
25/07/2023
πππππππ
Tonsils ni lymph node ambazo hupatikana sehemu ya nyuma ya kinywa (mdomoni ) na sehemu ya juu ya koo.
πππππ ππππ
ni visturucture vidogo vidogo mfano wa harage vilivyopo katika mfumo wa Lymph ( ni sehemu ya mfumo wa kinga mwili) ambavyo hufanya kazi ya kuchuja vitu vigeni na visivofaa mwilini katika majimaji ya lymph k**a vile seli za kansa na maambukizi mbalimbali k**a virusi au Bacteria au Fangas. Ndani yake hizi Lymph nodes kunakua na seli za kingamwili ambazo husaidia kushambulia na kuharibu vimelea vya magonjwa (Bacteria, Kirusi, Fangasi)
Kwahyo kazi ya Tonsils ni kuchuja bacteria na vijidudu vingine vyenye kusababisha magonjwa .
Sasa Tonsils katika kazi yake hii zinakumbana na Virus au Bacteria na hushambuliwa hadi kusababisha Tonsils kupata maambukizi ambapo kitaalamu huitwa πππππππππππ ambapo sasa huku mtaani ndio tunasema nina Matonses au mtu fulani anaumwa Matonses.
Na bacteria kutoka Group A streptococcus ndio mara nyingi husababisha sana πππππππππππ.
ππππππ ππ πππππππ (ππππππππ)
1. Ugumu/Maumivu wakati wa kumeza chakula au kitu chochote
2. Maumivu ya masikio
3. Kupata Homa na Kuhisi Baridi kali
4. Maumivu ya kichwa
5. Vidonda kooni ambavo vitakua kwa muda wa k**a masaa 48 (siku 2) au na zaidi ya Maumivu ya vidonda yanaweza kuwa makali sana .
6. Maumivi ya koo na Taya ukishika
7. Tonsils kubadilika na kuvimba na kuwa nyekundu
8. Kushindwa kupumua vizuri
9. Kukosa hamu ya kula
ππππππππ
Matibabu ya Tonsils yanategemea na hali ya mgonjwa kwani muda mwingine ya naweza kupona yenyewe tu kati ya masaa 24 hadi masaa 48, lakini pia unaweza pewa Antibiotiki na k**a ikionekana mtu amekua anapata maambukizi ya mara kwa mara ya πππππππππππ maamuzi yanaweza kufanyika ya kufanya operation na kutoa kabisa Tonsils kitaalamu huitwa πππππππππππππ.
πππππ ππ πππππππππ ππ πππππππ (ππππππππ)
Ili uweze kujikinga na Tonsils zako kushambuliwa bhasi unatakiwa uwe unaosha mikono yako mara kwa mara ili kuzuia peleka vijidudu vya magonjwa mdomoni lakini pia kusanya usafi wa kinywa vizuri kabisa na muda mwingine kuwa unaenda kwa mtaalamu wa meno mara kwa mara.