
23/11/2024
VYAKULA VYENYE KUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA.
Ikiwa tatizo hili la kukutoa maziwa ya kutosha wakati wa kunyonyesha halitokani na tatizo la ugonjwa k**a vile mama kuwa na uvimbe au jipu katika t**i
Mama tunamshauri kutumia mojawapo ya vyakula vifuatavyo:
1.TENDE
Kwa kula tende pekee au tende na maziwa au Juisi ya tende yenye maziwa .
Kwa wastani robo kilo ya tende kwa siku
2.PILIPILI MANGA
Kutumia pilipili manga kwa kuiweka kwenye uji au juisi au kuichemsha yenyewe na kuinywa k**a chai
3.MBEGU ZA MABOGA
Kula mbegu za maboga na boga lake au tafuna mbegu za maboga zilizokaangwa Mara kwa Mara kunasaidia uzalishaji wa maziwa kwa wingi
4.SUPU YA TAA/PWEZA
Kunywa supu ya samaki aina ya taa/pweza nako kunasaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha
SUPU YA NG'OMBE,MBUZI NA KONDOO
Mwanamama anapotoka kujifungua ni vizuri apate supu kila asubuhi na ni vizuri zaidi akapata supu ya
kongoro,nyama ya ngombe au supu ya kondoo kwani
supu za namna hii ni tiba nzuri kwa mama mwenye
matatizo ya kutopata maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto wake na pia hurejesha nguvu zilizopotea wakati wa kujifungua.
NDIZI ZA KUCHEMSHA
Pia ndizi za kuchemsha ni nzuri sana kwa kuondoa hili tatizo la kukosa maziwa kwamama mjamzito,zichemshwe vya kutosha mpaka ziwe laini na hata mtori pia unafaa katika kutibu hali hiyo.
MAJI
Mzazi anapaswa awe ni mwenye kujitahidi kunywa maji ya kutosha kila siku kwani nayo humsaidia kuongeza maziwa kwa ajili ya mwanae mpya.
UJI WA PILIPILI MTAMA/MANGA
Aidha mzazi anashauriuwa anywe uji wenye pilipili mtama,kwani pilipili mtama zina faida mbili kwa mzazi.
1.huondoa haraka makovu yaliyotokana na msuguano wa mtoto tumboni.
2.husaidia ongezeko la maziwa ya mama ili yapatikane ya kutosha kuweza kumnyonyesha mwanae na akapata afya njema
MBOGA MBOGA
K**a tunavyo juwa vyakula vya mboga mboga vinaumuhimu mkubwa sana katika kuchangia jambo hili hivyo mama mzazi anapaswa kutumia kwa bidii sana.
Kwa ushauri, elimu zaidi na matibabu unaweza kuwasiliana nasi kupitia njia ya WhatsApp no. +255767202621, .kimbokatz