17/06/2022
AINA ZA FANGASI, SABABU NA DALILI ZAKE
Tatizo la fangasi ni moja ya magonjwa ya kawaida na yaliyozoeleka zaidi katika jamii zetu. Makala hii inaangazia aina za fangasi kwa kina ikichambua sababu na dalili za tatizo hili pamoja na tiba mbalimbali.
Ugonjwa huu katika hali ya kawaida si hatari sana na kinga pekee ya mwili huweza kukabiliana na vimelea hivi vya fangasi.
Lakini inapotokea mwili umeshindwa tatizo huweza kuwa kubwa zaidi kiasi cha kuhatarisha uhai hasa kukitokea uzembe katika kupambana na tatizo hili.
Fangasi husababiswa na nini?
Maradhi ya Fangasi husababishwa na kundi la vimelea vijulikanavyo k**a fangasi. Vimelea hivi hupatikana na kuishi katika maeneo mbalimbali k**a vile maeneo yenye uchafu, katika hewa, katika mwili wako hasa Ngozi, katika mimea na katika vyombo na vifaa mbalimbali.
Kuna mamilioni ya aina ya vimelea hivi lakini ni aina chache tu ambazo ni hatari na husababisha magonjwa katika mwili wa mwanadamu.
Sehemu kuu ambazo huathiriwa na magonjwa ya vimelea vya fangasi ni Ngozi, vilevile vimelea hivi huweza kuathiri hadi sehemu za ndani za mwili k**a vile mifupa.
Katika mwili wa binadamu zipo sehemu nyingi ambazo vimelea hawa wanaishi bila kuleta madhara ikiwa ni sehemu ya ushirika wa kawaida wa faida kati ya fangasi na mwili wa binadamu. Sehemu hizi ni k**a vile ukeni.
Aina za fangasi, sababu pamoja na dalili zake.
Uwezo wa fangasi katika kusababisha maradhi katika mwili hauna mipaka, vimelea hivi huweza kuathiri kuanzia seli, tishu, ogani, mfumo au mwili mzima wa binadamu. Sehemu yeyote ya mwili huweza kuathiriwa.
Aina za maradhi ya fangasi yamegawanywa zaidi kuzingatia ni maeneo yapi ya mwili yameathiriwa na si kwa kigezo cha aina ya fangasi. Hii inatokana na sababu kwamba aina zaidi ya moja ya fangasi inaweza athiri sehemu moja ya mwili.
Zifuatazo ni baadhi ya aina za Maradhi ya fangasi kuzingatia maeneo ambayo yameathiriwa na dalili zake.
Maradhi ya Fangasi za mdomoni na kooni.
Aina hii ya fangasi hushambulia maeneo mbalimbali ya mdomo(ulimi, kuta za mdomo na sehemu ya nje ya mdomo), na katika koo la chakula.
Candida ni aina ya fangasi ambao kwa sehemu kubwa husababisha aina hii ya fangasi na katika mwili wa binadamu hupatikana zaidi katika uke wa mwanmke.
Mchoro ukionyesha kinywa kilichathiriwa na tatizo la fangasi hapo juu 👆🏽
Aina hii ya fangasi huambatana na
Utando maeneo ya mdomoni,
Vidonda au michubuko.
maumivu makali ya kifua.
Maumivu mithili ya moto katika ulimi na,
Kupata shida wakati wa kutafuna au kumeza, wakati mwingine unashindwa hata kutema mate.
Aina hii ya fangasi huweza kumpata mtu yeyote lakini wagonjwa wa UKIMWI, kisukali na wagonjwa wa saratani ya damu (hasa ile inayoathiri seli nyeupe za damu).
Vilevile wagonjwa wanaopata tiba ya mionzi, matumizi makubwa ya dawa aina ya corticosteroid na matumizi sugu ya dawa za antibiotiki.
Maradhi ya fangasi za ukeni.
Maeneo mbalimbali ya uke huathiriwa kuanzia mashavu ya uke, mfereji wa uke na mlango wa kizazi vyote huweza kuathiriwa na fangasi. Fangasi wajulikanao k**a candida ndio hasa chanzo kikubwa cha fangasi za ukeni.
Mchoro ukionyesha uke ulioathiriwa na tatizo la fangasi hapo juu 👆🏽. Aina za fangasi za ukeni ni moja ya tatizo linalooathiri wanawake wengi.
Aina hii ya Fangasi za ukeni zimegawanyika kutokana na kiwango zilivyoathiri,
Fangasi za kawaida na
Fangasi sugu za ukeni.
Ili kuitwa fangasi sugu kigezo kikuu ni ikiwa fangasi zimetokea zaidi ya mara moja kwa vipindi tofauti na aina ya fangasi aliyesababisha. Kwa hivyo hata matibabu yake ni tofauti.
Baadhi ya dalili za aina hii ya fangasi ni;
Vidonda ukeni.
michubuko.
kuwashwa.
kuhisi maumivu ya moto au kuchoma.
maumivu wakati wa kukojoa na
kuvimba mashavu ya uke.
utando mweupe au mwekundu na uchafu mweupe wenye harufu
Kushuka kwa kinga za mwili, Matumizi ya dawa za kupanga uzazi hasa zenye kiwango kikubwa cha kichocheo cha Estrogen na kisukari .
Vilevile ujauzito na matumizi ya manukato, sabuni kali, viua shahawa ukeni. vyote hivi vinatajwa k**a vyanzo vikuu vya fangasi ukeni.
Maradhi ya fangasi sehemu za siri (sehemu zinazofichwa zaidi).
Maeneo k**a makwapani, mfereji wa matako, maeneo ya mapaja na maeneo ya korodani. Maeneo yote haya yapo katika hatari ya kushambuliwa na fangasi kwa sababu ya hali ya unyevu na joto katika maeneo haya.
Unyevu na joto ni mazingira Rafiki zaidi ya fangasi. baadhi ya dalili za aina hii ya fangasi nipamoja na;
Utando mithiri ya vibarango.
muwasho.
maumivu.
Ngozi kutoka au kumenyeka unapojikuna na
maeneo kuwa na mabaka mekundu.
Uchafu, kuvaa nguo za kubana, matumizi sugu ya antibiotiki, kushuka kwa kinga, kisukari, kutobadilisha nguo kwa wakati.
Vilevile kuvaa nguo wakati maeneo hayajakauka vizuri ni baadhi ya sababu zinazopelekea aina hii ya fangasi.
Maradhi ya fangasi za Ngozi na seli zilizokufa.
Aina hii inahusisha maeneo mbalimbali ya Ngozi ikiwemo miguuni na vidoleni, mgongo, vidole, kucha, Ngozi ya kichwani na nywele. Trichophyton rubrum ni fangasi ambaye anahusika zaidi na aina hii ya fangasi.
Mchoro ukionyesha vidole kilichathiriwa na tatizo la fangasi hapo juu👆🏽. Aina za fangasi za kucha ni moja ya matatizo yanayoharibu kucha za watu wengi.
Fangasi hawa huweza kuathiri vidoleni hasa uwazi uliopo kati ya vidole na unyayo wa mguu. Mara nyingi ngozi huwa ngumu na kusababisha miguu kupasuka (magaga).
Wakati mwingine uvimbe mfano wa vijipu vilivyoo jaa maji hutokea. Vilviile maeneo mengine ya ngozi hutengeza vibalango. Baadhi ya dalili za aina hii ya fangasi ni;
Kuwashwa maeneo ya kucha.
Ngozi kubanduka.
kusababisha vidonda.
kupata maumivu makali.
maumivu ya kuchoma k**a moto na
mabaka mekundu.
Uchafu, kuvaa viatu kwa muda mrefu, kutobadili soksi kwa muda mrefu, unyevunyevu maeneo ya vidole, kugusana na mtu au maeneo hatarishi hizi ni baadhi tu ya sababu.
Aina nyinginezo za fangasi ni Pamoja na fangasi za machoni, fangasi katika kuta za moyo, fangasi katika mfumo wa mkojo na fangasi katika mfumo wa fahamu.
Maradhi ya fangasi ya koo la hewa na milija ya hewa.
Maeneo ya koo la hewa, milija ya hewa na matundu ya pua ndio huathiriwa zaidi na aina hii ya fangasi. Candida na aina nyingine ya fangasi hutajwa k**a chanzo kikuu cha aina hii ya fangasi.
Watu wenye UKIMWI na virusi vya UKIMWI, na watu wenye saratani ya damu ndio kundi linaloathiriwa zaidi na aina hii ya fangasi.
Baadhi ya dalili za aina hii ya fangasi ni;
Homa kali.
kupumia kwa shida.
vidonda sehemu za koo la hewa.
maumivu wakati wa kuvuta hewa na
makohozi ya mara kwa mara.
Wasiliana na Dr. Jawadu kwa namba zifuatazo 0755411190📞