
12/11/2021
Habar,Leo tutajifunza kuhusu ugonjwa wa tezi dume.tezi dume ni kiungo ambacho huzunguka mrija wa mkojo(urethra). kiungo hichi hua mwilini mwa mwanaume yeyote Mara baada ya kuzaliwa na huendelea kukua kila siku Ila huongeza Kasi ya ukuaji pale ambapo anakua ametimiza miaka 45 na zaidi ndipo maradhi ya tezi dume hujitokeza
Sababu za tezi dume
1.vyakula,kwa kipindi hiki Hata vijana hukutwa na tezi dume kutokana na vyakula vya kemikal na mafuta wanavyopendelea kutumia
2.kwa wazee, husababishwa na umri kwa sababu tezi dume huongeza Kasi ya ukuaji na kuleta madhara
N.b tezi dume mtu huzaliwa nayo na husaidia katika uzalishaji wa mbegu ya kiume na huzunguka urethra
Dalili za tezi dume
*Maumivu wakati wa kukojoa wakati unaanza Au kumaliza haja
*Kuhisi mkojo haujauisha unapomaliza haha
*Mkojo kuuma Mara kwa Mara
Kinga ya tezi dume
Tezi dume Haina Kinga Ila yakupasa kwenda hospital Mara kwa Mara kuangalia ukubwa na ukuaji wa tezi dume yako