Dr_Kassimu Na Afya.

Dr_Kassimu Na Afya. Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Dr_Kassimu Na Afya., Medical and health, Dar es Salaam.

MATIBABU YA MIFUPA BILA UPASUAJIMifupa ndio inayokupa muonekano na kukusaidia kufanya shughuli zote za nguvu ikiwa inasa...
18/10/2022

MATIBABU YA MIFUPA BILA UPASUAJI
Mifupa ndio inayokupa muonekano na kukusaidia kufanya shughuli zote za nguvu ikiwa inasaidiana na misuli ya nyama. Mifupa hufanya kazi kubwa wakati wa kutembea, kukaa , kusimama, kulima, na kazi mbalimbali, nk.
Kutokana na shughuli mbali mbali tunazofanya misuli hukak**aa na kusababisha kubadilisha mpangilio na muonekano halisia wa mifupa. Hii husababisha mifupa kuinda, kupishana, kusagana, kuvunjika n.k.

MAGONJWA YA MIFUPA
watu wengi nilio wahudumia huwa na matatizo yafuatayo ya viungo:-
1: Maumivu ya kichwa na shingo
2:Maumivu ya kiuno na nyonga
3: Maumivu ya magoti na miguu
4: Maumivu ya mabega, mbavu na mikono
5: Miguu kuwaka moto
6: Miguu kufa ganzi
7: Gauti
8: Arthritis

Wagonjwa baada ya vipimo vya xray, CTScan au MRI huweza kutambulika magonjwa yao na kuishiwa kupatiwa dawa za maumivu ambazo hutuliza tu maumivu bila kumaliza chanzo cha tatizo. Hii husababisha tatizo kuendelea kwa muda mrefu na baadae hulazimika kufanya upasuaji. Hata baada ya upasuaji huwa hakuna matumaini makubwa kwani madhara huwa yamefanyika kwa muda mrefu.
Tunatoa matibabu ya magonjwa ya mifupa kwa dawa nzuri zilizothibitishwa na mamlaka ya dawa na chakula Tanzania na Marekani. Dawa hizi hurekebisha tatizo na kutengeneza kinga ya kuzuia mifupa kusagana na kutengeneza gegedu, ute ute na mifupa kuwa imara. Tunaweza kukusaidia ukarudisha furaha katika maisha yako au ndugu yako unayemuhudumia.
Kwa matibabu, ushauri, maswali na maoni unaweza kuwasiliana nami.
0759490202
Dr Kassim

MAUMIVU YA NYONGA YANATIBIKAMaumivu ya nyonga yanawasumbua sana na yanaathiri ubora wa maisha. Mgonjwa hushindwa kufanya...
18/10/2022

MAUMIVU YA NYONGA YANATIBIKA

Maumivu ya nyonga yanawasumbua sana na yanaathiri ubora wa maisha. Mgonjwa hushindwa kufanya majukumu yake ya kila siku ya kujikimu k**a kuoga, kuvaa nguo, kutembea, kukaa, kusimama.nk. hii husababishwa na kuisha na kusagika kwa mifupa na ligament za maungio ya mifupa. Hii huchangiwa na kushindwa kutengenezwa kwa gegedu na mifupa hii baada ya kuumia. Mifupa pia huanza kuyeyuka kwa umri unapoanza kua mkubwa. Hii husababishwa na mwili kuacha kujijenga na kuanza kuyayusha mifupa kupata madini ya kalshiamu na kutumia sehemu nyingine ya mwili. Hivyo watu umri mkubwa wanashauriwa kupata virutubisho sahihi ili kuwezeshwa kutengeneza na kuzuia kuyeyuka kwa mifupa.

Kwa ushauri, maswali na maoni unaweza kuwasiliana nami.
0759490202
Dr Kassim.......!

10/10/2022

IJUE TOFAUTI YA KUTEGUKA NA KUVUNJIKA MGU
(JOINT DISLOCATION AND BONE FRACTURE)
Kuna tofauti kubwa kati ya kuteguka mguu na kuvunjika mguu. Kwa kifupi kuteguka na kupisha a kwa mifupa miwili ya karibu katika maungano na kuvunjika ni kukatika kwa mfupa mmoja na kutoa miwili au zaidi. unaweza kufikiri ipi ni hatari sana ukipata kuliko nyingine....! Kuteguka ni joint ni hatari zaidi kwani hupelekea watu wengi kukatwa viungo. Hii husababishwa na kuteguka maungio hupelekea mishipa ya damu kuziba na mishipa ya fahamu kutakika. Kuvunjika huwa hatari k**a mfupa uliovunjika utaenda kukata mshipa wa damu au fahamu uliokaribu. Na hii hutokea iwapo baada ya ajali majeruhi ataitumia mifupa iliyovunjika. Katika zote mbili inapotokea kwa huduma ya kwanza fanya yafuatayo.

HUDUMA YA KWANZA KWA MJERUHIWA
1: mlaze mgonjwa mahali salama
2: omba ruhusa ya kumhudumia mgonjwa
3: muulize sehemu alikoumia
4: baini jeraha na aina ya mvunjiko au kuteguka alikoumia mgonjwa
5: zuia damu k**a inatoka
6: funga eneo lililo vunjika au teguka kusiwe na kucheza cheza kabisa.
7: mpeleke mgonjwa hospitali kwa matibabu

Kwa maswali, maoni au ushauri unaweza kuwasiliana nami.
Dr Kassim
0759490202

09/10/2022

PRESHA, KISUKARI NA NGUVU ZA KIUME IJUE KINGA NA TIBA
Unaweza kutengeneza kitunguu swaumu kwa kuandaa juisi yake halisi, kuchanganya katika chakula au kutengeneza chai kwa kuchanganya na tangawizi. Kitunguu swaumu huondoa rehemu mbaya katika mishipa ya damu na kuzibua misuli hiyo na damu kusambaa vizuri.
Kwa maswali, maoni au ushauri tunaweza kuwasiliana.
Dr Kassim
0759490202

07/10/2022

MAGONJWA YA LIGAMENTS (KANO)
0759490202

matatizo mengi ya mifupa na viungo huweza kusababishwa na kuumia kwa kano au ligaments. Hizi ni ni nyama ngumu (fibrous tissue) zinazounganisha mfupa mmoja na mwingine. Huwezesha mtu kutembea, kuinama na kufanya kazi za kila siku. Watu wa mazoezi huumiza nyama hizi na hushindwa kushiriki mazoezi tena.

MAGONJWA YA LIGAMENTS
1: Ligaments kupasuka
2:Ligament kukatika
3: Ligament kuvutika
4:Ligament kuoza

DALILI ZA MAGONJWA YA LIGAMENT
1: Maumivu makali ya maungio (joint)
2: maungio (joint) kuvimba
3: kushindwa kukunja au kunyoosha joint
4: maungio kujaa maji

Uponyaji wa ligament huchukua muda mrefu sana kuyokana na kuwa na mishipa ya damu michache. Huweza kuchukua muda wa wiki tatu mpaka wiki sita na mara nyingine huenda mpaka miezi sita.

MATIBABU YA JERAHA KATIKA LIGAMENT
1: Weka kipande cha barafu
2: chua eneo lililo athiriwa
3: funga na bandage
4: Tumia dawa za kuponesha na kutengeneza ligament imara
5: unaweza kutumia dawa za maumivu

Kwa maswali, maoni na ushauri tunaweza kuwasiliana ili kuweza kusaidia juu ya matatizo ya kiafya.
Dr Kassim
0759490202

07/10/2022

UNAFAHAMU KUHUSU KICHOMI
kichomi ni tatizo la muda ambalo hutokea mara nyingi kwa wanamichezo au kwa mtu anayefanya kazi fulani. Kichomi ni maumivu makali ya ghafla katika nyama za eneo fulani ambayo mhanga hushindwa kukunja au kunyoosha au kutumia eneo lililo athiriwa.

SABABU ZINAZOSABABISHA KICHOMI
1: mazoezi makali
2: kutotumia kiungo fulani kwa muda mrefu
3: kukandamiza kiungo na kuzuia mawasiliano ya damu na fahamu


Kinachotokea ni hiki, mwili unategema kutengeneza nguvu (energy) kutoka katika glucose na kuichoma katika oxijeni. Endapo oxijeni itakosekana mwili huunguza glucose bila oksijeni na kutengeneza sumu inayojulikana k**a lactic acid. Kemikali hii ndio inayosababisha maumivu makali ya misuli. Kemikali hii inapoisha ndio mgonjwa nae hupata nafuu na kupona kabisa.

JINSI YA KUMSAIDIA MGONJWA
1: mlaze chini
2: piga piga eneo lililo athirika
3: maseji/chua taratibu eneo hilo
4: kunja na kunyoosha eneo hilo iwezekanapo
5: pata matibabu k**a hali si shwari

Kuna baadhi ya watu huwatokea hali hii bila kufanya shughuli yeyote ile wanakua wamekaa au wamelala. Maumivu huwa yanajirudia sana zaidi ya mara moja kwa siku. Kwa hali hii onana na daktari wako kwa uchunguzi zaidi.

Kwa ushauri, maswali na maoni unaweza wasiliana nami.
0759490202
Dr Kassim..........!

06/10/2022

GAUTI ( GOUT ) HUSABABISHA ULEMAVU
#0759490202
Magonjwa yasiyoambukiza yanaongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea. Gauti ni moja ya magonjwa yanayosumbua watu wengi kwa Tanzania. Gauti husababishwa na mwili kushindwa kutoa kiwango cha Urea katika damu ambacho hutengeneza chumvi chumvi inayo kwenda kuhifadhiwa katika maungio ya mifupa na misuli. Chumvi hii huleta madhara ya kuumiza eneo husika na kuharibu kabisa muonekano wa eneo husika.

DALILI ZA GAUTI
1: Maumivu ya eneo lililoathiriwa
2: kutoka nundu moja au nyingi ndogondogo katika eneo husika
3: eneo husika kuwa jekundu sana na baadae kubadilika kuweka vialama vyeupe
4: Nundu kupasuka na kutengeneza vidonda ambavyo kupona ni kazi sana.
5: kushindwa kutumia sehemu iliyo athirika

NINI CHAKUFANYA
1: kupata ushauri wa daktari unapopata matatizo haya
2: kula lishe bora inayowezesha kupunguza utengenezaji wa uric acid na kuongeza utoaji wa sumu hio mwilini
3: kunywa maji mengi na mazoezi

Unaweza kuwasiliana nami kwa ushuri, elimu na maswali
#0759490202
Ahsante

06/10/2022

AFYA YA NGOZI
1: kula vyakula vyenye ant-oxidant
2: mazoezi na kupumzika
3: kunywa maji mengi

YOUR HEALTH AND AGE ARE REFLECTED ON YOUR SKIN.
06/10/2022

YOUR HEALTH AND AGE ARE REFLECTED
ON YOUR SKIN.

04/10/2022

MADHARA YA SICKE CELL KWENYE MIFUPA
Sickle cell ni ugonjwa unaosababishwa na chembe hai nyekundu za damu badala kua na umbo la donati nzuri huharibika na kujikunja na kutemgeneza k**a ndizi mbinuko hivi. Hii husababisha chembe hai hizi kushindwa kupita katika mishipa ya damu midogo na kuziba kusiba. Hii husababisha maeneo yanayopata damu kutoka kwenye mishipa hii kuanza kufa kutokana na kukosa hewa na chakula. Dalili nyingi huonekana katika mfumo wa mifupa na hewa. Mifupa inayo athirika zaidi ni ile ya miguu, kiuno, na kifua ila huweza kuathiri mifupa yote ya mwili. Maumivu ya mifupa huwaathiri watu wenye matatizo ya sikle cell mara kwa mara. Na iwapo isipopata matibabu haraka mifupa inayokosa damu huanza kufa na kuoza taratibu taratibu.
Unaweza kumsaidia mgonjwa kwa kufanya yafuatayo.
1: Kuhudhuria kiliniki ya matatizo hayo bila kukosa
2: kupata lishe bora ili kutemgeneza kiwango cha damu kufidia kile kilichoharibika.
3: kuepuka vyanzo vinavyohatarisha afya ya mgonjwa
4: kufanya kazi za kawaida, kupumzika na kunywa maji mengi na matunda mara kwa mara
5: kupata matibabu sahihi iwapo hali hio itajitokeza

Kwa maswali, ushauri na maoni wasiliana nami
0759490202
Dr Kassim.

03/10/2022

DAWA ZA PRESHA HUPUNGUZA UWEZO WA KUFANYA TENDO LA NDOA.
Moja ya madhara yatokanayo kutokana na matumizi ya dawa za presha ni kupungua kwa nguvu au uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Kwa muda dawa zinapokua kwenye mzunguko wa damu huingiliana na fiziolojia ya uume kusimama na matokea unashindwa kusimama kabisa hali yakua unatamani kufanya tendo hilo.
Unaweza kubadili dawa zinazoleta madhara hayo na kutumia dawa rafiki na afya yako ya uzazi.
Kwa maswali, ushauri na elimu unaweza kuwasiliana nami.
#0759490202

19/09/2022

UPOFU KUTOKANA NA KISUKARI
0759490202

Kiwango kikubwa cha sukari husababisha mishipa ya damu kuziba na kupasuka na kumwaga damu kwenye majimaji ya jicho. Pia husababisha kuota kwa mishipa mingi katika retina nyuma ya jicho ambako hua ni sehemu mwanga unapokusanyika kwa ajili ya kupeleka taarifa kwenye ubongo. Uotaji wa mishipa ya damu huziba sehemu hii na miale ya mwanga kushindwa kutengeneza umbo la kitu hivyo kushindwa kupeleka taarifa katika ubongo.

DALILI ZA KUANZA UPOFU
1: kuona giza giza
2: kushindwa kuona rangi za kitu
3: kushindwa kuona usiku
4: jicho kubadili rangi
5: kushindwa kuona vitu vya pembeni na kuona katikati tu

Unaweza kuepuka matatizo haya kwa kufanya yafuatayo
1: kutumia dawa sahihi za kisukari
2: kupima macho mara kwa mara
3: kutumia mboga mboga zenye vitamin A

Dr Kassim
0759490202

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr_Kassimu Na Afya. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share