
05/07/2024
STROKE NI NINI?
Stroke au kiharusi ni tatizo linalotokea ghafla kwenye ubongo ambapo mtiririko wa damu kwenye eneo fulani la ubongo husitishwa ghafla au kupungua sana hivyo kusababisha eneo hilo la ubongo kukosa damu na virutubishi muhimu na seli za eneo hilo kuanza kufa.
Hili linaweza kutokea pale mishipa ya damu ya kuelekea kwenye eneo hilo ikiziba au mishipa ndani ya ubongo katika eneo hilo kupasuka. Seli za ubongo za eneo hilo zikianza kufa kwa kukosa damu, shughuli zote zinazoendeshwa na eneo hilo la ubongo husimama kwa mfano kumbukumbu au misuli.
*Dalili kuu za ugonjwa huu ni:*
1. Kuchanganyikiwa, mtu akipata shida ya kuongea na kuelewa anachoambiwa
2.Maumivu ya kichwa yanakwenda pamoja na kupoteza fahamu kwa vipindi na kutapika
3.Ganzi katika viungo vya uso, mkono na mguu na hasa vikiwa vya upande mmoja wa mwili
4.Kupata shida ya kuona kwa jicho moja au yote
5.Kupata shida ya kutembea vikichanganyika na kizunguzungu na kukosa mpangilio wa matendo ya mwili.
6.Msongo wa mawazo
7.Maumivu kwenye mikono na miguu yanayoongozeka baada ya viungo hivyo kufanya kazi au kutokea mabadiliko ya hali ya hewa.
8.Kupooza au udhaifu wa upande mmoja wa mwili
9.Kupata shida katika kufanya matendo ya kuonyesha hisia za mwili
10.Kushindwa kumudu matumizi ya kibofu cha mkojo au viungo vya njia ya haja kubwa. +255745517606