Jenga Misingi Ya Afya Bora

Jenga Misingi Ya Afya Bora AFYA KWANZA-PROGRAM❤️💪💪

"Udhaifu wa kutambua na kuyaelewa mambo  utakupelekea kukosea kwenye maamuzi  kitu ambacho kitakupeleka kwenye Matokeo m...
28/08/2025

"Udhaifu wa kutambua na kuyaelewa mambo utakupelekea kukosea kwenye maamuzi kitu ambacho kitakupeleka kwenye Matokeo mabovu yanayo endana na maamuzi mabovu yasiyo sahihi uliyo yafanya", Mfano; Unaumwa magonjwa halafu unakazana kumeza madawa huku ukijiaminisha akilini mwako kwamba unaimarisha Afya; Unacho kifanya hakina utofauti na kukazana kuweka madawa kwenye mmea ukiamini unaimarisha Afya ya mizizi ya mmea Badala ya kuweka mbolea/Rutuba🤔, Yaani Akili yako inawaza sahihi kuimarisha Afya lakini unacho kifanya hakina uhusiano wowote na kuimarisha Afya, Yote hii nikutokana na kukosa uelewe sahihi wa jambo unalo lifanya.

Maisha bila Maarifa sahihi ni zaidi ya Upofu, utajidanganya na kudanganywa, Utajipoteza na kupotezwa, Utajiangamiza na Kuangamizwa.., Hauwezi kuimarisha Afya kwa kutumia dawa kwasababu dawa ni siyo kirutubishi cha mifumo ya Afya bali dawa ni sumu/kemikali ambayo nguvu yake itaishia kwenye damu,

Ukitaka kuimarisha Afya ni lazima mwili upate Virutubisho/vijenzimwili hivi ndiyo vyenye uwezo wa kufyonzwa kwenye damu na kwenda kuimarisha mifumo ya Afya ambayo udhaifu wake ndiyo sababu kuu ya magonjwa yote mwilini Maana Mifumo ndiyo mizizi ya Afya, Hivo mizizi inapo kuwa dhaifu lazima Afya iwe dhaifu na magonjwa yanapata nguvu ya kujitawala bila kudhibitiwa.

K**a unaipenda Afya yako basi nikusihi sana, Haijarishi umefundishwa au umeambiwa au umeshauriwa na Dokta au mtu yeyote ni lazima kwanza ujiridhishe wewe mwenyewe Je, Ulicho jifunza au ambiwa au kushauriwa au kushawishiwa ni sahihi na kinaukweli ndani yake??, K**a haujalielewa jambo basi usilifanye na k**a unalifanya hakikisha umelielewa kwa kina, Acha kujiburuza au kuburuzwa hasa kwenye mambo ambavyo matokeo yake yanakupata wewe.

Imagine wewe vyakula vyako vikuu mwilini ni wanga na Junk foods, Vinywaji vyako ni vikuu ni Pombe na carbonated drinks, ...
26/08/2025

Imagine wewe vyakula vyako vikuu mwilini ni wanga na Junk foods, Vinywaji vyako ni vikuu ni Pombe na carbonated drinks, Mazoezi yako makubwa nikutembea, kukaa na kulala, Tiba zako kuu ukiumwa ni madawa ya hospital au Mitishamba🤔;

Asilimia kubwa mwili unapata vipaumbele vya magonjwa, Je, Utaweza kuyakwepa magojwa haya sugu kwa huo mtindo wako wa kuishi? K**a Kisukari, Presha, Saratani, Magonjwa ya Moyo, Magonjwa ya Figo,Ini na Mapafu, Magonjwa ya Uvimbe na Tezidume, *Unaweza kujijibu swali hili kulingana na Namna unavo ishi na mwili wako na Ukajipongeza au Kujisikitikia.

Ukiichukulia afya yako kawaida-kawaida basi Afya nayo itakuchukulia kawaida-kawaida, yaani mnazarauliana na hiyo ndiyo furaha ya magonjwa, Maana Afya au Magonjwa vinatokana na mahusiano ya kuishi baina ya mtu na mwili wake, Hivo unapo kuwa hauna mahusiano mazuri kiafya na mwili wako automatic unaidhoofisha mizizi ya Afya na Uhai wa mwili wako yaani Mifumo ya Afya na hiyo ndiyo faida kubwa kwa magonjwa maana kudhoofika kwa Afya ndiyo kurutubika kwa magonjwa, Bado nakukumbusha tu kwamba, Magonjwa siyo mdudu wa kusema unatakiwa umeze madawa ya kwenda kumuangamiza bali Magonjwa ni hali inayo tokea baada ya mfumo/mifumo ya Afya kudhoofika na hii chanzo chake ni wewe kuto ishi kiafya yaani mahusiano mabovu na mwili wako kwa mda mrefu.

Mahusiano mabovu siyo tu matumizi ya madawa ya kikemia wala Siyo tu Ulaji na Unywaji mbovu bali mahusiano mabovu ni pamoja na mwili kukosa vipaumbele muhimu vya Afya k**a Virutubisho, Mazoezi na Maji.

Unaweza kuishi vyovyote unavo penda, Ukala unacho penda, kunywa unacho penda haijarishi unavyo vipenda havina faida kiafya yaani Viburubisho Lakini ikiwa utakua mtumiaji mzuri wa Virutubisho vyenye nguvu ya Ant-oxdants na kiwango tosherevu k**a C24, Unafanya mazoezi angalau maramoja kwa siku hasa Asubhi na unakunywa maji ya kutosha hauwezi kupata magonjwa sugu kwasababu wewe utakua unaingiza sumu na takamwili lakini zinatoka kwa urahisi na Mifumo inajikarabati vizur kabisa maana vijenzimwili vinakuwepo.

JE, Unajua kwanini unaambiwa kuiaminisha akili yako kwamba umepona kwa kunywa madawa ya hospitalini yaani pharmaceutical...
23/08/2025

JE, Unajua kwanini unaambiwa kuiaminisha akili yako kwamba umepona kwa kunywa madawa ya hospitalini yaani pharmaceutical drugs Haina Utofauti kuidanganya akili yako ukaiaminisha kwamba umekua Tajiri kwa kupata mkopo na ukaanza kuishi kitajiri umesahau k**a ni deni!!, "Ukweli siku zote ni Mchungu lakini ndiyo Njia pekee ya Uhuru Na Uongo ni Mtamu lakini ndiyo njia pekee ya Utumwa"

Dawa za kikemia kazi yake nikutuliza magonjwa kwa mda mfupi na siyo kuyatibu na ndiyomaana baadhi ya magonjwa hospital unaambiwa hayanaga Tiba Nikwasababu dawa hazihusiki na kuimarisha Afya ila kuboost Afya, Hata siku moja usije kumeza madawa Ugonjwa ukatulia ukajiaminisha umepona utakua hauna utofauti na anaye ishi kitajiri kwa mkopo.

Na ndiyomaana huwa sishangai kukutana na watu wanao nambia Nimesha tumia madawa ya kila aina bila mafanikio au ugonjwa unatulia na kurudi, Shida ni kwamba wewe unatumia dawa kwaajili ya kutuliza Magonjwa na siyo kwaajili ya kuimarisha mifumo ya Afya ambayo udhaifu wake ndiyo sababu kuu ya magonjwa kujitawala mwilini.

Tunapo zungumzia Neno magonjwa maana yake ni Hali ya mifumo ya Afya kushindwa kuyadhibiti mazingira fulani yanayo ukumba mwili either ndani ya mwili au nje ya mwili, Mfano,
👉 Sukari inaingia mwilini lakini Mifumo wa kudhibiti sukari haufanyi kazi vizur lazima upate kisukar,
👉Sumu zinaingia lakini Mifumo ya kudhibiti sumu haifanyi kazi vizur lazima uweze ku-umwa. Na Matatizo ya Homoni imbalance, mifumo kushindwa kudhibiti presha, kushindwa kudhibiti Hali ya hewa either ya baridi au joto, kushindwa kuwadhibiti bacteria, kushindwa kudhibiti acidi, Kushindwa kudhibiti mmeng'enyo wa Chakula n.k.,

Magonjwa yote sugu chanzo ni udhaifu wa mifumo ya Afya na bila mifumo kuimarika hauwezi Ugonjwa wowote sugu mwilini.

Sasa unapo kuwa na tatizo k**a unahitaji kupona acha kutumia vitu vya kwenda kupambana na tatizo Bali tumia vitu vya kwenda kupambana na chanzo cha tatizo, Na Vitu hivyo ni Virutubisho pekee vyenye kiwango tosherevu kinacho kidhi mahitaji ya mwili mzima k**a C24/7, Kipitia Virutubisho hivi utaweza kudhibiti ugonjwa na kutoa sumu zote zisizo takiwa mwilini na vilevile utaweza Kuimarisha mifumo ya Afya na hapo utakua umetibu chanzo cha magonjwa.

Jitahid ukiweza kilasiku jipatie dakika 10, 20, hadi 30 za kukaa pekeako na kutafakari juu yako na Maisha yako kwa ujuml...
27/12/2024

Jitahid ukiweza kilasiku jipatie dakika 10, 20, hadi 30 za kukaa pekeako na kutafakari juu yako na Maisha yako kwa ujumla (Meditation) kwasababu bila kufanya hivi ningumu kuyatendea haki/usawa Maisha yako.

Kaa sehem yoyote yenye utulivu mkubwa ukiwa pekeako, iwe ni chumbani, iwe ni nyumbani, iwe ni gizani, iwe ni kanisani, iwe ni porini, iwe ni uwanjani au popote penye utulivu.

Bila kufanya hichi kitu ningumu kuyaelewa Maisha ni nini na ningumu ya kuyadhibiti Maisha yako kwa viwango yaani inil moderation.

Maisha ni asilimia 10% tu ya kinacho tokea na asilimia 90% namna unavo kipokea, Haijarishi kinacho tokea nikizuri kiasi gani au ni Kibaya kiasi gani Kinacho matter ni namna unavo kipokea kwenye akili na nafsi yako...

"Learn how to remain calm in any situation whether is too Good or too Bad"

Hivi unatambua kwamba ni zaidi ya mara elfu tatu  ndani ya kila saa moja unajizungumzishga mwenyewe na Akili yako kimawa...
23/11/2024

Hivi unatambua kwamba ni zaidi ya mara elfu tatu ndani ya kila saa moja unajizungumzishga mwenyewe na Akili yako kimawazo....

Siri Usiyo ijua ni Kwamba Maisha yako yapo chini ya Ubongo wako na Ubongo wako unafata amri Yako Kisha nao unatoa amri kwenye homoni za mwili na ndiyomaana unatakiwa kuhakikisha haingizi wala kutunza mawazo mabaya kwenye Akili yako kwasababu Ubongo wako unasikiliza na kutunza na endapo mawazo hayo yakijirudiaridia mara Kwa mara basi kunamuda yatakua matendo na madhara yake ndiyo hayo tunayo yaona kwenye Maisha ya watu wengi ....unaweza kuhisi amerogwa au una mapepo kumbe amejithiri kiakili kwasababu haujiwazii mazuri kwenye Maisha yako, muda wote hauna amani, umejaa Huzuni, unachuki bila sababu, unahasira, unawaza mikosi, Unaogopa, Hauna Imani, unakata tamaa🤔... Mawazo mabaya muda wote yanakuharibu kiakili kwasababu mawazo yako yanageuka kuwa matendo yaani unacho kiwaza ndicho unacho anza kukiamini na kupita kwenye njia zake.

Nikusihi sana, Haijarishi upo kwenye Wakati mgumu kiasi gani, Haijarishi unapitia magumu Mangapi kwenye Maisha hakikisha unavyo jizungumzisha baina yako mwenyewe ni Amani ,Furaha na matumaini Kwasababu Ubongo wako unasikiliza na unatunza kumbukumbu Hivo k**a unajizungumzia mabaya vitu visivyo na amani amini itakua Ivo kwasababu what you Think You become yaani Mawazo yatageuka kuwa Maisha halisi.

Kuwa makini na kila wazo unalo liingiza mara kwa mara kwa mara kwasabàabu Ubongo wako unasikiliza na unatunza k**a kumbukumbu kwahiyo kunamuda mawazo yako yatakua ni matendo...Hivo k**a unajizungumzisha mabaya, mikosi, Uoga, hofu basi vitakutesa sana hakuna uchawi mbaya k**a kujifunga kiakili yaani Kifikra,, unajifungia kwenye gereza ambalo wewe ndiyo chanzo bila kupata mwanasaikolojia Mzuri huwezi kuchomoka zaidi ya kuchanganyikiwa.

Kitu peke tunacho kitafuta kwenye maisha ni Furaha na Amani hakuna kitu kingine Hii ndiyo purpose ya Kuishi, hgivo basi kwa namna yoyote ile hakikisha haufanyi wala kutunza vitu vinavyo au vitakavyo haribu Amani ya Maisha yako... Ubongo wako unahitaji Furaha , Mawazo mazuri, Matumaini, Faraja, Imani, Unahitaji vitu vizuri na sahihi na SalamaTu...!

Lazima tufahamu ukweli kwamba maisha ni kilakitu kizuri au Kibaya, Magonjwa au Afya, kulia au kucheka, Uzima au vifo, sasa wewe focus na mambo mzuri.. maana ukijifunga kiakili nisawa na umeyafungia maisha yako kwa ujumla.

Maisha ni Asilimia 10% tu ya kila kinacho tokea na asilimia 90% ni namna unavo kipokea Yaaani haijarishi limetokea jambo baya kiasi gani namna utakavo lipokea ndivo litakavo kuwa baya Zaidi au litakua la kawaida kabisa hii utaweza ku-icontrol k**a unaelewa kwamba Kilakitu ni sehem ya Maisha ila k**a hautambui hili basi maisha yanaweza kuwa zaidi ya jela na chanzo ni wewe.

K**a binadamu tungezaliwa hatuna ufahamu yaani hatuna akili basi hakika Maisha yetu tungekua tunapangiwa na Mungu maana ...
29/09/2024

K**a binadamu tungezaliwa hatuna ufahamu yaani hatuna akili basi hakika Maisha yetu tungekua tunapangiwa na Mungu maana ndiye pekee angekua anazimiliki akili zetu na kutuongoza na sina hakika k**a tungekua na utofauti kwenye Maisha nahisi wote tungekua sawa kabisa.....

Binadamu tunajitahidi kuukimbia ukweli kwasababu tu ukweli umekaa upande mgumu unao umiza, Hivo basi binadamu wengi tunahisi Maisha ni mafanikio tu ila matatizo siyo maisha, Tunahisi misha nimajibu tu Ila siyo mitihani, Huku nikujifungia kwenye gereza lako mwenyewe maana mitihani inapo kuja mtu hayupo tayari kujifunza na kutafakari amekosea wapi ili arekebishe makosa Ila yupo tayari kuomba Mungu amtatulie matatizo Yake..Swali ni Je, kunahaja Gani ya Mungu kukupatia ufahamu/Akili..?

👉Usipo badilika wewe kifikra na Ki-matendo basi amini hakuna kitakacho weza kubadilika hata kwenye Afya yako

Kukosea na kujifunza ni sehemu ya maisha, Kosa lolote linalo fanyika kwenye Maisha yako sababu ni wewe haijarishi umekosea kwa bahatimbaya au kwa maksudi, kuendelea kufanya makossa bila kujifunza huo ni uzembe wako mwenyewe, Na ndiyomaana maana MUNGU anasema... "wangangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"... kiumbe pekee kilicho pewa ufahamu wa kuyamiliki Maisha yote duniani ni BINADAMU ndiyo pekee mwenye akili.

Ukweli ni Kwamba hakuna binadamu  ambaye nimzima yaani uzima wake umekamilika kiasi kwamba aishi huru na mwili wake tu b...
02/08/2024

Ukweli ni Kwamba hakuna binadamu ambaye nimzima yaani uzima wake umekamilika kiasi kwamba aishi huru na mwili wake tu bila kuusimamia akiamini yupo salama, Na ndiyomaana tunasema kuto kuumwa siyo Ishara ya kwamba Afya yako ipo salama bali ishara pekee ya kwamba upo salama kiafya ni kuangalia Namna Unavo ishi, je, mwili wako unapata vipaumbele vya Afya kuliko vya magonjwa..??? Hiyo Ndiyo njia Pekee ya kuyakwepa magonjwa hamna njia nyingine yoyote ya kweli itakayo kuepusha na magonjwa zaidi ya hii.

Magonjwa na Afya ni Vitu vinavyo shindana muda wote mwilini mwako, upande unao tawala mwili ni ule unao pokea vipaumbele vingi kuliko mwingine.

Inamaana kadri mifumo ya mwili wako inavo kosa vipaumbele vya Afya kwa kadri inavo fanya kazi hivi ndivo itakavo zidi kuchoka/kudhoofika na hii ni ishara tosha ya kwamba kuna muda magonjwa yatakua na nguvu kuliko afya maana udhaifu wa mifumo ya Afya ndiyo uimara wa magonjwa na uimara wa mifumo ya Afya ndiyo Udhaifu wa Magonjwa.

K**a unatamani Uwe na Uhakika wa Usalama wa Afya Yako usiache kuupatia Mwili Vijenzimwili yaani Virutubisho, mazoezi, maji ndiyo vitu muhimu kwaajili ya afya Yako... Ili mifumo yake ifanye kazi na kujiimarisha maana bila Virutubisho vimfumo itakua inafanya kazi ya kusababisha uhai na afya unayo ipata pasipo kujiimarisha na hii ndiyo itapelekea ifike muda magonjwa yawe na nguvu kuliko afya maana mizizi ya afya inakua tayari dhaifu.

Dr. Sylver Gilbert 0677867293

Haijarishi unatumia tiba ya Virutubisho vyenye nguvu kiasi gani haimaanishi ndiyo Ujiachie kula Junk foods yaani vyakula...
21/07/2024

Haijarishi unatumia tiba ya Virutubisho vyenye nguvu kiasi gani haimaanishi ndiyo Ujiachie kula Junk foods yaani vyakula na Vinywaji vya kisasa hasa ambaye tayari unachangamoto flani ya kiafya,,,, Ikiwa vitu Unavyo viingiza mwilini havina faida kiafya basi tambua kwamba mwili utakua unatumia nguvu kubwa kupambana navyo kuliko kuimarisha Afya yako, Maana kwako niviburudisho Ila Kwa mwili ni changamoto Yaani vinaenda kuwa Vikwazo,sumu/takamwili..... Chochote Unacho Ingiza mwilini either kinaenda kupunguza nguvu ya afya au kuongeza nguvu ya afya yako, Kwaivo Sasa lazima uwe makini navyo na uhakikishe mwili Unapata asilimia kubwa ya Mazingira ya kiafya zaidi kuliko Viburudisho..

Mwili nimkubwa na umeundwa Kwa Viungo Vingi yaani Mifumo Mingi ya ogani na Kila ogani inahitaji Kupata Virutubisho vyake Kwa Kadri unavo ishi nayo Ili ziweze kujiimarisha Kwa Kadri zinavo Fanya kazi Yaani kutumika, Maana Kila kazi ya ogani moja Inamchango mkubwa kukamilishia mzunguko wa Afya ya mwili mzima na Ndiyomaana Changamoto ya sehem Moja ya mwili hupelekea Afya ya mwili mzima Kuto kaa sawa..... Kwahivo nimuhimu hasa Kwa wewe ambaye unachangamoto yoyote Kiafya kuhakikisha mazingira unayo utengenezea mwli wako nimazingira sahihi ya kiafya kwaasilimia kubwa Ili kuipunguzia mifumo ya ogani majukumu yasiyo ya lazima Badala yake nguvu kubwa ya Virutubisho itumike kwenye kujiimarisha Kwa Mifumo na kuimarisha Afya ya mwili wako Kwa ujumla.

Dr Sylver Gilbert 0677867293

Kumbuka tu Kwamba mtu  pekee anaye weza kuilinda au kuiangamiza Afya Yako ni wewe mwemyewe,,, Wewe pekee ndiye dereva wa...
25/06/2024

Kumbuka tu Kwamba mtu pekee anaye weza kuilinda au kuiangamiza Afya Yako ni wewe mwemyewe,,, Wewe pekee ndiye dereva wa Mwili wako na Hautaweza kuilinda Afya Yako katikati ya Dunia hii ya leo k**a hauna maarifa nayo.... Tupo kwenye dunia ya kemikali yaani Dunia iliyo jaa vitu vyenye Sumu na takamwili na dunia iliyo Tengenezwa mazingira ya Uvivu na Uzembe wa Hali ya juu kwenye akili ya binadamu.

Kujifunza na Kutafakar mara Kwa mara juu ya afya kutazidi kukufanya uwe macho yaani makini mda wote Kwasabàabu Binadamu hatujakamilika, Tumeumbwa kukosea, kujisahau, kupuuzia, kurizika, kuzarau maranyingi mpaka uwe kwenye tatizo Ndipo utaanza kuumiza akili lakini Yote nikwasababu ya Uvivu na Uzembe wa Kujifunza na Kutafakar

Magonjwa ni hali inayo tokea pale mzani wa upande wa vipaumbele vya magonjwa unapo kuwa juu kuliko vya Afya Na pia Afya ni hali inayo kuwepo pale mzani wa vipaumbele vya Afya Unapo kuwa juu kuliko vya magonjwa....

Unapo kuwa unaishi na mwili wako bila kuupatia vipaumbele vyake vya Afya Yaani Virutubisho basi tambua kwamba mifumo yako ya Ogani inatumika bila kujiimarisha/Kujirutubisho, Hivo nguvu yake kilasiku inapungua na itafika muda itaelemewa na kushindwa Kudhibit Afya yako kwenye kiwango kizuri, Na hapo ndipo utaanza kujiskia kuumwa ugonjwa flani au magonjwa na ugonjwa mmoja mwilini ni mwanzo wa magonjwa mengi Kwasabàabu Kila mfumo unachangia asilimia 100 ya afya ya mwili mzima hivo mfumo mmoja ukiwa kwenye shida basi mifumo Yote ya ogani inaingia hatarini zaidi.

Ili uweze kuidhibiti Afya ya mwili wako ibaki kwenye kiwango kizuri muda wote inabidi uhakikishe kwa siku mwili wako unapata asilimia kubwa ya vipaumbele vya afya yaani Virutubisho /Vijenzimwili kuliko Viburudisho Yaani vitu visivyo na msaada kiafya au Kwa lugha nyingine vipaumbele vya magonjwa

👉🏿Yaani ikiwa ni kwenye mlo wako basi hakikisha mbogamboga na matunda vinachangia shibe yako kwa asilimia kubwa kuliko wanga na vyakula vingine.

👉🏿Ikiwa ni Vinywaji basi hakikisha Maji mwilini mwako yanachukua asilimia kubwa kuliko vinywaji vingine vyote.

👉🏿Lakini pia Hakikisha Kwa Siku mwili unashugulishwa Zaidi au Mazoezi kuliko kuupumzisha kukaa mda mrefu.

👉🏿Lakini pia ikiwa ni tiba basi hakikisha mwili wako unapata Virutubisho Kwa asilimia kubwa kuliko Madawa na vitu vingine.

Kwa kufanya Ivo utakua unachangia asilimia kubwa za kuyaadhoofisha magonjw, Pia kutengeneza mazingira mepesi ya mifumo yako ya Afya kujiboresha zaidi na kufanya kazi vizuri, Kumbuka Mifumo ya Afya ndiyo Mizizi ya Uhai wako..,

Ivi unafahamu kwamba hauwezi kuimarisha Afya yako Kwa kupambana na magonjwa maana  utapoteza muda na gharama tu  Bali  u...
06/06/2024

Ivi unafahamu kwamba hauwezi kuimarisha Afya yako Kwa kupambana na magonjwa maana utapoteza muda na gharama tu Bali unauwezo Wa kupambana na Magonjwa Kwa Kuimarisha Afya,,, Namna pekee Unaweza kuusaidia mwili wako kujiimarisha Kiafya ni kuhakikisha unaupatia mwili vipaumbele vyake Muhimu vya Afya ,yaani Vijenzimwili na siyo Kuupatia vitu vya kwenda kupambana na Ugonjwa.

Kwa akili ya kawaida tu hakuna Changamoto utaishinda kwenye maisha kwa kupambana nayo bali utaishinda Changamoto Kwa kuimarisha makosa makosa uliyo yafanya,, Ukisema uifate Changamoto basi utaishia kupoteza muda na gharama maana Ndiyo kwaanza utazidi kuipalilia izidi kuwa na nguvu Zaidi.

Magonjwa ni Ishara tu au njia ya mwili kuwasiliana na wewe kwa Lengo la kuhitaji vijenzimwili Ili kuimarisha nguvu ya Mifumo ya Afya ambayo Ndiyo mizizi ya uhai.., Nik**a vile mwili Unavo Kuupatia Taarifa za njaa na Kiu......Kwahiyo poteza muda na gharama kwenye Vipaumbele vya Afya na siyo Vipaumbele vya magonjwa.

Dr. Sylver Gilbert 0677867293

Kwa kawaida Ukisha ona Umesumbuliwa na changamoto flani ya kiafya kwa mda mrefu basi inabidi utambue tu kwamba sehem nyi...
27/05/2024

Kwa kawaida Ukisha ona Umesumbuliwa na changamoto flani ya kiafya kwa mda mrefu basi inabidi utambue tu kwamba sehem nyingi za Mwili zimesha athirika kupitia changamoto hiyo na ndiyomaana k**a unataka Afya iweze kuimarika Unatakiwa utumie kitu kitakacho enda Kuimarisha mifumo Yote ya mwili kwa ujumla Vinginevo utajikuta tatizo Moja baada ya lingine yanaibuka..., Hii ndiyo Sababu ya bidhaa k**a C24/CPE kutengenezwa katika kiwango kikubwa Cha Virutubisho lengo ni Kuimarisha mifumo Yote ya mwili kwa kadri inavo Fanya kazi lakini pia Kudhibiti chanzo Cha Ugonjwa na madhara yake yote.

Mfano..., Ukisha ona umesumbuliwa na changamoto ya Sukari Kwa mda mrefu,, Inabidi utambue tu kwamba Presha yako haipo salama, Figo haziwezi kuwa Salama, moyo hauwezi kuwa salama, mapafu hayawezi kuwa salama, Ini haliwezi kuwa salama,Mifupa Haiwezi kuwa salama, ngozi Haiwezi kuwa Salama..,Yaani asilimia kubwa Kila kiungo Cha mwili hakiwezi kuwa salama kwasabàabu ya changamoto ya Sukari tu!.

Kila kiungo Cha mwili kinafanya Kazi ya kuchangia uhai na afya ya mwili mzima Kwa asilimia 💯 Hivo endapo Kuna kingo flani cha mwili hakifanyi kazi vizur basi viungo vyote vya mwili vinakua kwenye changamoto na vinaanza kuathirika taratibu...

Siyo mpaka Viungo Vyote vikuonyeshe Dalili za Kuumwa ndipo ujue vinashida hapana Na ndiyomaana hata kujitokeza rasmini kwa Magonjwa k**a Kisukar au Presha inachukua zaidi ya miaka kumi...., Unapo Ona Ugonjwa umeanza kukuletea misukosuko niishara ya kwamba mifumo ya ogani inayo husika na jukumu lile imesha athirika Kwa Kiasi kikubwa* Na ndiyomaana unaambiwa kuto Kuumwa Haimaanishi kwamba Afya Yako ipo salama Mpaka uhakikishe mwili unapata vipaumbele vyake sahihi Yaani Virutubisho, mazoezi na maji Kwa asilimia kubwa kuliko vitu vingine vyovyote.

By Dr. Sylver Gilbert 0677867293

Maisha yanasura mbili yaani Sura ya Uongo na Sura ya Ukweli...,  Sasa bila kujifunza na kutafakari hasa Karne hii ya kis...
21/05/2024

Maisha yanasura mbili yaani Sura ya Uongo na Sura ya Ukweli..., Sasa bila kujifunza na kutafakari hasa Karne hii ya kisasa ningumu kutambua na kufata njia sahihi na nirahis kutambua na kufata njia za uongo yaani feki kwasababu ndiyo vitu vilivyo tawala uso wa Dunia Kwa Karne hii ya kisasa.

⏩Njia pekee ya kuishi ni Kukua
⏩Njia pekee ya kukua ni kubadilika
⏩Njia pekee ya kubadilika ni kujifunza na kutafari Ili kufahamu ukweli na Kufanya maamuzi sahihi na Kwa wakati Sahihi.

Mungu amekupatia akili K**a ramani ya maisha yoko,,, Lakin kosa kumbwa litakalo yagharimu maisha Yako nikuacha kuiongoza akili yako na kuwaachia walimwengu waiongoze na wakufanyie maamuzi kitu ambacho haina utofauti na dereva kuachia gari lijiongoze lenyewe kitakacho fata ni ajari na madhara....

Duniani tupo tofautitofauti wapo wazuri na wapo wabaya, Yapo mazuri na yapo mabaya, Vipo vizur na vipo Vibaya, na Maranyingi vitu vibaya vinakuja Kwa sura Nzuri kiasi kwamba bila kutuliza Akili na kutafari huwezi kuvitambua na ndiyo Kwaanza Utazidi kuvipatia ukaribu mpaka vikuathiri ndipo unafunguka na inakua tayari umesha chelewa.., Na ndiyo kinacho fanyika Kwa Sasa, Maisha ya kisasa Yaani Feki wengi ndiyo wanayaona original na Maisha Original yanaonekana k**a ni feki yote ni kwasababu ya kuto jifunza na kutafakari na kuufata ukweli ... Nirahis mtu kuona pombe ni Muhimu kuliko maji, Nirahis mtu kuona Dawa za kisasa ni Muhimu wanafya ya Mwilini kuliko Virutubisho, Nirahis mtu kuona Check-up ya Vipimo vya Kieletronic Nisahihi kuliko check-up ya Lifestyle yake,, Yaani kinacho fanyika na uhalisia wa kinacho tegemewa kutokea ni Vitu viwili Tofauti.

Usipuuzie kujifunza kwasababu Ukweli ni kwamba "Maisha hayadanganyi Kila Kinacho tokea kwenye Maisha Yako asililimia zaidi ya 75 wewe ndiyo umeitengezea kiwe kizuri au Kibaya"

Kwa msaada zaidi Wasiliana nami Kwa number 0677867293.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jenga Misingi Ya Afya Bora posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Jenga Misingi Ya Afya Bora:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram