14/03/2022
DALILI ZA UGONJWA WA FIGO.
KUVIMBA USO:
1)Kuvimba uso, miguu na tumbo, ni ishara za ugonjwa wa figo. Dalili za kuvimba kutokana na ugonjwa wa figo huwa inaanzia chini ya kibukio cha jicho (eye lids) na hutambulika sana asubuhi. Kushindwa kwa figo ni sababu ya kawaida na muhimu ya kuvimba. Lakini tunahitaji kuelewa kuwa kuvimba si lazima iwe ni figo kushindwa. Kuna ugonjwa mwingine wa figo licha ya figo hufanya kuvimba kutokea (mfano nephritic syndrome). Hoja nyingine ni vema kuwekwa akilini ni kuwa kuvimba huenda kusionekane kabisa kwa wagonjwa wachache wa ugonjwa dhahiri wa figo kushindwa kazi.
2)Kukosa hamu ya chakula, kusikia ladha isiyo ya kawaida mdomoni na kushindwa kula chakula vyema ni shida za kawaida zinazopatikana kwa watu wenye hitilafu ya figo. kushindwa kwa figo zaidi kwa sababu ya sumu nyingi mtu huwa na kichefuchefu, kutapika na kwikwi.
3)Kupanda kwa damu/ Shinikizzo la damu – hypertension
Kwa wagonjwa wa kushidwa kwa figo kufanya kazi, shinikizo la damu ni kawaida. Iwapo shinikizo la damu kunatokea katika umri mdogo (chini ya miaka 30) au shinikizo la damu liko juu wakati wa uchunguzi, sababu yaweza kuwa shida ya figo.
4)Kuvimba kwa uso chini ya macho mara kwa mara inaonyesha dalili ya ugonjwa wa figo.
5(Anemia (ukosefu wa damu) na kuwa dhaifu
Kuwa dhaifu, kuchoka mapema, kukosa kutulia sehemu ya kazi ni malalamishi ya mara kwa mara ya mtu mwenye anemia (low hemoglobin level). Wakati mwingine hizi ni dalili pekee za mtu mwenye hali za mwanzo za ugonjwa sugu wa figo kutofanya kazi. Iwapo anaemia haiponi baada ya matibabu kamili, ni vyema kufikiria kushindwa kwa figo k**a moja ya sababu ya anemia hiyo.
6)Malalamishi yasiyo kawaida
Kuumwa chini ya mgongo, kuumwa mwili, kujikuna na maumivu ya miguu (cramps) huwa ni malalamishi ya mara kwa mara ya ugonjwa wa figo. Kutoendelea kukuwa, mtu kuwa mfupi na kujikunja (bending) kwa mifupa ya miguu ni dalili nyingine kwa watoto wenye ugonjwa wa figo.
7)Kupata shida ya mkojo
Dalili za kawaida za kulalamikia mkojo :
1. Kiwango cha mkojo kilichopungua, ambacho husababisha kuvimba ni wazi kwa magonjwa mbalimbali ya figo.
2. Muwasho wa mkojo, kukojoa mara kwa mara na kukojoa damu au usaha ni dalili za maambukizo ya njia ya mkojo.
3. Ugumu wa kukojoa kunaweza kusababisha ugumu wa kusukumwa na kupitisha mkojo, mkojo hafifu au kudondokwa kwa mkojo. Katika hali mbaya kabisa kutopitisha/ kuziba kabisa mkojo ni hali ya kawaida kwa mgonjwa huyu,
Zingatia:
Ingawa mtu anaweza kuwa na dalili zilizotajwa hapo juu, hii haidhihirishi kuwa mtu huyu anaugua ugonjwa wa figo. Hata hivyo, kukiwa na dalili hizi, inahimizwa kumwona daktari na kuthibitisha k**a kuna dalili yoyote ya ugonjwa wa figo kwa kupima na kufanya uchunguzi.
Ni vyema kukumbuka kuwa, shida kubwa za ugonjwa wa figo zinaweza kuwepo chini chini kwa muda mrefu bila dalili au ishara zozote muhimu.
Nb:
Kwa shida ya FIGO na shida nyingine nyingi
K**a , TEZI DUME bila Upasuwaji, kuziba MKOJO, VIDONDA vya tumbo SUGU, bawasili KUTOKA kinyama njia ya haja kubwa, change limalozuia uzazi/ kutokunasa ujauzito, KUTOKWA UCHAFU MWEUPE UKENI, moyo, shida ya mapafu, SARATANI nk contact 0672789066