Health Care

Health Care Our health is the single most priceless thing we get for free when we enter this world. It is our sole responsibility to take good care of it.

KUTOKWA NA KIJINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA( HEMORRHOIDS)MIWASHO, MAUMIVU NA VIMBE KATIKA TUNDU LA HAJA KUBWABawasiri ni u...
15/10/2020

KUTOKWA NA KIJINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA
( HEMORRHOIDS)

MIWASHO, MAUMIVU NA VIMBE KATIKA TUNDU LA HAJA KUBWA

Bawasiri ni ugonjwa ambao unatokana na kuathirika kwa mishipa ya sehemu ya ndani na nje ya tundu la haja kubwa na hupelekea wakati mwingine kutoa damu wakati wa kutoa haja kubwa.

Ugonjwa huu unasababisha muwasho na maumivu makali katika tundu la haja kubwa.

Ila kwasasa ugonjwa huu unawaathiri mpaka watoto wa umri wa chini kabisa:
CHANZO CHA UGONJWA WA BAWASIRI.

Bawasiri ni tatizo linaloanzia kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Huu mfumo ukishakua mbovu hupelekea kutokupata choo vizuri(Haja kubwa)

Mfumo mbovu wa mmeng'enyo wa chakula unasababisha chakula kisimeng'enywe vizuri kwenye utumbo mdogo na hivyo kupelekea chakula kupiliza kwenda moja kwa moja k**a kilivyo kwenda kwenye utumbo mkubwa ambapo maji maji kutoka kwenye chakula hufyonzwa na kuacha chakula kikiwa kikavu.Inapofikia wakati wa kupata choo; choo kinakua kikavu hivyo unatumia nguvu nyingi kukisukuma choo kitoke.

Hali hii hupelekea misuli ya haja kubwa kutanuka na kupelekea kukwanguliwa na choo kigumu na hivyo kinyama kuanza kujitengeneza, Hivyo husababisha kuanza kusikia maumivu na miwasho kwa ndani, na mara nyingine kupata choo chenye damu.

Hivyo basi kadri unavyoendelea kupata choo kigumu misuli ya tundu la haja kubwa huendelea kuathirika zaidi k mpaka kinatokeza.

Mtu mwenye afya nzuri anapata choo kulingana na milo aliopata kwa siku. K**a unauwezo wakupata milo mitatu kwa siku, unasitahili kupata choo mara tatu kwa siku, tena choo chako kitoke na urefu sawa wa ndizi mbivu, bila kujikatakata k**a kile cha mbuzi.

Bawasiri pia huweza kusababishwa na:

-Kufanya mapenzi kinyume na maumbile,

- Ujauzito

- kuhara kwa mda mrefu

-Kutopata choo kwa mda mrefu
DALILI ZA UGONJWA WA BAWASIRI

- Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa. Huu muasho unakuja kwa kujirudia mara kwa mara baada ya muda furani.

- Kukatishwa kwa haja kubwa na kurudi ndani wakati wa kujisaidia. Kitendo hiki huongeza msuguano katika mishipa ya ndani ya tundu la haja kubwa.

- Kujitokeza kwa uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa. Uvimbe huu unaanza kuota k**a upele na huambatana na miwasho na maumivu makali.

- Kujitokezea kwa kijinyama katika tundu la haja kubwa. Kinyama hiki kinaanzia ndani ya tundu la haja kubwa na kutokea nje ya Tundu la haja kubwa. Hatua hii huashiria tatizo limesha kuwa kubwa na una hili tatizo la bawasili kwa muda mrefu, na linaweza kusababisha vifo vya gafla kwa sababu mishipa inayosafirisha damu ndio inakwanguliwa na mwishowe kuathirika.

Chukua tahadhari mapema kabla hujaathirika sana au upoteze maisha; kwasababu hiki ni chanzo cha kupatwa na magonjwa mengine mengi ya kiafya.

- Kujisaidia kinyesi chenye damu na kunuka kwa harufu mbaya sana

- Kupumua na kushindwa kuzuia kinyesi wakati ukipumua(kujamba na kutoa haja kubwa)
MADHARA YA UGONJWA WA BAWASIRI

Upungufu wa damu mwilini

Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa na kusababisha mishipa ya sehemu ya haja kubwa kukwanguliwa.

Kuna uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya utumbo (Cancer) kwasababu kile kinyama kinakaa k**a kidonda

Kutopata hamu ya tendo la ndoa kwa jinsia zote. Yaani Mwanamke na Mwanaume.

Kuathirika kisaikolojia na hupelekea kuptojiamini katika hadhara ya watu hasa pale miwasho inapoanza.

Kuvuja damu, maumivu ya mda mrefu na hupelekea kushindwa kukaa.

Maumivu ya mgongo ya mara kwa mara na kiuno.

Kwa msaada, ushauri na tiba wasiliana nami moja kwa moja
WhatsApp
https://wa.me/255716497275

Call and text
255689606285

Prepared Dr Chaula

🔰Ijali afya yako.

UGONJWA WA PID NI CHANZO CHA UGUMBA KWA WANAWAKE WENGI, JE NINI SULUHISHO...!!!UGONJWA WA PID (Pelvic Inflammatory Disea...
13/10/2020

UGONJWA WA PID NI CHANZO CHA UGUMBA KWA WANAWAKE WENGI, JE NINI SULUHISHO...!!!

UGONJWA WA PID (Pelvic Inflammatory Disease) au Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke. Mara nyingi wataalamu wengi huuchanganya wakifikiri ni UTI.

✍🏻Magonjwa ya zinaa ndio sababu kuu ya wanawake kupata maambukizi katika mfumo wa uzazi yaani (PID). Mwanamke 1 kati ya wanawake 8 waliopota PID katika wakati wowote ndani ya maisha yao hupata tabu kushika mimba.

PID NI NINI?

✍🏻PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa k**a gonorrhea na chlamydia, Ila kuna aina us maambukizi mengine mbali na magonjwa ya zinaa yanaweza kusababisha maambukizi ya PID.

JE! MWANAMKE HUAMBUKIZWAJE PID?

✍🏻Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na:

➡️K**a una ugonjwa wa zinaa na haujatibiwa kwa muda mrefu.
➡️Kufanya ngono zembe isiyo salama (yani kulala na wanaume tafauti tafauti)
➡️Kuwa na mpenzi ambaye ana wanawake wengi nje
➡️Kuwa na historia ya PID hapo nyuma
➡️Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
➡️Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
➡️Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa mpango
➡️Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID

DALILI NA UTAMBUZI WA PID

✍🏻Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni:
👉Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
👉Kupata maumivu ya mgongo
👉Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
👉Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
👉Kupata maumivu au kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa
👉Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
👉Kupata homa
👉Kupata damu nje ya siku zako zako za kawaida kupata damu ya hedhi
👉Wakati fulani kuhisi kichefuchefu k**a mwanamke mja mzito na kutapika

VIPIMO VYA PID

➡️Kuchunguza mkojo ili kufahamu k**a mgonjwa ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au mwenye uwezo wa kubeba mimba
➡️Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
➡️Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na uambukizi huo au k**a kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa kitaalamu huitwa (Full Blood Picture).
➡️Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa (Cervical culture)
➡️Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya kujamiiana, k**a vile virusi vya ukimwi na kisonono.
➡️Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia k**a kuna athari yeyote katika mfumo wake wa uzazi.

MADHARA YA PID ISIPOTIBIWA

👉Maumivu ya mfuko wa uzazi ya kudumu
👉Kupatapata ugumu wa kushika mimba
👉Ectopic pregnancy (mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi)
👉Kuziba kwa njia ya uzazi

JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI

➡️Njia hakiki ya kujizuia na maambukizi haya ni kuwacha ngono zembe na kufanya ngono salama ndani ya ndoa halali kwani zina ni haramu, k**a utakuwa mwenye kutaka dhambi basi tumia kondomu ili usiwaambukize watu wengine
➡️Wahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa
huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa au anatembea na wanawake wengine
➡️Fanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI) khususan ugonjwa wa chlamydia ufanyie vipimo kila mwaka mara 1
➡️Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema.

MATIBABU

✍🏻Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya zinakuwa hazina msaada tena maana tatizo linakuwa limeenea. Ukitumia unaweza kupona kwa muda na baadae tatizo kujirudia.

✍🏻TUMIA maji kwa wingi, mboga za majani, Vitunguu swaumu (kutafuna asubuhi na jioni), Vitunguu maji (juice take, au saga changanya na asali, au chemsha), matunda kwa wingi, Kunywa mchai chai asubuhi na jioni, mtindi mara kwa mara, tafuna karoti mbichi, Epuka vyakula vya viwandani na madawa ya hospitali itakusaidia pia KUEPUKA na KUZUIA MAGONJWA MENGINE YA UZAZI KWA URAHISI.

☎️Kwa ushauri wa BURE, msaada na tiba wasiliana nami moja kwa moja
WhatsApp
https://wa.me/255716497275

Call and text
255689606285

🔰Ijali afya yako.

NAMNA SAHIHI YA KUKABILIANA NA MAAMBUKIZI YA BACTERIA UKENI.1. Kuosha sehemu ya siri kwa kutumia maji na kitambaa kisafi...
11/10/2020

NAMNA SAHIHI YA KUKABILIANA NA MAAMBUKIZI YA BACTERIA UKENI.

1. Kuosha sehemu ya siri kwa kutumia maji na kitambaa kisafi kila siku na kuosha kuanzia mbele kuelekea nyuma, epuka kurudia ukishafika nyuma.

2. Epuka matumizi ya sabuni zenye manukato, bubble baths, vaginal deodorant products, na bath powder.

3. Vaa chupi ambazo hazibani sana na zilizotengenezwa kwa kutumia pamba au hariri (silk), epuka synthetic underwear.

4. Epuka mavazi yoyote ya kubana k**a jeans za kubana kila wakati nk.

5. Badilisha nguo za ndani (chupi) kila zinapopata unyevunyevu.

6. Fua chupi zako kwa maji yenye nyuzi joto 90 na kuendelea anika juani.

7. Tumia pad wakati tu unapozihitaji (k**a umeingia kwenye mzunguko wako wa hedhi).

8. Kula mlo wenye virutubisho vyote kamili (balanced diet) na Kunywa Maji kwa wingi.

9. Epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako ambaye amepata maambukizi ya fangasi.

10. Epuka kuoga maji moto sana (hot baths) tumia maji ya uvuguvugu, hii kwa wale ambao wanaishi kwenye ukanda wa joto (tropical climate)
11. Matumizi ya vifaa vya ngono (s*x toys), vifaa vya upangaji uzazi (diaphragms, cervical caps) yanaweza kuleta kujirudia kwa maambukizi ya fangasi k**a havitaoshwa na kukaushwa vizuri baada ya kutumiwa.

12. Baadhi ya tafiti zilizofanyika, zimethibitisha ya kwamba unywaji wa maziwa ya mtindi (yoghurt) yenye live culture, husaidia kupunguza maambukizi ya fangasi.

Prepared by Dr Chaula

For more help Contact with us :-
WhatsApp
(+255) 716497275

Call and text
(+255) 689606285

Ukiwa umependa makala hii na ungepanda kupata elimu sahihi ya afya kila siku, usisahau kubonyeza link ya ukurasa Wetu hapo chini ili kutopitwa na makala zetu pendwa za afya.
https://chat.whatsapp.com/LVDN47FDsVlBcOWnc3hmJ3

“JIFUNZE na Chukua Hatua Juu Ya Afya Yako”.

SABABU ZA TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI.Mara nyingi gesi tumboni inaletwa na chakula ambacho hakijameng’enywa vizuri au...
10/10/2020

SABABU ZA TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI.

Mara nyingi gesi tumboni inaletwa na chakula ambacho hakijameng’enywa vizuri au kumeza kiasi kikubwa cha hewa. Mtu anapokula au kunywa anameza kiasi fulani cha hewa, hata hivyo zipo baadhi ya sababu zinazomfanya mtu ameze kiwango kikubwa zaidi cha hewa na kusababisha tumbo kujaa gesi. Sababu hizi ni pamoja na: .
➢ Kula au kunywa kwa haraka. .
➢ Uvutaji wa sigara.. ➢ Hitilafu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
➢ Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
➢ Msongo wa mawazo na hasira.
➢ Kula haraka haraka na kula unaongea.
➢ Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula hasa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
➢ Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi k**a maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k

Dalili za tatizo la tumbo kujaa gesi.

➢ Kutoa hewa mara kwa mara kupitia mdomoni (kubeua).
➢ Kutoa hewa mara kwa mara kupitia njia ya haja kubwa.
➢ Tumbo kuunguruma mara kwa mara.
➢ Tumbo kuwa k**a limebanwa na mkanda au limejaa sana.
➢ Kuharisha damu
➢ Kukosa hamu ya kula na kutapika
➢ Hali ya homa na uchovu.

Mtu mwenye tatizo hili asipotibu kwa wakati atakua kwenye hatari ya kupata tatizo la kupata choo kwa shida. Na hivyo anapata tatizo la kutokwa na kijinyama katika njia ya haja kubwa yaani bawasili au mgolo.

Na k**a ni mwanaume asipotibu kwa wakati atapatwa pia na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Mtu mwenye tatizo hili anashauriwa kutokula vyakula na vinywaji vyenye vyenye carbon (mf, cola kwa aina zake) lakini tatizo likizidi nivema kupata ushauri wa daktari aliye karibu nawe.

Tunapatikana Dar Es salaam Tanzania, na k**a upo mkoani unaweza kupata msaada na huduma zetu kokote ulipo kwa wakati kwa kuwasiliana nami moja kwa moja
WhatsApp
https://wa.me/255716497275

Kawaida
255689606285

WhatsApp group bonyeza link ya hapo chini ujiunge bure ili usipitwe na makala ya afya yako
https://chat.whatsapp.com/LVDN47FDsVlBcOWnc3hmJ3

🔰Ijali afya yako...

TATIZO LA HARUFU MBAYA YA KWAPA NA JINSI YA KULIZUIA..!!Jasho ni moja ya njia maalumu ya mwili ya kurekebisha kiwango ch...
09/10/2020

TATIZO LA HARUFU MBAYA YA KWAPA NA JINSI YA KULIZUIA..!!

Jasho ni moja ya njia maalumu ya mwili ya kurekebisha kiwango cha joto la mwili, ila inapofika wakati jasho hili linaanza kutoa harufu mbaya huwa kero kwa mtu anayetoa harufu na kwa jamii nzima inayomzunguka.

Kwa kawaida jasho huwa halina harufu, kwani jasho ni mchanganyiko wa maji na aina mbalimbali za madini ya chumvichumvi yanayotolewa k**a taka mwili,
Harufu mbaya ya kwapa husababishwa na bakteria ambao humeng`enya aina fulani ya protini inayozalishwa pamoja na jasho kutoka katoka tezi maalumu za jasho ziitwazo apocrine glands. Tezi hizi zinapatikana katika maeneo ya matiti, maeneo ya sehemu za siri, katika kope za macho huku idadi kubwa ya tezi hizi ikiwa katika makwapa hivyo kupelekea kiwango kikubwa cha jasho kuzalishwa katika maeneo ya makwapa.
Jasho hasa la kwapa kutoa harufu ni jambo la kawaida lakini kwa baadhi ya watu hali hii ya kunuka kwapa huwa sugu sana na hivyo kuwa kero kwao na jamii kwa ujumla.

Ili kupunguza harufu au kuimaliza kabisa yapaswa kupunguza pia kiwango cha jasho unalozalisha kwa siku kwa kufanya yafuatayo;

√. Kula mlo kamili na fanya mazoezi ili kupunguza mwili kwa sababu watu wanene huathiriwa sana na tatizo hili kwa sababu ya mikunjo mikunjo ya ngozi yao hivyo kutoruhusu jasho kukauka mwilini.

å Vaa nguo za pamba , nguo za aina hii husharabu (hunyonya) jasho la mwili na kukuacha mkavu, epuka pia nguo zinazokubana sana.

å Tumia manukato mbalimbali ili kupambana na harufu pia tumia dawa maalumu zinazoweza kupunguza kiwango cha jasho linalizalishwa kwenye makwapa (muone daktari wako kwa kupata dawa hizi)

√• Kuwa na tabia ya kuoga mara kwa mara ili kuondoa kiwango cha jasho kinachokuwa kimezalishwa hivyo kutoruhusu bakteria kufanya mmeng’enyo. Pia kila baada ya kufanya shughuli yoyote ya kukutoa jasho, ni vizuri kutumia medicated soap ili kuua bakteria wanaozalisha harufu mbaya.

å Epuka vyakula na vinywaji vinavyosababisha uzalishaji mkubwa wa jasho. Mfano vyakula k**a pilipili, kahawa, pombe, vitunguu.

å Nyoa nywele za kwapani na tunza makwapa yako katika hali ya usafi. Kwa sababu uwepo wa nywele hizi husababisha jasho kutokauka. hivyo bakteria kuzalisha harufu kutokana na jasho hili.

å Badilisha nguo na kuvaa nguo safi kila siku ili kupunguza mrundikano wa jasho.

Muone daktari wako endapo una matatizo yafuatayo.
ikiwa unatoka jasho kwa wingi sana wakati wa usiku mpaka unalowanisha nguo au shuka zako.unatokwa na jasho kwa wingi kuliko kawaida ulivyozoeaunatoka jasho kipindi cha baridi.jasho lina kunyima uhuru wa kufanya kazi zako za kila siku.Uzalishaji wa jasho usio wa kawaida unaweza kuwa ishara ya uwepo wa tatizo la kiafya hivyo ni vyema kumuona daktari wako haraka iwezekanavyo.

Prepared by Dr Chaula

For more help Contact with us :-
WhatsApp
(+255) 716497275

Call and text
(+255) 689606285

Ukiwa umependa makala hii na ungepanda kupata elimu sahihi ya afya kila siku, usihaau kulink hapo chini ukurasa Wetu ili kutopitwa na makala zetu pendwa za afya.
https://chat.whatsapp.com/LVDN47FDsVlBcOWnc3hmJ3

“JIFUNZE na Chukua Hatua Juu Ya Afya Yako”.

UNAIJUA SIKU YAKO YA KUTUNGA MIMBA...!!!Baadhi ya Mambo yanayokuchanganya katika KUHESABU MZUNGUKO WA HEDHIK**a wewe ni ...
07/10/2020

UNAIJUA SIKU YAKO YA KUTUNGA MIMBA...!!!

Baadhi ya Mambo yanayokuchanganya katika KUHESABU MZUNGUKO WA HEDHI

K**a wewe ni mara yako ya kwanza kabisa kujifunza mzunguko wa hedhi basi itakufaa kuwa na KALENDA yako ya ukutani na PENI nyekundu na nyeusi k**a utaweza.

Mambo muhimu ya kuweka akilini haya:
1- Siku ya kwanza umepata bleed (wengi husema nimeingia siku zangu) ndio siku ya kwanza ya mzunguko wako wa hedhi katika mwezi husika.

2- Siku ya mwisho ya mzunguko wako wa hedhi ni siku moja kabla hujapata hedhi ya mwezi mwingine.

3- Mzunguko wa hedhi sio lazima kila mwezi uje siku ile ile na tarehe ile ile...

4- Mzunguko wa hedhi sio lazima kila mwezi uwe na urefu/ukubwa uleule.

5- Mzunguko wa hedhi ni nini?
Ni idadi ya siku unazochukua kuanzia siku ya kwanza umepata hedhi/bleed mpaka siku moja kabla ya kupata hedhi nyingine ya mwezi mwingine.

6- Siku za Hedhi ni nini?
Siku za Hedhi ni siku kuanzia siku ya kwanza umepata bleed/damu mpaka siku ya mwisho zinapokata

7- Siku za Hatari ni nini?
Siku za Hatari ni siku zote ambazo unaweza kufanya tendo la ndoa na kupata mimba.

8- Siku za Uzazi ni zipi?
Siku za uzazi ni zile siku ambazo kwa mtu anayetaka kupata mimba ndio siku zenye uwezekano mkubwa wa kupata mimba, ni siku ambazo dalili zote za yai kutokea au kutoka zinaonekana (kawaida ni siku 3-4)

9- Siku ya Yai Kupevuka au siku ya Mimba (ovulation)
Hii ni siku ambayo yai hutoka ktk vifuko vya mayai au ovari na kuelekea kwenye mirija ya uzazi ili kushika mimba kwa kiingereza inaitwa ovulation day.

10- Mwanamke akisema ameingia kwenye siku zangu basi anamaanisha ameanza kutoa damu ya hedhi/bleed. K**a atasema leo niko mwezini siku ya pili basi anamaanisha ako katika siku ya pili ya hedhi na siku ya pili ya mzunguko wa hedhi.

KWA MFANO
K**a mwezi wa MEI ulianza kupata hedhi siku yeyote ile basi siku hiyo ya kwanza ulipopata damu ndio siku yako ya kwanza ya mzunguko wa hedhi kwa mwezi huo wa MEI mfano k**a ASHURA ataingia siku zake tarehe 05/05/2020 basi tar 22/05 ni siku yake ya 18 ya mzunguko wa hedhi. Haijalishi k**a atamaliza damu yake ya hedhi tarehe 08/05 au kabla ya hapo. Kwa hiyo kitu muhimu hapa ni kuwa siku za mzunguko wa hedhi na siku za hedhi ni vitu viwili tofauti.


K**a umenielewa vizuri basi twende pamoja hapa kufahamu jinsi ya kuhesabu jumla ya mzunguko...

Ili kujua mzunguko wako ni siku ngapi.
Chukua tarehe ya siku ya kwanza uliyoona hedhi na tarehe ya siku moja kabla ya hedhi iliyofuata.

Kwa mfano tuseme January wewe ni ASHURA na uliona damu ya hedhi tarehe 20 na ukaja kuona tena hedhi tarehe l6 mwezi wa pili.
Utahesabu kuanzia tarehe hiyo 20.JANUARI mpaka tarehe l5 na jumla yake ndiyo mzunguko wako wa hedhi....
Hebu tuone hesabu zinavyokuwa 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31, 01, 02, 03, 04, 05, 06, 07, 08, 09, 10, 11, 12, 13, l4 na l5. Kwa hesabu hii mtu anakuwa na mzunguko wa siku 27 kwa maana tutasema mzunguko wa ASHURA ni mzunguko wa siku 27.

Chukua kumbukumbu zako na tarehe muhimu kisha fanya hesabu uone mzunguko wako unaendaje jumla ya siku ngapi.

Namna ya kuzitambua siku za hatari za kubeba mimba.

Ili uweze kujua siku za kubeba mimba
👇🏻
Chukua jumla ya siku za mzunguko wako mzima kisha toa siku 14,,, jibu utakalolipata ndio siku yenyewe ya uzazi. Kwa mfano tuseme mzunguko wako huchukua siku 30.
Siku ya mimba itakuwa 30-14=16 kwa maana unapoanza hedhi, siku ambayo tunategemea yai lishuke kwa ajili ya upevushaji ni siku ya 16. Ila kwa sababu ya mazingira, vyakula na ulaji homoni zinaweza kubadilika yai likashuka mapema kabla ya siku ya 16 au kuchelewa kushuka hivyo huwa tunaweka siku 4 mbele na siku 4 nyuma ya siku ya mimba kwa ajili ya tahadhari, hii ndio tunaita siku za hatari
•••Kwa mfano kwa mzunguko wa siku 30 tumeona siku ya mimba ni siku ya 16 ktk kalenda.

Kwa mzunguko wa siku 30 Siku za hatari zitakuwa hivi 16-4=12 na 16+4=20 kwa maana siku za hatari tunasema ni kuanzia siku ya 12 mpaka siku ya 20 katika mzunguko wa mtu mwenye siku 30.

Kwa maana ishu ya muhimu ni wewe kujua kwanza mzunguko wako huchukua siku ngapi kisha kufanya hesabu.

Sasa kwa ndugu yangu mwenye mzunguko ambao unarukaruka haueleweki ni lazima tuelekezane namna ya kulizuia hili, na bila shaka utakuwa una baadhi ya dalili k**a;

>>Ukavu ukeni
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kutoa jasho usiku
- Maumivu chini ya kitovu su chini ya kitovu wakati wa hedhi
- Upungufu wa hamu ya tendo la ndoa
- Mabadiliko ya siku za hedhi na kupata hedhi kwa muda mrefu unaozidi siku
-Kukosa ute wa uzazi
-(heavy bleeding, au kujaza pedi moja kwa saa moja)
- Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye mabonge mabonge wakati wa hedhi
- Uchovu wa mara kwa mara bila sababu
- Hasira za mara kwa mara
- Kukosa usingizi

Njia sahihi ya kuliepuka hili ni pamoja na kujiwekea utaratibu wa kula, mboga za majani, supu ya nyama au mchemsho wa ndizi, kitunguu maji, korosho, viazi vyekundu, fenesi, mrehani, asali mbichi, maziwa aina yoyote, msamitu, soya, mbegu za tikiti au maboga, mapera, mimea jamii ya mikunde, tende na karoti huku ukiachana na soda, vinywaji baridi wakati wa hedhi, kahawa na ngano ya kukobolewa k**a mkate mweupe, chapati na maandazi...

K**a una dalili zaidi ya moja kwa mfano tuseme huwa unahisi maumivu ya kiuno, uchafu kutoka ukeni, mgongo kuuma, maumivu chini ya kitovu, kuhisi hali ya homa baadhi ya nyakati, kukosa hamu ya kufanya mapenzi, kuwa mkavu wakati wa kufanya mapenzi na dalili nyinginezo kuhusiana na mfumo wa uzazi hapo ninakushauri kutumia Tiba maalum ambazo zitakusaidia kutatua.

K**a tatizo limeshakuwa sugu kiasi limepelekea mimba kushindwa kunasa na unahitaji mtoto kwa haraka ili kuleta amani ya moyo na hata ndani ya ndoa, ninazo dawa asili kwa ajili ya kusafisha mirija, kuondoa uchafu katika uzazi na kuongeza wingi wa homoni ili mzunguko wa hedhi uzidi kubalansi + mayai kupevuka kwa wakati na kulea mimba isichoropoke.

☎️Kupata Tiba, ushauri na elimu zaidi unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa msaada zaidi
WhatsApp
https://wa.me/255716497275

Call and text
255689606285

WhatsApp group bonyeza link ya hapo chini ujiunge bure
https://chat.whatsapp.com/LVDN47FDsVlBcOWnc3hmJ3

🔰Ijali afya yako.

JE KIPIMO CHA MIMBA KINASOMA BAADA YA MUDA GANI? Muda gani mzuri wa kupima mimba ni upi?Unapotaka kubeba mimba au unapok...
06/10/2020

JE KIPIMO CHA MIMBA KINASOMA BAADA YA MUDA GANI?
Muda gani mzuri wa kupima mimba ni upi?

Unapotaka kubeba mimba au unapokua na wasiwasi kwamba umepata mimba, mara nyingi hua ni changamoto kwa wasichana kwani wengi wao hujikuta wanapima siku hiyohoyo au kesho yake kuangalia k**a mimba imeingia kitu ambacho hata kwa vipimo vya kisasa zaidi huwezi kupata majibi sahihi kwa muda mfupi hivyo.

Muda mzuri wa kupima mimba kwa uhakika zaidi ni pale unapokosa siku zako za hatari za mwezi unaofuata, kipindi hiki zile homoni ambazo kitaalamu ndio zinasomwa kwenye mkojo mtu akiwa na mimba kwa jina la human chorionic gonadotrophin hormone zinakua tayari ziko za kutosha hata kwa vile vipimo ambavyo havina nguvu sana vinasoma kwa uhakika.

Muda unaotumika kwa kipimo kusoma inatofautiana kwa wanawake tofauti..

Wakati unataka kupima mimba unatakiwa ujue kwamba wanawake wanatofautiana sana wao kwa wao kutokana na urefu wa mizunguko yao yaani wengine mizunguko mirefu na wengine mfupi.

Yai la mwanamke na mbegu ya mwanaume vinapokutana huchukua siku saba mpaka kumi kuweza kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi, baada ya hapo baada ya siku mbili mpaka tatu ndio mimba inaweza kusoma...hivyo kwa ujumla tunasema inaweza kuchukua siku 14 mpaka siku 21 kusoma k**a mimba imeingia au haijaingia baada ya kulala na mwanaume. wanawake wengine hutokwa na damu kidogo mimba inapojishikisha kwenye ukuta wa uzazi kitaalamu tunaita implantation bleeding, damu hii hua inakua kidogo sana kuliko ile ya kawaida ya hedhi lakini kipindi hiki mimba inakua bado haijasoma kwenye kipimo.

Unatakiwa upime saa ngapi?

Kila unavyopima kipimo cha mkojo, unakua unapima homoni ya human chorionic gonadotrophin hormone ambayo nimeitaja hapo juu.

Muda mzuri ambayo homoni hiyo inaonekana ni asubuhi, hivyo zingatia kupima mimba asubuhi kwa majibu mazuri zaidi, wakati mwingine ukipima mchana unaweza kuona mistari ambayo inafifia yaani haina rangi nyekundu ya kutosha.

☎️Kwa msaada, ushauri na tiba wasiliana nami moja kwa moja
WhatsApp
https://wa.me/255716497275

Call and text
255689606285

🔰Ijali afya yako.

TATIZO LA CHAKULA KURUDI KWENYE KOO LA CHAKULA ( Gastroesophageal Reflux Disease ) ;Hili ni tatizo la chakula au maji ku...
05/10/2020

TATIZO LA CHAKULA KURUDI KWENYE KOO LA CHAKULA ( Gastroesophageal Reflux Disease ) ;

Hili ni tatizo la chakula au maji kurudi katika koo la chakula mara baada ya kuwa kimeshamezwa, lakini ilikuelewa vizuri tatizo hili linavyotokea tunatakiwa kujua vizuri jinsi chakula kinavyofika tumboni.

Mara baada ya mtu kutafuna chakula au kunywa maji,chakula husafirishwa kupitia mrija wa chakula (Esophagus) hadi tumboni lakini juu kidogo kati ya tumbo na mrija huu wa chakula kuna kizuizi kilicho na sura ya bangili ( lower esophageal sphincter ), kibangili hiki hufanya kaxi ya kuzuia chakula kisurudi mdomoni au kwenye koo baada ya kuwa kimeshamezwa, kibangiri hiki ndicho kinacho mfanya mtu ale huku amening'iniza kichwa chini miguu juu na chakula kisirudi tumboni. baada ya chakula kuingia tumboni , huchanganyikana na vimengenya pamoja na tindikali ambayo hufanya kazi ya kuua vimelea vyote vilivyoingia pamoja na chakula,mchanganyiko huu husababisha chakula kupata chachu ambayo matokeo yake huwa ni raihisi sana kuweza kurudi katika koo la chakula endapo kizuizi cha juu ya tumbo kitakua kimepata hitilafu au viambukizi. dalili kuu za tatizo hili ni kiuungulia cha mara kwa mara, dalili za tatizo hili kwa watoto hujionesha pale mtoto anapotapika kupita kiasi au kupali mara kwa mara.

CHANZO CHA TATIZO;
Kunasababu nyingi zinazoweza kuambatanishwa na tatizo lakini wengine hujitokeza kwa pamoja ,

1. Kudhofika kwa utendaji kazi wa kizuizi cha juu ya tumbo ( Lower esophageal sphincter) ,
kudhohofika kwa kizuizi hiki husababishwa na utumiaji wa madawa k**a nitrates,bisphosphonates,estrogen,oral contraceptives,progesterone,alpha adrenergic agents,theophyline,calcium channel blockers,benzodiazepines,anticholinergics, na tricyclic antidepressants ,aina ya dawa hizi zimeonekana kuharibu sana utendaji kazi wa kizuizi hiki.
~ kuvuta sigara ,kula chakula ndani ya muda mchache kabla ya kulala na unywaji pombe, hupunguza nguvu ya misuli ya kizuizi hiki pamoja tumbo kwa ujumla.
~ ulaji vyakula k**a chocolate,vinywaji vyenye caffeine,kula chakula chenye nyanya nyingi pamoja na matunda au juisi yenye chachu nyingi,hupelekea chakula kutaka kurudi kwenye koo.

2.Mfumo dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula ( hasa wenye kisukari ).

3.Tindikali ( Hydrochloric acid) kuzidi tumboni.

4.Ngiri ya tumbo.

5.Kuongezeka kwa uzito wa sehemu ya chini ya tumbo kutoka na ujauzito.

DALILI ZA TATIZO HILI;
Dalili kuu ya tatizo hili ni kiungulia,ambayo huambatana na koo la chakula kuwaka moto,maumivu ya kifua,hali hii huzidi zaidi pale mtu anapolala kichwa kimeinama.kiungulia hiki huanza baada ya lisaa limoja na kuisha baada ya masaa mawili baada ya kula.

Dalili zingine ni k**a;
~Mdomo kua mchungu,
~kuijihisi chakula kinarudi kooni,
~Kupata shida wakati wa kumeza chakula,
~ Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka.
~Meno kuoza,matatizo ya fizi za meno,kupumua kwa shida.

m
MADHARA YAKE;
Tatizo hili linapozidi husababisha mtu kupatwa na tatizo la moyo pamoja na kansa ya koo la chakula.

UCHUNGUZI WA TATIZO HILI;
Uchunguzi watatizo hili hufanyika kwa njia ya x-ray,ambapo mgonjwa hupewa kiminika maalumu mabacho hukimeza ili kuonesha utendaji kazi wa mgumo wa chakula pindi atakapofanyiwa x-ray,lakini tatizo linapokua kubwa zaidi kipimo aina ya Endoscopy hutumika,hiki ni kimrija chenye kamera ni kadogo sana ,huingizwa kupitia koo la chakula hadi tumboni kisha kuonesha kwenye screen jinsi mfumo ulivyo.

MATIBABU YAKE;
Mara nyingi tatizo hili limepelekea watu kufanyiwa upasuaji baada ya kutumia dawa k**a za kupunguza tindikali ( antacid) na zingine k**a cholinergic agenys,Hestimamine H2 Antagonists,Prokinetic Agents na proton Pump Inhibitors.

JINSI YA KUJIKINGA KUTOKUPATA TATIZO HILI;
~Epuka vyakula vyenye mafuta mengi.

~Punguza mlo wako.

~Epuka aina ya vyakula vyote unavyohisi vinaweza kuchangia kwa tatizo lako.

~ Sitisha unywaji wa vinywaji vyenye caffein vyote.

~Kula kwa mpangilio ili chakula kiweze kumeng'enywa taratibu tumboni,sio kila wakati unakula tena kwa kuchanganya changanya.

~Acha sigara na pombe.

~Jaribu kupunguza mwili wako,k**a wewe ni mnene sana.

~Epuka kuvaa nguo zinaxokubana mwili.

~lala baada ya masaa matatu mpaka manne baada ya kula.

~Hakikisha unalala kichwa chako kiwe juu,yaani weka mto kichwa pindi unapolala.

zingatia hayo yatakusaidia, endapo k**a utashindwa kuondoa tatizo hili wasiliana na mimi ,ili uweze kupata dawa yenye kurekebisha mfumo mzima wa chakula na kuondoa dalili zote za tatizo katika mfumo huu.

☎️Ushauri, msaada na tiba wasiliana nami moja kwa moja
WhatsApp
https://wa.me/255716497275

Call and text
255689606285

WhatsApp group bonyeza link ya hapo chini ujiunge bure kwa kujifunza zaidi
https://chat.whatsapp.com/LVDN47FDsVlBcOWnc3hmJ3

🔰Ijali afya yako.

JINSI YA KUJIKINGA NA FANGASI SEHEMU ZA SIRIMaambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwep...
02/10/2020

JINSI YA KUJIKINGA NA FANGASI SEHEMU ZA SIRI

Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu k**a Candida albicans. Bakteria hawa kuwepo maeneo hayo huwa haina madhara yoyote yale.

Inapotokea Bakteria hawa wakaongezeka kwa wingi kuliko uwezo wa mwili kuweza kuwadhibiti, hapo ndipo hubadilika kutoka kuwa walinzi wa mwili na kuwa maadui wa mwili.
Dalili za tatizo hili la fangasi katika via vya uzazi.

1. Miwasho katika sehemu za siri.

2. Vipele vidogo vidogo sehemu za siri.

3. Kutokwa uchafu mzito k**a maziwa mtindi usio na harufu.
4. Vidonda au michubuko sehemu za siri.

5. Kupatwa na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

6. Kuvimba na kuwa na wekundu katika sehemu za siri za mwanamke

7. Kuhisi hali ya kuwaka moto kwenye via vya uzazi.

Jinsi ya kujikinga.

1. Epuka matumizi ya vinywaji na vyakula vyenye sukari nyingi maana huchochea kuongezeka kwa bakteria hawa.

2. Kula mlo kamili ili kupunguza mazingira ya bakteria hawa kuongezeka na kukushambulia.

3. Zingatia usafi wa nguo za ndani. Nguo ya ndani ivaliwe mara moja na ifuliwe na kuanikwa juani.

4. Usivae nguo ya ndani k**a haijakauka vizuri.

5. Tumia nguo za ndani za pamba na sio nailoni ili kuepusha kutunza joto jingi sehemu za siri.

Kwa msaada, ushauri na tiba wasiliana nami moja kwa moja
WhatsApp
https://wa.me/255716497275

Call and text
255689606285

Ukiwa umependa makala hii na ungepanda kupata elimu sahihi ya afya kila siku, usihaau kubonyeza link ya ukurasa Wetu ili kutopitwa na makala zetu pendwa za afya.
https://chat.whatsapp.com/LVDN47FDsVlBcOWnc3hmJ3

Pia Unaweza kuwa mwalimu kwa wengine kwa KUS-hare makala hii zaidi na zaidi ili wengi wapate Elimu hii uliyoipata wewe.

🔰“JIFUNZE na Chukua Hatua Juu Ya Afya Yako”.

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 10:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Health Care posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram