
11/05/2022
Timu ya mradi mtambuka wa Saratani Tanzania(TCCP) inashiriki katika kutoa elimu na kuwapatia chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (Humanpapilomavirus vaccine) katika shule 30 za wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Zoezi hili lilianza tarehe 9/05/2022 na litadumu kwa siku Tano (hadi tarehe 13/05/2022) na tayari zaidi ya wanafunzi wakike 677 wameshapata elimu juu ya Saratani hii pamoja na chanjo. Tunategemea kuwafikia wanafunzi wakike 1500 na zaidi katika kipindi hiki na baada ya hapo timu ya mradi itahamia wilaya nyingine/mkoa mwingine.