05/06/2023
0783611438.
Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizo kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (va**na) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari.
Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote. Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno.
Dalili Za PID
PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa:
Maumivu – yanayoweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi Maumivu wakati wa kujamiiana Homa, wakati mwingine kusikia baridi Maumivu wakati wa haja ndogo, haja ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida.
Chanzo Cha PID
Kuna bakteria wa aina nyingi wanaoweza kusababisha PID, lakini maambukizo ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi. Bakteria hao huambukiza wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya kutumia kinga.
Aghalabu, bakteria hawa huingia kwenye viungo ya uzazi vya mwanamke pale ulinzi wa kwenye shingo ya kizazi (cervix) unapovurugwa. Hii inaweza kutokea mathalani, wakati wa hedhi na baada ya kuzaa, mimba kuharibika au kutoa mimba. Mara chache bakteria huweza kujipenyeza wakati kifaa cho chote cha tiba kinapoingizwa kwenye nyumba ya uzazi.
Mazingira Hatarishi
Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID, navyo ni:
Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja Kufanya mapenzi bila kinga Kujisafisha na maji mara kwa mara Kuwa uliwahi kupata