15/03/2026
πΈ WIKI YA 37+ YA UJAUZITO β NITAJUAJE UCHUNGU UMEANZA? π€°π½β³
Mfuatiliaji wetu mmoja ameuliza:
π¬ βDaktari, huu ni ujauzito wangu wa kwanza. Niko wiki ya 37 lakini sijui dalili za uchungu. Sijisikii kitu tofauti. Nitajuaje uchungu umeanza, na nifanye nini?β
Kwanza kabisa mama hii ni hali ya kawaida sana, hasa kwa ujauzito wa kwanza. Wajawazito wengi hawajui uchungu unaanza vipi hadi pale unapoanza kweli.
π DALILI ZA KWELI ZA UCHUNGU WA KUJIFUNGUA
βοΈ Maumivu ya tumbo au kiuno yanayokuja na kupotea kwa mpangilio
Maumivu huanza taratibu lakini yanaanza kuja mara kwa mara na kuongezeka nguvu.
βοΈ Maumivu kuongezeka kadri muda unavyopita
Tofauti na maumivu ya kawaida, uchungu wa kujifungua haupungui unapopumzika.
βοΈ Kutoka ute mzito wenye damu kidogo (bloody show)
Hii ni dalili kwamba mlango wa uzazi umeanza kufunguka.
βοΈ Maji kutoka ukeni (kupasuka kwa chupa ya uzazi)
Unaweza kuhisi maji mengi ghafla au yanayotoka kidogo kidogo.
π₯ UFANYE NINI UKIPATA DALILI HIZI?
ππ½ K**a maumivu yanarudi kila dakika 10β15 au chini, anza kujiandaa kwenda hospitali.
ππ½ K**a maji yametoka, wahi hospitali hata k**a uchungu haujaanza.
ππ½ Ukiwa na damu nyingi au kupungua kwa mateke ya mtoto, nenda hospitali haraka.
π‘ KUMBUKA
Wajawazito wengi hupata uchungu kati ya wiki ya 38 hadi 41.
Hivyo k**a bado hujapata uchungu wiki ya 37, si jambo la ajabu.
π€ Mwili wako unaandaa kila kitu polepole.
π¬ Swali kwa akina mama:
Ulipojifungua mara ya kwanza, dalili ya kwanza ya uchungu ilikuwa ipi?
Shiriki uzoefu wako ili kumsaidia mama mwingine anayesubiri siku yake ππ½