
28/09/2021
IJUE CHANGAMOTO YA SHAMBULIO LA KWENYE KIZAZI (P.I.D)
Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke (PID)
Tiba na ushauri
kwa mawasiliano zaidi;
Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana k**a cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu k**a salpingitis.
PID husababishwa na nini?
Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.
Je mwanamke huambukizwaje PID?
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na
Kufanya ngono isiyo salama Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period) Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage) Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
Dalili za PID ni zipi?
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni
- Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu - Kupata maumivu ya mgongo - Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya. - Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa - Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa - Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi - Kupata homa - Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na Pia kutapika
Vipimo vya PID
Ili kuweza kutambua k**a mwanamke ameambukizwa ugonjwa huu, tabibu anaweza kufanya vipimo kadhaa vikiwemo
Kuchunguza mkojo ili kufahamu k**a mgonjwa ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au mwenye uwezo wa kubeba mimba
Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza kuoteshwa katika maabara kwa