28/01/2026
Nikulinganishe na nani Bwana! upate kuwa sawa naye!? Ni nani wa kupigana na wewe hata akushinde!? Ukisema Neno hakuna wa kukupinga, ukiamuru hakuna wa kubisha, ukibariki hakuna wa kulaani, ukiinua hakuna wa kushusha. Utakatifu ndio vazi lako uweza na nguvu ndio pumzi yako, hakuna wa kulinganishwa wala wa kufananishwa na wewe Mungu uliyeumba Mbingu na Nchi na jeshi lake lote!