
02/07/2024
JE! NITARAJIE KUJIFUNGUA LINI?🤔
Moja kati ya maswali yanayowasumbua wajawazito wengi ni “je! Nitarajie kujifungua lini?” k**a ww ni mmojawapo unayejiuliza swali k**a hili, usihofu majibu yako yatapatikana hapa.
FAIDA YA KUJUA TAREHE YA KUJIFUNGUA
*Humsaidia mjamzito kujiandaa kimwili na kisaikolojia kwa ajili ya mapokezi ya mtoto, mf; kupanga likizo ya kutoka kazini , kuandaa chumba cha mtoto n.k.
*Humsaidia mjamzito kuandaa vifaa vya kujifungulia mapema.
*Inasaidia kujipanga kifedha ili kujilinda na kumlinda mtoto kutokana na changamoto za uzazi.
*Inasaidia kuwezesha ufuatiliaji mzuri wa ujauzito na kuhakikisha unaenda kliniki kwa wakati unaofaa.
*Inasaidia kupanga safari ya kujifungua k**a utajifungulia kwenye hospitali husika.
JE! WIKI ZA KUJIFUNGUA NI ZIPI?
Mjamzito anatakiwa au anatarajiwa kujifungua kati ya wiki ya 36 hadi 40, ndani ya wiki hizi mtoto huwa salama zaidi. Haitakiwi kupungua au kuzidi wiki, ikiwa wiki zitapitiliza inabidi kumuona daktarin kwa ushauri.
N/B; lakini mara nyingi k**a unahudhuria kliniki k**a inavyotakiwa itajulikana mapema zaidi.
USHAURI / CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA UJAUZITO NA UZAZI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0627292775