07/05/2023
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa dharura wa Troika plus wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinazochangia Vikosi kwenye Force Intervention Brigade (FIC) leo tarehe 07 Mei, 2023.
Mkutano huo utajadili hali ya usalama Mashariki mwa Nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
. Hanc Tz updates