15/08/2021
JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME (PART 1)
Kulingana na tamaduni zetu, wengi huwa tunamtanguliza Mungu una kumuomba atupatie mtoto tunayemtaka.
.
Mwanamke huzalisha mbegu aina moja ‘XX’ (X-Chromosomes) Mwaanaume anazalishwa mbegu za aina mbili ‘X’ (k**e) na ‘Y’ (kiume) (XY-Chromosomes).
Wakati wa uchavushaji;
Mama akitoa X na baba X = XX (mtoto wa k**e)
Mama akitoa X na baba Y = XY (mtoto wa kiume)
Mbegu ‘X’ ni imara ukilinganisha na ‘Y’, pia ‘X’ zinatembea polepole kulinganisha na mbegu ‘Y’ ambazo zenyewe ni dhaifu (sio imara na hufa mapema), lakini zina mwendokasi mkubwa.
Kalenda
Lazima ujue mzunguko wa mwanamke husika ni wa aina gani… kwa maana kuna mizunguko ya wastani wa siku 28 ambayo hii yai lake hutoka siku ya 14, kuna mzunguko mfupi wa siku 21 na yai hutoka siku ya 10 na pia wale wa mzunguko mrefu wa siku 36 ambao yai hutoka katika siku ya 18.
Mfano unaweza pata HEDHI kuanzia tarehe 1-5 na wengine huchukua siku 7. Hiki ni kipindi ambacho uterus hutoa damu baada ya yai la mwanamke kukosa kurutubishwa na mbegu za kiume.
SALAMA, SIKU YA 6-10.
Hiki ni kipindi ambacho mwanamke hawezi kupata mimba japo kinaelekea kipindi cha hatari
HATARI, SIKU YA 11-18.
Hiki ni kipindi ambacho mwanamke akijamiiana anapata mimba.
K**a mfumo wake wa uzazi upo sawa. Yaani hana uvimbe sehemu yoyote, homoni zimebalance vizuri, mirija haijaziba, hana infections zozote km vile PID, fangasi na UTI, kizazi hakina mikwaruzo. Hapa atapata mimba bila shida.
SALAMA SIKU YA 19-28.
Hiki ni kipindi kingine baada ya Ovulation ambapo mwanamke hawezi kushika mimba. Anajiandaa kupata hedhi nyingine kwakuwa yai halikurutubishwa siku za hatari. Endapo limerutubishwa hawezi ona hedhi nyingine.
Imeandaliwa na
……………….INAENDELEA…………