Naimulika Afya

Naimulika Afya Aina ya Vitu Unavyo kula mara kwa mara + Mtindo wako wa Maisha Ndio Matokeo ya Afya yako Leo /Kesho.

To Day Another One ✅Mafanikio yako mafanikio yangu💪.Yani nami huwa na Furaha upatapo Matokeo.Naimulika Afya 0718 750 220...
02/05/2025

To Day Another One ✅

Mafanikio yako mafanikio yangu💪.

Yani nami huwa na Furaha upatapo Matokeo.
Naimulika Afya
0718 750 220
Afya-Coffee.
0718 750 220

Kisukari. ni kundi la magonjwa ambayo husababisha sukari nyingi kwenye damu (glucose ya juu ya damu).AINA ZA KISUKARI.i/...
02/05/2025

Kisukari. ni kundi la magonjwa ambayo husababisha sukari nyingi kwenye damu (glucose ya juu ya damu).

AINA ZA KISUKARI.

i/Type 2 diabetes. aina ya pili ya kisukari ambapcho kongosho hutengeneza insulini kidogo kuliko kawaida, hupelekea mwili kuwa kukizana na insulini.

ii/Type 1 diabetes. ni hali ambayo kongosho hustop kuzalisha insulini kabisa.

iii/Prediabetes ni hali ambayo kiwango cha sukari mwilini kinakuwa kipo juu isipo chukuliwa tahadhari na matibabu mapema huelekea kuwa na kisukari aina ya pili.

iv/Gestational diabetes. ni aina ya sukari ya juu ya damu inayoathiri wanawake wajawazito.

DALILI ZA KISUKARI.

-Kuhisi kiu kuliko kawaida.

-Kukojoa mara kwa mara.

-Kupunguza uzito bila sababu.

-Kuhisi uchovu na udhaifu.

-Kuhisi kukasirika au kuwa na mabadiliko mengine ya mhemko.

-Kupata maambukizi mengi ya fizi, ngozi na maambukizi ya ukeni.

-Kuwa na uoni hafifu.

-Kuwa na vidonda vinavyo chelewa kupona.

-Dalili za kuwa na ganzi mikononi au miguuni.

Wapendwa Dalili hizi☝️ ni viashiria vya ugonjwa wa kisukari, uwonapo dalili hizi fika hospitalini mapema kufanya vipimo kuthibitisha ili kupata ushauli au wa kukontro au kuchukua hatua za matibabu haraka.

Kesho tutaendelea na sehem ya pili kujifunza chanzo cha kisukari na athari zake.

Iwapo una tatizo linakusumbua wewe ndugu jamaa au rafiki yako wasiliana nasi
Rich ☎️🥏0718750220
Afya-Coffee.
0718 750 220

FAHAM KUHUSU PROSTATE CANCERProstate cancer ni Saratani inayo tokea kwenye tissue za tezi dume.DALILI ZA SARATANI YA TEZ...
29/04/2025

FAHAM KUHUSU PROSTATE CANCER

Prostate cancer ni Saratani inayo tokea kwenye tissue za tezi dume.

DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME.

_Dalili za saratani ya tezi dume zinaelekea kufanana na Dalili za kupanuka kwa tezi dume_

Dalili za saratani ya tezi dume.

•Kupata haja ndogo mara kwa mara hasa usiku.

•Kuhisi maumivu au kuungua kwenye njia ya haja ndogo wakati wa kukojoa.

•Dalili za damu kwenye mkojo au shahawa.

•Kujisaidia mkojo zaifu.

•Ugumu wa kuanza au kuacha kukojoa.

•Maumivu chini ya mgongo, kwenye hips au mapaja.

•Kupoteza hamu ya kula.

•Upungufu wa nguvu za kiume.

•Kupungua uzito bila sababu

•Maumivu ya mifupa.

MUHIM SANA

_Upatapo Dalili tajwa hapo juu vyema ukafika Hospital kwa ajili ya vipimo ili kuthibitisha na kupata matibabu Haraka_

VYANZO VYA SARATANI YA TEZI DUME.

✓Kuvurugika Kwa homoni.

✓Mabadiliko ya DNA kwenye seli za tezi dume

✓Kurith kutoka kwa familia.

✓Umli wa utuuzima wa umli kuanzia miaka 50+

✓Unene Kupitiliza

✓Uvutaji sigara.

🙋🏽‍♂️Epuka vyanzo vya tatizo uwishi salama na uwonapo Dalili za saratani ya tezi dume fika hospital upesi kufanyiwa uchunguzi

Tunayo tiba ya kutanuka kwa tezi dume na Saratani ya tezi dume.

Iwapo una tatizo na unaitaji piga number
Rich ☎️🥏0718750220

DALILI ZA KUPANUKA KWA TEZI DUME (Prostate Enlargement).-Mkojo kuwa na damu-Kushindwa kuuzuia mkojo (mfano wakati wa kuc...
29/04/2025

DALILI ZA KUPANUKA KWA TEZI DUME (Prostate Enlargement).

-Mkojo kuwa na damu

-Kushindwa kuuzuia mkojo (mfano wakati wa kucheka au wakati wa shughuli zingine).

-Baada ya kumaliza kukojoa inatokea hali ya mkojo kuendelea kuvuja kidogo kidogo wenyewe.

-Kupata ugumu wa mkojo kutoka unapo anza kukojoa.

-Pindi unakojoa unatumia nguvu kusukuma mkojo utoke kuliko kawaida yake.

-Kuwa na mtiririko zaifu wa mkojo.

-Baada ya kumaliza kukojoa unasikia dalili za uwepo wa mkojo kwenye kibofu.

-Kushindwa kushiriki tendo na mwenza ipasavyo.

MUHIM UFAHAM
Dalili zote hizi hazitoshi kudhibitisha kuwa una tezi dume, nimuhim kudhibitisha, kwakufanyiwa vipimo.

WALIOPO ATALINI KUPATA TATIZO KUPANUKA KWA TEZI DUME.

1•Watu wazima wenye umli kuanzia miaka 50 Kuendelea.

2•Walio na Babu Baba au kaka alie wahi kuwa na tatizo la kupanuka kwa tezi dume.

3•Wenye kisukari,

4•Wenye magonjwa ya moyo na pressure.

5•Wenye Unene kupitiliza na wanao tumia muda mwingi kukaa chini.

MATIBABU.

Matibu ya kupanuka kwa tezi dume yatategemea na chanzo cha tatizo unaweza pewa dawa au ushauli au kufanyiwa upasuaji.

iwapo una tatizo wewe ndugu jamaa au rafiki yako wasiliana nasi
Rich ☎️🥏0718750220
Afya-Coffee.

TEZI DUMETezi dume (Prostate) ni kiungo kidogo chenye umbo la jozi/njugu kinacho patikana katika mfumo wa uzazi wa mwana...
29/04/2025

TEZI DUME
Tezi dume (Prostate) ni kiungo kidogo chenye umbo la jozi/njugu kinacho patikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume ipo chini kidogo ya kibofu cha mkojo na mbele ya njia ya haja Kubwa (re**um).

-Kila mwanaume ana tezi dume ila hugeuka kuwa tatizo tezi pale tezi dume inapo ongezeka ukubwa kuliko size yake ya kawaida tunasema (prostate enlargement).

CHANZO CHA KUPANUKA KWA TEZI DUME (prostate enlargement)

-Maambukizi ya bacteria

-Mabadiliko ya hormones.

-Mashambulizi ya kinga ya mwili.

-Historia ya kuugua uti.

-Kurith

-Kupata ajari kwenye eneo husika la nyonga.

-Msongo wa mawazo na kubadilika kwa mtindo wa maisha.

MUHIM UFAHAM PIA

Kazi ya tezi dume ni kutoa majimaji ambayo huchanganyikana na mbegu za kiume kutoka kwenye korodani ili kutengeneza shahawa.

Kwenye mchakato huo misuli ya tezi dume pia inahusika kuhakikisha shahawa zinashinikizwa kupita kwa nguvu kwenye urethra kisha kutolewa nje wakati mwanaume unapo fika kufika kileleni.

Swali ni je mtu anaweza kuwa na prostate enlargement na isiwe prostate cancer? Jibu ni ndio.

Prostate cancer ni Saratani inayo tokea kwenye tissue za tezi dume. tutaliangazia hili siku sikuzijazo endelea kujifunza🤝

Iwapo una tatizo linakusumbua lolote lile iwe mama Baba au kijana wasiliana nasi kupata matibabu kutoka kwetu ama ushauli wa Bure Piga Rich ☎️🥏+255 718 750 220
Afya-Coffee.

*UVIMBE KWENYE MFUKO WA MAYAI (OVARIAN CYSTS).*Ovarian cyst.Ni uvimbe ulio jaa maji maji unaotokea ndani au nnje ya mfuk...
29/04/2025

*UVIMBE KWENYE MFUKO WA MAYAI (OVARIAN CYSTS).*

Ovarian cyst.
Ni uvimbe ulio jaa maji maji unaotokea ndani au nnje ya mfuko wa mayai ya mwanamke (ovari).

Kwa kawaida vimbe hizi hupotea zenyewe Baada ya miezi kazaa na zisipo ondoka huweza kusababisha matatizo kwenye mfuko wa mayai au kuathili swala la uzazi kwa mwanamke kushindwa kushika mimba au kuwa zina haribika.

DALILI ZA OVARIAN CYST.

Baadhi ya dalili hizi ni kiashiria cha uwepo wa ovarian cysts.

•Kupata maumivu makali ya tumbo kipindi cha hedhi kabla au daada ya hedhi.

•Kupata maumivu makali eneo la nyonga kushoto au kulia au pande zote.

•kupata maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

•Kutokwa na damu ukeni kipindi ambacho sio cha hedhi.

•Kubanwa na mkojo mara kwa mara.

•Kupata maumivu makali chini ya mbavu mbavu, upande mmoja au pande zote

•Kupata haja kubwa kwa shida na maumivu makali.

•Kujisikia kushiba Kuliko Kawaida baada ya kula kidogo.

•Kuongezeka uzito.

•Tumbo kuongezeka ukubwa (k**a mjamzito).

VISABISHI VYA OVARIAN CYST.

1•Mvurugiko wa homoni.

Ambapo unaweza Kutokana na madawa ya uzazi wa mpango, ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye chamical na sukari nyingi, mabadiliko ya mazingila na mtindo wa maisha.

2•Mvurugiko wa hedhi.

3•Utumiaji wa baadhi ya madawa ya kupevusha mayai.

4•Maambukizi kwenye mfumo wa mayai. yanayo tokana na Uti, pid, gono n.k

5•Kuwa na mafuta mengi (Unene).

6•Ugumba kushindwa kushika mimba.

TIBA YA UVIMBE OVARIAN CYSTS BILA KUFANYIWA UPASUAJI.

_Tunayo tiba ya ovarian cyst ambapo itakuchukua week mbili mpaka mwezi mmoja kupona kabisa._

_Iwapo tatizo lako litakuwa Kubwa zaid itakulazim Kuendelea na dose kwa muda wa miezi 2-3 na Kuendelea._

Matumizi ni rahisi na Salama kwa mtumiaji

kupata huduma zetu Rich ☎️🥏0718750220
Afya-Coffee.

FAHAM MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA KUVURUGIKA KWA HOMONI.•Kisukari •Rovu (goiter)•Tezi dume (Prostate cancer)•Unene kup...
29/04/2025

FAHAM MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA KUVURUGIKA KWA HOMONI.

•Kisukari

•Rovu (goiter)

•Tezi dume (Prostate cancer)

•Unene kupitiliza

•Hedhi zisizo za kawaida.

•Fibroids (Uvimbe kwenye kizazi)

•Endometriosis

•Ugumba.

•Acromegaly/gigantism(kuwa mlefu sana)

•Haipakotism (Addison's disease)

•Ugonjwa wa Cushing.

•Ugonjwa wa kuzoofika kwa mifupa.

•Pituitary adenoma (Uvimbe kwenye tezi ya pituitary ili kwenye ubongo)

•Polycystic o***y syndrome (PCOS)/Ovarian cyst.
(Uvimbe kwenye mfuko wa mayai).

Tunazo tiba maalumu zinazo tibu na kuondoa tatizo la Kuvurugika Kwa homoni, iwapo una tatizo la Kuvurugika Kwa homoni na mengineyo wasiliana nasi kupata Suluhisho.
Rich ☎️🥏0718750220
Afya-Coffee.

ILI KUONDOKANA NA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME PENDELEA KULA HIVI.1•Matunda matunda.✓Ndizi mbivu.✓Parachichi✓Tikiti maji✓com...
29/04/2025

ILI KUONDOKANA NA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME PENDELEA KULA HIVI.

1•Matunda matunda.

✓Ndizi mbivu.
✓Parachichi
✓Tikiti maji
✓comamanga
✓Berry

2•Nafaka kamili.

✓kula dona (ugali usio kobolewa)
✓ugali wa mhogo na mtama
✓Wali. tumia mchere wa kahawia na k**a unakula huu wa kawaida (mweupe)changanya na maharage na mboga mboga za majani
✓kula na nafaka zingine unazo zijua.

3•Kula mboga mboga za majani tofauti tofauti mara kwa mara.

4•Penda kula
✓karanga
✓korosho
✓almond
✓mbegu za maboga.

5•kula vyakula vya protein k**a vile.

✓mbaazi,dengu
✓samaki mchemsho
✓kuku kyenyeji mchemsho
✓mayai ya kuchemsha

6•Nyongeza.
✓Kunywa maji lita 1½-2
✓Tumia tangawizi ✓Kitunguu saumu
✓Fanya mazoezi
✓Tumia liven coffee ☕.

🫵🏽Epuka matumizi ya pombe na sigara, Soda, juice za makopo vyakula vyenye Sukari nyingi na mafuta mengi. Iwapo unatatizo lakiafya linakusumbua wasiliana nasi

Rich ☎️🥏0718750220
Afya-Coffee.

VISABABISHI VYA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA MWANAMKE•_kwa kawaida homoni hubadirika kipindi cha kubalee, wakati wa hedhi, u...
24/04/2025

VISABABISHI VYA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA MWANAMKE•

_kwa kawaida homoni hubadirika kipindi cha kubalee, wakati wa hedhi, ujauzito, na kipindi cha kufikia umli wa ukomo wa hedhi (menopause)._

_Vyanzo vingine vinavyo changia Kuvurugika Kwa homoni za mwanamke na kusababisha changamoto za kiafya._

1•Dawa za uzazi wa mpango na dawa za kuzuia mimba P2.

Huzalisha sumu/homoni zinazo ingilia homoni za asili za mwili kuzivuruga ili usipate mimba.

2•kuongezeka kwa sumu mwilini .

Huzuia, au kuingilia homoni asilia za mwili, kuathiri uzalishwaji wa homoni, kuashiria na utendakazi wa vipokezi vya homoni. Je unajua sumu unazipataje?

3•Lishe duni/Ulaji wa vyakula usio na tija.

Milo ya vyakula vilivyochakatwa, sukari nyingi na mafuta yasiyofaa inaweza kuathiri vibaya viwango vya homoni, wakati pia upungufu wa virutubisho muhimu kuchangia.

4•Stress.
Msongo sugu huinua viwango vya homoni ya cortisol, ambayo huingiliana na utendaji mwingine wa homoni k**a vile estrojeni, projesteroni, na homoni za tezi.

5•Unywaji pombe na uvutaji sigara.

Kukaa Karibu na wavutaji husababisha tatizo la Kuvurugika kwa homoni zako pia.

6•Unene kupita kiasi.

7•Kuzidi kwa sukari kwenye damu.

8•Miyonzi kwa ajili ya kutibu Cancer (Chemotherapy or radiation).

9•Matumizi ya Baadhi ya dawa zinazo tumika kutibu tatizo la mfadhaiko k**a vile.
-Amitriptyline.
-Amoxapine.
-Desipramine.
-Doxepin.

10•Kutopata usingizi wa kutosha.

11•Matatizo kwenye tezi.
Husababisha tezi kuto zalisha kiwango cha homoni kinacho takiwa.

kuzidi au kupungua kwa kiwango cha homoni hupelekea Kuvurugika kwa homoni.

Athali Kubwa ya Kuvurugika Kwa homoni kwa mwanamke ni kupata matatizo ya kushika au kuharibika kwa mimba mara kwa mara, matatizo ya hedhi, kuharibika kwa ngozi na kupata ugonjwa wa cancer.

Iwapo unahisi au unafaham una tatizo hili wewe ndugu jamaa au rafiki yako wasiliana nasi Rich ☎️🥏 0718750220
Afya-Coffee.

DALILI/MADHARA YA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA MWANAMKE.Kuvurugika Kwa homoni kwanamke kunaweza kusababisha kushindwa kushik...
24/04/2025

DALILI/MADHARA YA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA MWANAMKE.

Kuvurugika Kwa homoni kwanamke kunaweza kusababisha kushindwa kushika mimba au kuharibika kwa mimba mara kwa mara, zipo dalili nyingi zinazo ashiria kuvurugika kwa homoni kwa mwanamke.

1•Matatizo ya hedhi.

Kubadilika badilika kwa mzunguko, kupata hedhi ya mdamlefu, kiduchu, mabonge mabonge na hata kukosa hedhi n.k

2•kushindwa kushika mimba au mimba kuharibika mara kwa mara.

3•Maumivu ya nyonga, Ukavu ukeni na maumivu makali wakati wa tendo.

4•kupoteza au kupungua kwa hamu ya tendo.

5•Kuongezeka kwa hamu ya kula mara kwa mara au Kupoteza hamu ya kula

6•Kuongezeka au kupungua uzito.

7•Kujihisi kuchoka choka mara kwa mara.

8•Kubadilika badilika kwa moods na matatizo ya usingizi.

9•Kuharibika kwa ngozi kuwa kavu/kupata chunusi mapele na nanywele kupungua.

10•Maumivu ya kichwa na kipanda uso wakati wa hedhi

11•Huchangia Kupata endometriosis/fibroids/ovarian cyst

12•Kuvugika kwa homoni huchangia hatali ya kuongezeka kwa magonjwa ya Kisukari/unene na magonjwa ya moyo.

Iwapo unasumbuliwa na Baadhi ya dalili tajwa hapo juu wasiliana nasi nasi upate matibabu.
Rich ☎️🥏 0718 750 220
Pia wasaidie wengine kwa kuwapa habari zetu.
Afya-Coffee.

VYANZO VYA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA MWANAUME.Zipo sababu mbali mbali zinazo weza kusababisha tatizo la Kuvurugika kwa ho...
24/04/2025

VYANZO VYA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA MWANAUME.

Zipo sababu mbali mbali zinazo weza kusababisha tatizo la Kuvurugika kwa homoni za mwanaume.

1•Stress sugu.

Stress za mdamlefu zinaweza kusababisha viwango vya juu vya homoni ya cortisol kuzalishwa, ambayo inaweza kuingilia kati uzalishaji wa testosterone na michakato mingine ya homoni likawa tatizo.

2•Lishe duni/lishe isiyo kua na tija.

Lishe isiyofaa, haswa iliyo na vyakula vingi vya kusindika na sukari nyingi, inaweza kuchangia upinzani wa insulini na usawa mwingine wa homoni.

3•Kutokufanya mazoezi.

Mazoezi ya mara kwa mara ya kimwili ni muhimu ktk kudumisha viwango vya homoni. Maisha ya kukaa tu yanaweza kuchangia kutofautiana kwa homoni.

4•Kunywa pombe Kupita kiasi na uvutaji wa Sigara.

-Unywaji wa pombe kupita kiasi huweza kuvuruga uzalishaji wa homoni na kusababisha homoni kutowiana.

-Uvutaji sigara huvuruga usawa wa homoni za kiume kwa kuathiri homoni kadhaa, ikiwa ni pamoja na testosterone, homoni za tezi, na homoni za pituitary. Nikotini, sehemu kuu ya moshi wa sigara, yenye uwezo mkubwa katika kuharibu uwiano wa homini.

5•Unene/uzito kupitiliza.

Uzito/unene Kupita kiasi kunaweza kuathiri hormones ya testosterone na kuongeza hatari ya kutofautiana kwa hormone.

6•Kisukari.

7•Utumiaji wa Baadhi ya madawa ya hospitalini & kuzungukwa au kufanyia kazi kwenye mazingila ya chemical.

8•Matato au vimbe kwenye tezi.

9•Uzee na kutopata Usingizi wa kutosha.

Jifunze kuishi maisha ya balance upate kudumisha afya yako.

Iwapo una tatizo wewe ndugu jamaa au rafiki yako wasiliana nasi
Rich ☎️🥏 0718 750 220
Afya-Coffee.

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 21:00
Tuesday 09:00 - 21:00
Wednesday 09:00 - 21:00
Thursday 09:00 - 21:00
Friday 09:00 - 21:00
Saturday 09:00 - 21:00

Telephone

+255718750220

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Naimulika Afya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share