Huduma za kiroho na kimwili ktk Uislamu

Huduma za kiroho na kimwili ktk Uislamu Kutatua changamoto za kiroho ili kuondoa msongo wa mawazo, kwa kutoa elimu sahihi.

16/10/2023
Assalaamu alaykum warahmatullaahi wabarakaatuh.Karibuni ndugu zangu tuanzie hapa. NASAHA ZA NDOA     No_01 (1) KUTOSHEKA...
16/10/2023

Assalaamu alaykum warahmatullaahi wabarakaatuh.

Karibuni ndugu zangu tuanzie hapa.

NASAHA ZA NDOA
No_01

(1) KUTOSHEKA
Kutosheka kwa mume na mkewe ni miongoni mwa sababu za kuingia Peponi.
Mtume, swalallahu alayhi wa sallam, anasema.
(Haijuzu kwa mwanamke kufunga na hali mumewe yupo ila kwa idhini yake, na haruhusiwi katika nyumba yake bila idhini yake).

(2) UAMINIFU
Uaminifu katika kushughulika baina ya wanandoa ni miongoni mwa mambo yanayojenga mazingira ya ukarimu, maelewano na mapenzi baina ya wanandoa, halikadhalika maisha ya ndoa ambayo Msingi wake ni mahusiano mazuri, maelewano, urafiki na upendo Ndoa Hiyo ndio yenye mafanikio zaidi.

(3) KUSIKILIZANA
Mke kusikiliza mazungumzo ya mume ni moja ya mambo ambayo hujenga hali ya Ukarimu, maelewano na upendo baina yao, na Mke mwenye akili timamu anapaswa kujua kwamba mume siku zote Anapenda Kuongea kuliko kumsikiliza mke, kirafiki na kimapenzi.

MUME
Unaweza kutenga muda wa kutoka na kutembea naye Mke Wako,, na siku hii Unapotembea nje ya nyumba inaweza kuwa siku ya kujadili mambo yoyote ya maisha.

(4) BUSARA
Mke lazima awe na Busara na kuelewana na mume wake, na ikiwa Akimkuta Amemkasirikia, Awe Mpole Juu ya Kumtuliza na K**a Ndio Anazidisha Hasira Zake Basi Aachane na Mazungumzo na akae mbali naye wakati huu ili Asije Akamchokoza kabisa, na ajue kuwa muda wa mwanaume kurudi kutoka kazini sio wakati wa kulalamika na kununa Nuna.

Kukosolewa mara kwa mara ni mojawapo ya mambo ambayo mwanamke anapaswa kuepuka katika kushughulika na mumewe, na lazima aonyeshe Hali ya Kuomba Msamaha na sio kuzingatia hatia iliyotokea huko nyuma ili kutishia maisha yake na moto wa baadaye.

Unyoofu katika uhusiano wa ndoa, kutoa imani kwa mume, na kusema ukweli katika mazungumzo ni miongoni mwa mambo yanayofanya kazi katika maisha ya ndoa yenye afya isiyochafuliwa na aina yoyote ya shaka.

Kumtendea mke vizuri na familia ya mume ni moja ya mambo ambayo yanafanya kazi ya kujenga upendo kati yake na mumewe.

No_02 Ipo Njian......

05/09/2022

MWANAMKE IBEBE NDOA YAKO
1. Mwanamke ukiwa ndani ya ndoa, kwanza KUBALI KUWA WEWE NI MKE WA MTU. Hiyo ni hatua ya kwanza kabisa ya kudumu ndani ya ndoa yako.
*ISHI K**A MKE WA MTU NA USIISHI KWA KUSHINDANA NA WANAWAKE WASIO NA WAUME WALA KUSHINDANA NA MUMEO K**A NI MKE MWENZA WAKO.*

2. Hakuna Mwanamke ambaye ndoa yake imekufa *AKAFURAHI.* Yaani k**a wapo basi ni mmoja katika mia.
*ILA KIUJUMLA WENGI HUSONONEKA* .

3. Hivyo k**a unaweza kuishi ndani ya ndoa yako kwa AKILI na kuiepusha TALAKA usisubiri baadae, FANYA SASA HIVI AKILI HIYO. ANZA SASA, *USISUBIRI WAKATI WA MAGOMVI, WAKATI NI HUU WA MAPENZI NDIO WAKATI WA KUIFUKUZA TALAKA NDANI YA NDOA YAKO* .

4. Wale ambao ndoa zao ni changa, yaani zipo chini ya miaka mitano, *NAWAOMBA SANA TENA SANAAAA, ISHINI KATIKA NDOA ZENU KWA AKILI YA KUWA WEWE NI MKE WA MTU NA KUJITUMA* .

Kaweni mbali na walozivunja *NDOA ZAO, HAO NI HATARI SANAAAA KWA NDOA ZENU* .

5. Usiskilize mtu Asemae
"MWANAUME HATA UMFANYIE NINI HABADILIKI, HARIDHIKI WALA HAPENDEKI"

Na ninyi waambieni hivi
*"HUKO MNAPOKIMBILIA KUNA NINI? MNAFANYIWA NINI? AU MNAENDA KUKAA, KUISHI, KUOLEWA AU KUZINIWA ?"*

*CHUKUA HII MWANAMKE ULIYEMO NDOANI.*
"Mwanamke mwema hufanya sasa wakati wa amani nafuraha, hujitahidi kuzidisha manjonjo, mahaba, vikorombwezo, utundu, mbinu Mpya, urembo nk " *FANYA SASA USISUBIRI WAKATI UJAO* .

Mwanamke mjinga huiharibu ndoa yake kwa mikono yake na kauli zake yeye mwenyewe.

Ndugu yangu *DUMISHA NDOA YAKO*

13/11/2019

*MAMBO KUMI 10 UNAYOSTAHIKI KUYAPATA UKIWA KATIKA NDOA YAKO*

Kuna vitu kadhaa unastahiki kuwa navyo unapokuwa katika ndoa.

Ndoa yenye vitu hivi tunasema ni *NDOA YENYE FURAHA.*

Hapa chini ninakuletea mambo 10 ambayo unatakiwa kuwa nayo katika ndoa yako:

09/11/2019

Kuwa karibu mola wako kutakufanya upendeze mbele ya waja wake, nenda mbele yake uwapate waliompendeza

Mwanzo kuharibika kwa mtu ni kuweka mahisiano yake na mola wake hatarini, rejea hapa ili kujenga mwili na roho vyema 4:1...
09/11/2019

Mwanzo kuharibika kwa mtu ni kuweka mahisiano yake na mola wake hatarini, rejea hapa ili kujenga mwili na roho vyema 4:112 Qur an.

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255688263798

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Huduma za kiroho na kimwili ktk Uislamu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram