
09/01/2023
Kunyonyesha ni njia Nzuri sana sanaaaaaaa ya KUPUNGUZA UZITO
Ila UNYONYESHE MIEZI SITA bila Kumpa mtu kitu kingine(EXCLUSIVE BREASTFEEDING FOR 6MONTHS), Au mbadala wowote(na kunyonyesha hapa ni pamoja na KUKAMUA), muhimu mwanao atumie MAZIWA YAKO TU, lakin baada ya miezi sita kupita,Endelea kunyonyesha mpaka mwanao AFIKE MIAKA MIWILI AU ZAIDI...unapopata muda nyonyesha sana,inasaidia ku burn calories sana na wanawake wengi hii ni njia inawafanya Warudie miili yao ya kabla ya uzazi(ila LAZMA PIA ULE HEALTHY FOODS, usile sile Ovyo ovyo vyakula vya kunenepesha).
Wamama wengine kipindi cha kunyonyesha ndo wanafumuka sanaaa miili Yao kuliko hata kipindi cha ujauzito😃😃👐, nadhan chanzo kikubwa ni ULAJI, hata k**a unanyonyesha, Be selective vitu vya kula na kuzalisha MAZIWA ya kutosha bila kukufanya Unenepeane Kupita kawaida
Trust me, UKIZINGATIA UNYONYESHAJI HUO, Ukapata balanced diet yako, maji ya kutosha, na ukajiboost na vitu vya kuongeza uzalishaji wa maziwa(Virutubisho lishe), UTAPUNGUA na MWANAO ATAPATA AFYA na KINGA kutoka kwa Maziwa ya mama ake.
-
Wewe ulipojifungua mwanao na kuzingatia unyonyeshaji sahihi mwili wako ulikuaje..!? Tushare experience kwa pamoja kwa Mama wanaokuja 🤰🏽🤱