01/01/2026
KWA NINI UNAKOSA HEDHI NA HUNA UJAUZITO
Unaweza kukosa hedhi bila kuwa mjamzito kutokana na sababu zifuatazo:
📌Msongo wa mawazo (stress)
📌Mabadiliko makubwa ya uzito wa mwili
📌Kufanya mazoezi kupita kiasi
📌Mabadiliko ya homoni (k**a PCOS au matatizo ya tezi/thyroid)
📌Kuanza au kuacha kutumia njia za uzazi wa mpango
📌Matumizi ya baadhi ya dawa
📌Maambukizi au magonjwa yaliyopo mwilini
Sababu hizi huathiri ishara kutoka kwenye ubongo au viwango vya homoni vinavyodhibiti mzunguko wa hedhi, hivyo kusababisha kuchelewa au kukosa hedhi kabisa. Hedhi zisizo na mpangilio ni jambo la kawaida, hasa kwa wasichana wenye umri wa miaka 13–19, lakini mabadiliko yanayoendelea kwa muda mrefu yanahitaji kumwona daktari.
Au piga simu 0742251310 kwa msaada