21/10/2022
*TATIZO LA BAWASIRI*
Ni ugonjwa unaotokana nna kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine kwenye njia ya haja kubwa na kusababisha kutoka kinyama au uvimbe.
Tatizo hili huathiri watu wote ila zaidi huathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30-40.
*AINA ZA BAWASIRI*
Kuna aina mbili za bawasiri
*I. BAWASIRI YA NDANI:* Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa, huwa haiambatani na maumivu bali muwasho mkali na wengi huwa hawajitambui kuwa wana tatizo hili.
*2. BAWASIRI YA NJE:*
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu hilo pia husababisha mishipa ya damu kupasuka na damu kuganda.
*CHANZO CHA TATIZO LA BAWASIRI*
Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha ugonjwa wa bawasiri ambavyo ni:-
I. Kupata choo kigumu
2. Kukaa kitako muda mrefu
3. Gesi kujaa tumboni
4. Magonjwa ya moyo na figo
5. Uzito kupita kiasi
6. Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
7. Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu
*DALILI ZA BAWASIRI*
I. Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa.
2. Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
3. Kutoka uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
4. Kujitokeza kinyama katika eneo la tundu la haja kubwa
5. Choo kigumu k**a cha mbuzi
6. Kutopata choo kwa muda mrefu
7. Kutoka damu wakati wa kupata haja kubwa
*MATATIZO YA BAWASIRI*
1. Kupata upungufu wa damu
2. Kupata tatizo la kutoweza kuhimili choo
3. Hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa
4. Kuathirika kisaikolojia
5. Kukosa morali ya kufanya kazi kutokana na maumivu makali
Kwa mawasiliano 0713934680