01/02/2022
FAHAMU DHANA YA UKATAJI KIMEO.
Habari tena.Jana niliishia kuelezea sababu ya kwanza kwa nini kimeo huvimba?...
sasa tuendelee ...
2.Allergies/mzio
Watoto wanapitia katika mazingira mengi ambayo hawajawahi kupitia,k**a vile baridi,joto,vyakula,mafuta,dawa,hewa n.k..kwa njia moja ama nyingine mazingira hayo yanawafanya wapate Allergy ambayo inapelekea kuvimba kwa kimeo.
3.Maambukizi.Hii inatokea pale mtoto anapopata maambukizi ya baktria/virus sehemu za karibu na kimeo k**a vile kooni,Masikio,tonsils,Adenoid ama mapafuni.
Mazingira ya ukataji Kimeo.
-Kazi hii hufanywa na waganga wa hadi wasio na utaalamu wowote wa maswala ya afya.
-Si Salama kiafya ,utakasaji wa vifaa vitumikavyo hauzingatii kanuni(IPC),udhibiti wa utokaji damu nyingi na maambukizi ya bakteria /virus hatari..
-Ni ujasiliamali hatari kwa jamii,wakataji wanajipatia fedha huku wakiwaacha watoto katika hatari kubwa ya kufa.
Nini madhara ya ukataji vimeo?
1.Kufubaza tatizo..haiondoi chanzo cha tatizo.
2.Upungufu wa Damu nyingi.
3.Maambukizi ya VVU,Homa ya ini na Tetanus.
4.Kushindwa kutamka baadhi ya maneno.
5.Kupata maambukizi ya koo Mara kwa Mara.
6.Ni ukatili wa kimwili(ukeketaji part 2).
7.Ongezeko gharama za matibabu..yani matokeo ya kukatwa hupelekea tatizo halisi kukomaa na kuhitaji matibabu zaidi.
8.Kifo..iwapo hayatatibiwa mapema.
Kwa nini wanaokatwa kuna wanaopona na wengine hawaponi???
Iko hivi..Mtoto a naweza pona baada ya kukatwa kwa sababu dalili alizonazo Mtoto kisababishi chake ni virus,allergy hivi vyote huwa havina dawa maalumu hivyo ni subira ya muda tu maana mwili mwenyewe hupambana hadi kujiponyesha ama wengine wanawakata kisha wanawambia wakaendelee kutumia dawa za Antibiotics ambazo zinasaidi baadhi ya visababishi vya tatizo...kwa upande mwingine Wengi wao hawawezi pona licha ya kukatwa kwa sababu bado chanzo cha tatizo kipo pale pale(kukatwa kwao ni sawa na kutaka kumuua nyoka kwa kumpiga mkiani).
Nini kifanyike??????
1.Elimu,Elimu..wataalamu tuzidi kutoa Elimu kwa njia zote ili jamii yetu iwe na afya tele.
2.Tuachane na mila potofu...wazazi vijana tunayoambiwa na wazee tuchuje ,ni Ujinga kufanya kila kitu unachoambiwa.
3.Wataalamu tuwachunguze kwa makini na kuwapima watoto vizuri ili kujua chanzo cha matatizo kwa watoto ili kuzuia wazazi kuwapeleka kwa sangoma.
4.Tupatapo mtoto aliyezidiwa tumtibu na tuombe walete PF3 kutoka polisi ili kuwabaini wanafanya kazi hiyo.
Endelea kufuatilia ukurasa wangu nitakuletea dhana ya kubemenda usiwe mbali.