IJUE AFYA YAKO

IJUE AFYA YAKO Karibu ujipatie elimu ya afya na ushauri
Tunaruhusu maswali
Call 📞 +255622245928
wa.me/255622245928

I've just reached 300 followers! Thank you for continuing support. I could never have made it without each and every one...
08/03/2024

I've just reached 300 followers! Thank you for continuing support. I could never have made it without each and every one of you. 🙏🤗🎉

JE, UNAFAHAMU KUWA HAKUNA UGONJWA USIO KUA NA TIBA ISPOKUA KIFO NA UZEE? 🌹Kuna huu ugonjwa wa PID, ugonjwa huu huwasumbu...
29/11/2023

JE, UNAFAHAMU KUWA HAKUNA UGONJWA USIO KUA NA TIBA ISPOKUA KIFO NA UZEE?

🌹Kuna huu ugonjwa wa PID, ugonjwa huu huwasumbua sana wanawake wengi katika jamii.
🌹Wanawake wengi huangaika kutafuta tiba na kutumia gharama nyingi sana bila kupona.
🌹Wengi hutumia dawa za kumeza, za kupaka, sindano na dawa mbalimbali za Antibiotics bila mafanikio.
🌹Wengine hutumia dawa na kupata nafuu alafu ile hali inarudia tena.
🌹Wengine hufikia hatua ya kutumia tiba asili bila mafanikio.
🌹Wengine wanaenda mbali zaidi mpaka kwa waganga wa kienyeji wakidhani wamerogwa.
🌹Mbaya zaidi kuna wale ambao wameshakata tamaa na kusema PID haina tiba.

LEO naomba nikufahamishe kwamba hakuna ugonjwa usio kua na tiba.
1. Kila ugonjwa una tiba yake.
2. Kila tiba ina dawa zake.
3. Kila dawa zina utaratibu na matumizi yake.
4. Kila ugonjwa una dawa na tiba yake sahihi.

JIULIZE je ,ulipata tiba sahihi? Je ulipewa dawa sahihi?. Je ulipewa maelekezo sahihi? Je ulifata maelekezo sahihi?

Usihangaike na kuteseka na PID kiasi kukosa furaha ya tendo la ndoa.
Usipoteze ndoa yako sababu ya PID

Njoo tukuhudumie kwa uwaminifu tukupatie tiba sahihi ufurahie maisha ya ndoa

Follow
WhatsApp/call +255 622245928

JE UNAFAHAMU KUWA STROKE NI NINI??🧠 Stroke ni neno la kingereza kwa kiswahili tunaita kiharusi ama kupooza 🧠 Stroke ni u...
13/11/2023

JE UNAFAHAMU KUWA STROKE NI NINI??
🧠 Stroke ni neno la kingereza kwa kiswahili tunaita kiharusi ama kupooza
🧠 Stroke ni ugonjwa unaopelekea tatizo la kupooza kwa mwili
🧠 Kupooza kwa mwili kunaweza kutokea upande mmoja wa mwili ama baadhi ya viungo vya mwili wakati mwengine mwili mzima
🧠 Kuna aina kuu 3 za stroke 1. Ischemic stroke 2. Haemorrhagic stroke 3. Transient Ischemic Attack 《TIA》(Hizi tutakuja kuzichambua badae)
🧠 Stroke ni ugonjwa unaosababishwa na shida katika ubongo.
🧠 Shida katika ubongo inakuaje? Ubongo ndio kiungo mama katika mwili wa Binadamu.

🧠 Ubongo unapokosa damu safi huanza kusinyaa na kukauka nabadae ni Stroke aina hii tunaita Ischemic stroke.
🧠 Ubongo una mirija midogo inayosambaza damu pale ikitokea mirija hii kuziba ama kupasuka na damu kuvujia katika ubongo hupelekea Stroke.

🧠 Kwanini mirija ya damu izibe? Sababu ya mafuta mengi mwilini hujitengeneza na kuganda kisha huziba mirija hiyo pale damu inapotembea na kuzuia damu kufika baadhi ya sehemu za ubongo.
🧠 Kwanini mirija ya damu ipasuke? Sababu ya presha inapokua juu zaidi ya kiwango sahihi hupelekea mirija hii kupasuka na kumwagikia damu katikati ubongo matokeo yake ni Stroke.

🧠 STROKE sio ugonjwa wa KISHETANI bali ni ugonjwa wa mabadiliko ya kimwili hususan ndani ya ubongo.
🧠 STROKE ni ugonjwa unaozuilika kabla pia ni ugonjwa unaoweza kupona.

🧠 Tuondokane na fikra mbaya pamoja na imani potofu kuamini STROKE ni ugonjwa wa KISHETANI.
🧠 Tupeleke wagonjwa hospital mara baada ya kuonyesha dalili za kupooza tuache kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji ili tuokoe maisha yao.

🧠 Je, mpaka hapa kuna dalili yeyote ile ya Shetani?
🧠 Je, umemuona shetani akisababisha stroke?
🧠 Je, shetani amehusika na nini kupelekea Stroke?

✍️ Elimika na uwaelimishe wengine tuokoe jamii na tutokomeze Imani Potofu.

Follow
WhatsApp 0622245928

NDIO ANAWEZA KUPATA MIMBA 1. Kwa kawaida mwanamke anatakiwa kila mwezi apate hedhi. 2. Kuna tofauti ya mzunguko wa hedhi...
11/11/2023

NDIO ANAWEZA KUPATA MIMBA

1. Kwa kawaida mwanamke anatakiwa kila mwezi apate hedhi.

2. Kuna tofauti ya mzunguko wa hedhi kuna wa siku 28, 30, mpaka 37 wengine hufika.

3. Kwa kawaida kila mwezi yai huchavushwa na kuachiwa kutoka katika ovari kushuka chini kwaajili ya kurutubishwa na hudumu takribani masaa 12 hadi 24 kusubiria mbegu.

4. Pale yai linapochavushwa basi uwezekano wa kupata mimba unakua mkubwa sana.

5. Kwa wenye mzunguko wa siku 28 hadi 30 muda wa uchavushwaji unakua kati ya siku ya 11 hadi 14 na huwa siku za hatari zaidi kupata mimba.

6. Kwahiyo uwezekano wa kupata mimba kunategemea uchavushwaji wa yai na sio kupata ama kutopata hedhi.

Je, kuna ulichojifunza na kuelewa?

Follow
WhatsApp +255622245928

FAHAMU AINA 10 ZA VYAKULA VINAVYO CHOCHEA UZALISHAJI WA HOMONI YA KIUME IITWAYO TESTOSTERONE HORMONE 🧵TESTOSTERONE ni ho...
16/10/2023

FAHAMU AINA 10 ZA VYAKULA VINAVYO CHOCHEA UZALISHAJI WA HOMONI YA KIUME IITWAYO TESTOSTERONE HORMONE

🧵TESTOSTERONE ni homoni ya kiume ambayo yenyewe inapopungua husababisha upungufu wa nguvu za kiume na inapoongezeka huchochea ufanisi katika tendo la ndoa.

🧵Na hizi ndio aina 10 za vyakula vinavyo saidia kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
🧵Vipo vyakula vingi ila leo tuvijue vyakula 10.

1. Kitunguu swaumu
2. Kitunguu maji
3. Ndizi tamu za kuiva
4. Karoti
5. Limau/Ndimu
6. Tangawizi
7. Tikiti maji
8. Parachichi
9. Komemanga
10. Chungwa

🧵Darasa linalofata tutaenda kuangalia na kuchambua kila moja namna inavofanya kazi na faida zake kiujumla.

Karibu uulize na ujibiwe

The beauty of Mafia Island
07/10/2023

The beauty of Mafia Island

JE UNAJUA KUWA TATIZO LA KUTO LALA VIZURI HUSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME..!!?✍️ Unapokosa ama kushindwa kupata u...
03/10/2023

JE UNAJUA KUWA TATIZO LA KUTO LALA VIZURI HUSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME..!!?

✍️ Unapokosa ama kushindwa kupata usingizi na kulala vizuri tambua ndio chanzo cha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

✍️Kutopata usingizi wakati mwengine husababishwa na msongo wa mawazo , jitahidi kuondoa msongo wa mawazo.

✍️Unapokosa ama kushindwa kupata usingizi na kula vizuri hii hupelekea kupunguza kiwango cha homoni ya kiume.

✍️Homoni ya kiume (Testosterone) inapopungua huathiri ufanisi wa tendo la ndoa.

✍️Unapokua na tatizo hili pata ushauri kwa daktari.

Karibu tukupe elimu na ushauri wa afya

Follow

MSONGO WA MAWAZO VS UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1. Msongo wa mawazo huathiri namna ya ubongo unavotuma taarifa kwenda kwe...
01/10/2023

MSONGO WA MAWAZO VS UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

1. Msongo wa mawazo huathiri namna ya ubongo unavotuma taarifa kwenda kwenye uume ili kuruhusu kusambaa kwa damu.

2. Hii huathiri uwezekano katika ufanisi wa tendo ama kushindwa kabisa kufanya tendo la ndoa.

3. Msongo wa mawazo huchochea ongezeko la uzalishaji wa homoni inayoitwa Stress hormone.

4. Stress hormone inapunguza uzalishaji wa homoni ya kiume iitwayo Testosterone homoni ambayo inahusisha katika mfumo mzima wa tendo la ndoa.

5. Msongo wa mawazo huathiri katika kujiamini, kujithamini, huathiri hisia na hamu ya tendo la ndoa.

EPUKA MSONGO WA MAWAZO UFURAHIE TENDO LA NDOA

Kwa ushauri na tiba Call/WhatsApp +255622245928

JE UNAJUA KUWA KITAMBI NDIO SABABU YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.1. Kitambi huathiri mirija ya damu kwasababu Kitambi hu...
27/09/2023

JE UNAJUA KUWA KITAMBI NDIO SABABU YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

1. Kitambi huathiri mirija ya damu kwasababu Kitambi hupelekea hatari ya kupata magonjwa ya presha, kisukari na kadhalika.

2. Kitambi hupunguza Testosterone . Testosterone inafanya kazi katika ukuwaji wa tissue za mfumo wa uzazi na kuchochea ufanisi katika tendo la ndoa.

3. Testosterone ni homoni ya kiume inapopungua enzyme Oromatase huibadili Testosterone kwenda Estrogen ambayo ni homoni ya k**e.

4. Kitambi husababisha uvimbe mwilini ambao hupelekea tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Follow

JE, UNAFAHAMU KWANINI UZITO ULIOPITILIZA HULETA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1. Uzito uliopitiliza ndio chanzo cha shiniki...
25/09/2023

JE, UNAFAHAMU KWANINI UZITO ULIOPITILIZA HULETA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

1. Uzito uliopitiliza ndio chanzo cha shinikizo la damu
2. Uzito uliopitiliza hupelekea kitambi
3. Uzito uliopitiliza hupelekea ugonjwa wa kisukari
4. Uzito uliopitiliza hupelekea tatizo la neva
5. Uzito uliopitiliza hupelekea maumivu ya viungo vya mwili
6. Uzito uliopitiliza hupelekea tatizo la mfumo mbovu wa usafirishaji damu katika mwili
7. Uzito uliopitiliza hupunguza kasi na ufanisi katika kuliendea tendo la ndoa.

MAMBO HAYA 7 NDIO CHANZO CHA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

N.B
A. Kwanza uzito unatakiwa uendane na urefu pamoja na umri
B. Tunajuaje kwamba uzito tulionao ni sahihi. Tunapima kwa kutumia mfumo unaoitwa B.M.I index ( Tutakuja kutoa somo namna ya kutumia B.M.I index inavofanya kazi)

FAHAMU AINA 3 ZA MAZOEZI YANAYO TATUA CHANGAMOTO YA NGUVU ZA KIUME 1. MAZOEZI YA TUMBO           Haya ni mazoezi yanayoh...
24/09/2023

FAHAMU AINA 3 ZA MAZOEZI YANAYO TATUA CHANGAMOTO YA NGUVU ZA KIUME

1. MAZOEZI YA TUMBO
Haya ni mazoezi yanayohusisha sehemu za tumbo, hususan wenye vitambi hulazimika kufanya haya mazoezi.
Kwanini ufanye mazoezi ya tumbo. Kwasababu mazoezi ya tumbo huimarisha misuli ya tumbo na nyoga kwa pamoja (Abdominal pelvic ) na kupeleka kufunguka kwa mishipa ya damu ambayo huruhusu damu kufika sehemu za nyonga na uume kwa ufanisi na kuimarisha tendo la ndoa.

2. MAZOEZI YA NYONGA
Haya ni mazoezi yanayohusisha sehemu za nyonga (Pelvic flow) hufanya nyonga kutanuka na kufunguka pamoja na kuzibua mishipa ya damu na mirija ya uzazi ambayo husafirisha damu kwenda katika uume na kuimarisha ufanisi wa tendo la ndoa.

3. MAZOEZI YA KEGEL
Haya mazoezi yanajumuisha tumbo na nyonga kwa pamoja (Abdominal-pelvic) husaidia katika mfumo wa damu kuwa fanisi kwani damu inapofika katika kila kiungo cha mwili ndio ufanisi na utendaji kazi wa kiungo hiko. KEGEL huimarisha misuli na mishipa ya fahamu ya sehemu za siri ikiwemo tumbo, nyonga na uume na tendo la ndoa kua madhubuti

N.B Fanya mazoezi kuimarisha afya ya mwili na akili, mazoezi ni kinda na tiba ya maradhi mbalimbali ikiwemo Pressure, Sukari, msongo wa mawazo na tatizo la nguvu za kiume

Tunaposema kula kwa kuzingatia afya tunamaanisha nini?1. Kula chakula kilichoandaliwa vizuri kwa kuzingatia usafi 2. Saf...
23/09/2023

Tunaposema kula kwa kuzingatia afya tunamaanisha nini?

1. Kula chakula kilichoandaliwa vizuri kwa kuzingatia usafi
2. Safisha mikono kabla na baada ya kula.
3. Kula chakula unachokifahamu
4. Kula chakula halisi na sio vya viwandani
5. Kula vyakula mchemsho na sio vilivyo kaangwa
6. Kula matunda kila siku
7. Kula mboga za majani
8. Kula vyakula vya nyuzi nyuzi
9. Kunywa maji safi na salama
10. Kula usishibe

MAMBO 10 YA KUZINGATIA KUTATUA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME 1. Kula kuzingatia afya 2. Fanya mazoezi 3. Punguza uzito uliopi...
23/09/2023

MAMBO 10 YA KUZINGATIA KUTATUA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

1. Kula kuzingatia afya
2. Fanya mazoezi
3. Punguza uzito uliopitiliza
4. Ondoa kitambi
5. Punguza msongo wa mawazo
6. Lala vizuri
7. Punguza/acha matumizi ya vileo (Pombe na sigara)
8. Kula matunda na mbogamboga
9. Pata elimu ya mahusiano
10. Pata tiba ya saikolojia

KUNA SABABU KUU 8 ZINAZO PELEKEA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1. Matatizo ya neva (Neurological problems)2. Magonjwa ya mo...
18/09/2023

KUNA SABABU KUU 8 ZINAZO PELEKEA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

1. Matatizo ya neva (Neurological problems)
2. Magonjwa ya moyo (Cardiovascular Diseases)
3. Madawa (Medications)
4. Uzito uliopitiliza (Obesity)
5. Kiwango cha chini/kidogo cha testosterone (Low testosterone levels)
6. Wingi wa lehemu (High cholesterol)
7. Shinikizo la juu la damu (High blood pressure)
8. Ugonjwa wa kisukari (Diabetes)

Hizi ndio sababu kuu zinazopelekea changamoto hii na kila sababu ina namna yake inavosababisha tatizo la nguvu za kiume.

Ni vipi unaweza kutatua jibu lake ni kukabiliana na hizi Sababu 8.

Kufahamu zaidi kuhusu sababu hizi jinsi zinavopelekea upungufu wa nguvu za kiume uliza kwenye comment tupate kupeana elimu

ERECTILE DYSFUNCTION (ED) ni nini?   Ni upungufu wa nguvu za kiume ambalo hutokea kwa mwanaume kushindwa kuliendea tendo...
11/09/2023

ERECTILE DYSFUNCTION (ED) ni nini?

Ni upungufu wa nguvu za kiume ambalo hutokea kwa mwanaume kushindwa kuliendea tendo la ndoa kwa ufanisi na wakati mwengine uume kushindwa kusimama.

MAKUNDI 4 YA ED

1. DESIRE DISORDER: Ni hali ya ukosefu wa matamanio ama hamu ya tendo la ndoa.

2. AROUSAL DISORDER: Ni hali ya mwili kupoteza ama kutokua na uwezo wa kusisimka /ashki wakati wa tendo.

3. OR**SM DISORDER: Ni hali ya kutokuepo ama kushindwa kufika kileleni.

4. PSYCHOLOGY DISORDER: Ni hali ya kutokua timamu kiakili na kifikra.

SABABU ZINAZO PELEKEA ED

1. Ugonjwa wa kisukari
2. Msongo wa mawazo
3. Kuongezeka kwa hormone ya prolactin
4. Kuvimba kwa uume (Priapism)
5. Matumizi ya vilevi
6. Uvutaji wa sigara
7. Shida katika tezi dume (Prostate hormone)
8. Shinikizo la damu (Pressure)
9. Wingi wa lehemu katika damu (Blood cholesterol)
10. Tatizo la usingizi kuto lala vizuri
11. Kitambi/ uzito uliopitiliza
12. Matumizi ya baadhi ya dawa mfano: Dawa za Pressure na cancer
13. Kiwango kidogo cha High Density Lipoprotein
14. Kutofanya mazoezi
15. Punyeto/Puli

N.B Sababu nyengine ambayo ipo nje ya science ni Jini/Shetani mahaba hupelekea tatizo la nguvu za kiume

Je umepata kitu cha kujifunza na kuelimika ?
Je kuna sehemu ambayo hujaelewa? Uliza comment ntakujibu

PELVIC INFLAMMATORY DISEASE (P.I.D)?  Ni ugonjwa unaoshambulia mfumo wa uzazi wa mwanamke.   PID husababishwa na mchanga...
07/09/2023

PELVIC INFLAMMATORY DISEASE (P.I.D)?
Ni ugonjwa unaoshambulia mfumo wa uzazi wa mwanamke.
PID husababishwa na mchanganyiko wa bacteria.

SABABU ZINAZO PELEKEA PID

1. Kuwahi kubaleghe kwa mwanamke
2. Kuchelewa kubaleghe kwa mwanamke
3. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
4. Kua na mpenzi zaidi ya mmoja
5. Kutojitibia magonjwa yanayohusisha sehemu za siri. Mfano UTI, Kisonono, kaswende Fungus n.k

DALILI ZA PID

1. Uchafu ukeni
3. Harufu mbaya ukeni
4. Maumivu wakati wa haja ndogo
5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
6. Maumivu chini ya kitovu
7. Maumivu pembeni ya tumbo
8. Kutoka damu wakati wa tendo
9. Kutoka matone ya damu katikati ya mzunguko wa hedhi
10. Kuumwa mara kwa mara magonjwa ya mfumo wa mkojo.

N.B: Ukiwa na dalili kuanzia 3 na kuendelea jua una PID

MATIBABU YA PID

Matibabu ya PID hutegemea na hatua iliyofikia, kuna hatua ya awali, ya kati na ya mwisho kutokana na muda wa hilo tatizo na dalili zake

Unapotibia PID lazima wenza wote wawili wapate matibabu.

Tiba yake ni mchanganyiko wa dawa na sio dawa aina moja kwasababu husababishwa na mchanganyiko wa bacteria.

Hakuna ugonjwa usio kua na tiba


Follow
Mawasiliano angalia kwenye Bio

Tupo kwaajili yako....Afya yako ndio mtaji wako Ushauri bure wa.me/255622245928 WhatsApp
07/09/2023

Tupo kwaajili yako....Afya yako ndio mtaji wako
Ushauri bure wa.me/255622245928 WhatsApp

Karibu Mafia IslandKaribu nyumbani Karibu Mafia Festival
07/09/2023

Karibu Mafia Island
Karibu nyumbani
Karibu Mafia Festival


Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when IJUE AFYA YAKO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to IJUE AFYA YAKO:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram