19/12/2025
Zipo sababu nyinyi zinazo pelekea mtu kupata kipara katika umri mdogo wa kati na kuendelea.
Mabadiliko Hormone
Urifhi (Genetic
Dawa
Msongo wa Mawazo
Matunzo mabaya ya nywele
Lishe
Umri
Magonjwa ya Kinga
Mazingira
Leo tutazungumzia kwa kifupi jinsi gani homoni inachochea kupata kipara na ndio mara nyingi vinatokana na kurithi.
Jinsia zote hubeba homoni ijulikanayo Testosterone, japo kwa mwanamke hupatikana kwa kiwango kidogo ukilinganisha na Mwanaume , japo kipara imezoeleka kwa wanaume.
Hormone ya Testosterone huchochea uzalishaji wa homone ya Androgen (DHT) kwa msaada wa kimeng'enyo (enzymes) ijulikanayo 5-alpha reductase.
Hii androgen homoni no zao la Testosterone kwa lugha nyepesi.
Kitendo cha mwili kuzalisha hormone hizi za uzazi, lakini wapo baadhi watu miili yao huzalisha kwa wingi Androgen (DTH) hormone.
Watu hawa wenye vinasaba vinavyo chochea uzalishaji mkubwa wa homoni hii ya Androgen ni rahisi kupata kipara katika umri wa mapema.
Homoni hii huchochea mtiririko mbaya wa damu kwenye mizizi ya nywele;
Hufupisha muda wanywele kukua
Hupunguza ukubwa wa vinyweleo
Hivyo nywele zinakuwa nyembamba fupi dhaifu , hatimaye huacha kukua na kipara kujitokeza.