
05/05/2024
SEHEMU YA PILI ๐จ
Aina mojawapo ya endometriosis ni endometriosis inayopatikana ndani ya msuli wa mfuko wa uzazi. Aina hii ya endometriosis huitwa Adenomyosis. Mara chache hutokea endometriosis kuwa sehemu zilozo mbali na viungo vya uzazi k**a vile kwenye mapafu, jambo ambalo husababisha kukohoa damu wakati wa hedhi (catamenial hemoptysis).
๐ฅ Dalili za Endometriosis ni zipi?
Dalili za uwepo wa endometriosis ni pamoja na;
Maumivu wakati wa hedhi kwa kitaalam (dysmenorrhoea)
Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au siku za hedhi kuwa nyingi zaidi
Kushindwa kupata ujauzito (infertility),
Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa (dyspareunia)
Maumivu wakati wa haja kubwa au ndogo.
๐ฟUtambuzi wa Endometriosis
Mwanamke mwenye dalili za endometriosis anatakiwa kupimwa na daktari ili aweze kupewa ushauri wa matibabu.
Zipo njia kuu tatu:
Njia ya uchunguzi wa pelvis inayofanywa na daktari
Kwa njia ya ultrasound
Kupimwa kwa njia ya upasuaji wa matundu madogo (laparoscopy). Njia ya upasuaji wa matundu madogo ndio inayotumika zaidi kwenye kugundua uwepo wa endometrisis na hapohapo ugonjwa huweza kuondolewa.
Daktari hupeleka sehemu ya ugonjwa aliyoitoa kwenye vipimo vya maabara (pathology) ambayo huthibitisha uwepo wa tishu aina ya endometriosis.
Kutokana na kutokuwepo kwa njia hii katika vituo vingi vya huduma nchini Tanzania, ugonjwa wa endometriosis hausikiki sana nchini, lakini upo na wanawake wengi wenye maumivu yasiyotibika kwa dawa wakipimwa wanauwezekano mkubwa wa kukutwa na ugonjwa huu
TUENDELEE...??๐