee. Achana na wanahabari wengineo ambao hujui chanzo cha taarifa zao.

KARIBUNI KWA MASWALI AMBAPO HUJAELEWA, MAONI AMBAPO KUNA NYONGEZA.

SAMBAZA KWA MARAFIKI NA MAKUNDI TOFAUTI ULIYOPO, ILI SOTE TUWE NA UELEWA SAWA NA KUEPUKA KUPANIKI NA KUPANIKISHANA.

AHSANTNI KUELEWA.

Namba za kupiga simu bure endapo utaona una dalili au utaona mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Korona        0800110124   ...
17/03/2020

Namba za kupiga simu bure endapo utaona una dalili au utaona mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Korona

0800110124
0800110125
Namba hizi kupiga Ni bure hata k**a hauna salio kwenye simu yako.

DALILI ZA UGONJWA WA CORONA

Dalili zionekanazo mara kwa Mara:
• Homa
• Kikohozi kibichi
• Uhemaji wa tabu
• Maumivu ya mwili
• Kuuma kwa koo mfano wa
matonses (tonsillitis)
• Kukosa hamu ya kula

Dalili za mara chache:
• Kuhara
• Kutapika
• Kichwa kuuma
• Kukohoa damu
• Maumivu ya kifua

Nani hupatwa na korona?

• Watu wote (wakike kwa kiume) waweza
kudhurika na korona
• Wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa Zaidi.
• Wazee pia wapo katika hatari kubwa kupatakorona kwani wana kingamwili hafifu.

KINGA:

• Kuosha mikono vizuri kwa maji safi na sabuni
• Tumia vikinga pua na mdomo (masks) ikiwa unahudumia washukiwa wa korona.
• Epuka kugusa na kurekebisha kikinga mdomo na pua (mask) na uso.
• Zingatia walau umbali wa futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona
• Hakuna chanjo mpaka sasa

Kirusi cha korona katika mwili wa
binadamu:

• Huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona (incubation perion)
• Huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au kugusana moja kwa moja.
• Epuka kusalimiana kwa mikono

LEO TUZUNGUMZIE  KIRUSI CHA KORONA KWA KINA.JAMBO UNALOPASWA KUJUA; JINSI VIRUSI VYA KORONA VINAVYOSAMBAA/KUENEA.Mtu ali...
16/03/2020

LEO TUZUNGUMZIE KIRUSI CHA KORONA KWA KINA.

JAMBO UNALOPASWA KUJUA; JINSI VIRUSI VYA KORONA VINAVYOSAMBAA/KUENEA.

Mtu aliyeshambuliwa na virusi hivi akikohoa au kupiga chafya, matone madogo madogo ya majimaji au mate huruka kutokea mdomoni na puani mwake yakiwa yamebeba virusi kuingia hewani.
Utaambukizwa pale ambapo hao virusi wataingia mdomoni mwako, au puani au machoni.

Hivyo ukimuona mtu anayekohoa, kupiga chafya hadharani au mbele yako, au anayeumwa, Basi wewe chagua kufanya yafuatayo:

1. Simama mbali naye k**a umbali wa hatua 3 za mtu mzima. Hii itakusaidia usipatwe na matone yenye virusi yatokayo kwa mgonjwa, kwa maana haya matone kutokana na kuwa na maji maji huwa na uzito unaosababisha kudondoka chini wala hayaendelei kuelea hewani. Hivyo matone hayo hudodoka umbali wa nusu hatua hadi hatua 2 za mtu mzima kutoka aliposimama mgonjwa aliyepiga chafya.

2. Mpe kifaa/kitambaa maalumu cha kufunika pua na mdomo ( kifunika pua/mask). Kitasaidia yeye kukohoa na kupiga chafya ndani ya mask lakini zile chembe chembe za mate hazirudi tena kusambaa nje. Hivyo wewe amabaye haujaambukizwa utabaki salama, na kila mmoja wenu aliye karibu pia atabaki salama.

KIUJUMLA
Epuka msongamano au mkusanyiko wa watu au usichangamane na watu bila sababu ya lazima au ya muhimu kufanya vile. Kwani watu wanaweza kuwa wameshapata virusi hivi vya korona lakini bado hawajaanza kuonesha dalili yoyote.
Kumbuka mtu akishakuwa na virusi hivi ana uwezo wa kuambukiza wengine hata k**a yeye bado hajaanza kuonesha dalili yoyote ya ugonjwa.
Hii ndiyo sababu ya msingi ya kukutahadharisha kutoingia kwenye mikusanyiko ya watu bila sababu ya lazima.

LAKINI PIA mate ya mgonjwa yanaweza kuwa kwenye vitu vifuatavyo k**a atavigusa kwa mkono wake; kwenye mikono yao wenyewe, vitasa vya milango, sehemu ya kushika kwenye daladala au usafiri, kalamu, vipanya vya compyuta, vifaa vingine vya umeme k**a simu, vikombe, vyombo vingine vya chakula, vibonyezeo (button) vya lift, kingo za ngazi na hata nyuma/nje ya mask uliyovaa wewe mwenyewe ambaye hujaambukizwa nk.
Endapo utagusa miongoni mwa vitu hivyo ambavyo kavigusa mgonjwa alafu ukashika pua, macho, uso wako, au uso wa mwenza wako, wote mnaweza kuambukizwa na kuugua.

NI NINI UFANYE
Kwa kuwa Virusi hawa wanaweza kubaki kwenye vitu kwa mda wa masaa 12, Osha mikono yako kwa maji na sabuni na uoshe hivyo vitu vyote kwa maji na sabuni ili kuondoa virusi waliokuwa wamebaki hapo.

ANGALIZO
Tahadhari ya kuepuka magonjwa na kubaki salama inasema hivi "KILA MTU UNAYEMWONA MBELE YAKO MCHUKULIE K**A NI MGONJWA ILI UCHUKUE TAHADHARI UNAPOKUWA KARIBU NAYE.
Hivyo kwa tishio la korona pia itatakiwa iwe hivyo.

Kwa wale wanaohitaji kiingereza pia, nimeambatanisha kwa mfumo wa picha hapa chini.

Ahsante sana, karibu kipindi kinachofuatia kinachoelezea kuhusu NJIA MADHUBUTI ZA KUJIKINGA DHIDI YA KORONA

Like, comment, share, weka pendekezo lako la wapi panahitaji marekebisho.

MWITIKIO WAKO NA UTAKAO WASHIRIKISHA ELIMU HII NDIYO VITATUPA NGUVU YA KUENDELEA NA VIPENGELE VINGINE KUHUSU KORONA

UJUMBE KUTOKA UNICEF JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA.
10/03/2020

UJUMBE KUTOKA UNICEF JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA.

FURAHA NI KIINI CHA MAISHA BORA NA AFYA NJEMA.Kuwa na furaha ni hatua moja kubwa ya kumiliki Afya njema kwa kila mmoja w...
13/02/2020

FURAHA NI KIINI CHA MAISHA BORA NA AFYA NJEMA.
Kuwa na furaha ni hatua moja kubwa ya kumiliki Afya njema kwa kila mmoja wetu. Ukiwa na furaha katika maisha yako, unaepuka magonjwa mengi ya akili, na hivyo umejikinga dhidi ya magonjwa na mtenguko wa kiafya.
HERI FURAHA BADALA YA UTAJIRI:
Hata uwe tajiri bila furaha bado ni kazi bure.
Hivi vitu 6 ni baadhi tu ya mambo yanayochangia furaha na afya njema.

Address

Magomeni
Dar Es Salaam

Opening Hours

Friday 18:00 - 00:00
Saturday 00:00 - 18:00

Telephone

+255754650106

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Ya Jamii Kwa Wote posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya Ya Jamii Kwa Wote:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram