
20/11/2022
Fibroids au uvimbe ndani ya kizazi cha mwanamke, ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha, unaoota na kukua kwenye nyumba ya uzazi (uterus). Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.
CHANZO CHA FIBROIDS:
Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imekuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.
DALILI ZA FIBROIDS:
✔️Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu kwa muda mrefu
✔️Kutokawa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi
✔️Mauvimu ya nyonga (uvimbe kukandamiza kwenye viungo vya nyonga)
✔️ Kupata haja ndogo mara kwa mara
✔️Maumivu ya mgongo
✔️Maumivu wakati wa tendo la ndoa
✔️Maumivu ya kichwa
✔️ Maumivu kwenye miguu
✔️Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)
✔️Uzazi wa shida
✔️ Mimba za shida
✔️Kutopata mimba
✔️Kutoka kwa mimba mara kwa mara
AINA ZA FIBROIDS:
Kuna aina nne za Fibroids
🔴INTRAMURAL: Fibroids aina hii hukua kwenye kuta za uterus. Hii ndiyo aina ya fibroids inayowapata wanawake wengi.
🔴SUBSEROSAL FIBROIDS: Fibroids aina hii hukua nje ya kuta za uterus na huweza kuwa na shina. Subserosal fibroids huweza kukua na kuwa kubwa sana.
🔴 SUBMUCOSAL FIBROIDS: Fibrioids aina hii huota na kukua kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za uterus.
🔴 CERVICAL FIBROIDS: Fibroids aina hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).