26/11/2020
Tatizo la tezi dume na kupanuka kwa tezi
0688896151
Tezi dume hupatikana kwa wanaume tu.Tezi hili likiongezeka kwa ukubwa yaani inapopanuka,hasa kwa wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka sitini, hutatiza kukojoa.Ugonjwa huu unazidi kuongezeka duniani kwani watu wanaishi maisha marefu zaidi siku hizi.
Tezi dume ni nini na kazi yake ni nini?
Tezi dumeni kiungo kidogo na ni sehemu moja ya uzazi wa wanaume.Hupatikana chini ya kibofu na mbele ya mwanzo cha njia itoayo mkojo hupitia ndani ya tezi dume.Tezi dume ndiyo hutoa maji yabebayo mbegu (manii)ya mwanaume.
Tezi dume kupanuka
Kupanuka kwa tezi dume ni tatizo la kawaida ambalo halisababishwi na ugonjwa wa saratani(kansa).Huwa ni jambo la kawaida kwa karibu kila mwanaume mzee.Miaka inavyoenda,ndivyo tezi dume huzidi kuwa kubwa; na hufinya njia ya mkojo na kuziba mkojo.Hivyo mkojo hutoka polepole .
Ugonjwa wa kutanuka kwa tezi dume ni ugonjwa wa wanaume wazee.
Dalili za kupanuka kwa tezi dume
Dalili huonekana baada ya umri wa miaka ya arobaini na kuendelea. Karibu wanaume wote wenye umri wa sabini na themanini huwa na tatizo hili.Dalili huanza polepole na kuzidi jinsi miaka inavyoongezeka.Dalili hizi ni k**a zifuatazo:
Kukojoa mara nyingi hasa nyakati za usiku.Hii ni dalili ya mapema sana.
Kulazimika, mara nyingi hasa nyakati za usiku, kutumia nguvu kuanzisha mkojo kutoka. Hata pale mgonjwa anahisi kibofu kimejaa. Hii ni dalili ya mapema sana.
Mkojo kutiririka polepole, hukatikakatika na hutumia nguvu kutoka.
Mkojo kushidwa kutoka hata wakati mtu anapohisi kukojoa.
Mkojo kuendelea kutoka kidogokidogo baada ya kukojoa, matone ya mkojo huendelea kutoka hata baada ya kukojoa hivyo nguo za ndani hulowa.
Kibofu hakiishi mkojo.0688896151