23/11/2022
Kuna NGUVU kubwa sana kwenye uwezo wako wa KUSUBIRI. Sio kila kitu kitatokea K**a unavyotaka, kuna vitu kwenye Maisha ni matokeo ya MUDA.
K**a ambavyo KUKU asipoatamia yai lake kwa siku za kutosha, anatoa YAI VIZA ndivyo ilivyo kwenye baadhi ya mambo kwenye maisha. Ukiyalazimisha yatokee kabla ya muda wake, Hata K**a ni mambo sahihi ila hautapata matokeo sahihi.
Utajuaje K**a unachokilazimisha kitokee sio kwa muda sahihi?
Ukiona Ndani yako kinachokusukuma ni kutaka “kuprove” kitu fulani kwa watu, ujue una hatari ya kufanya kitu kwa muda usio sahihi.
Yaani, unapoona bidii yako ya kutaka Jambo fulani litokee sio kwa sababu unaona unalihitaji sana, ila ni kwa sababu UNATAKA KUZIBA WATU MIDOMO au KUWAJIBU KWA VITENDO, hapo Una hatari ya kutoa yai viza.
Dalili nyingine ni pale unapotaka kuonyesha kuwa UMESHINDA. Sio kwamba kitu hicho unataka kitokee kwa sababu UNAKITAMANI na UTAKIFURAHIA bali kwa sababu unataka KUWAONYESHA WATU/MTU kuwa UMESHINDA na HAWAJAKUKWAMISHA.
Kuna wengi ambao wameingia kwenye NAFASI ZA KAZI, wameanzisha BIASHARA au KUINGIA kwenye MAHUSIANO katika hali hizi.
Matokeo yake, HAWAJAFURAHIA KABISA walichokipata kwa sababu ukweli ni kuwa HAWAKUWA WANAKIHITAJI wao bali walitaka KUWAONYESHA WENGINE.
Usisahau kuwa FURAHA yako haitakuja kwa KUWAONYESHA, KUWAJIBU au KUWATHIBITISHIA wengine…Furaha yako iko kwenye kupata kitu ambacho MOYO WAKO unakihitaji.
USIFANYE haraka ukajikuta unatoa YAI VIZA.
Bado MUNGU anakuwazia Mema, HUWA HAWAI wala HACHELEWI.
Tafadhali Ukimaliza Kusoma Share na wengine🙏🏼🙏🏼
See You At The Top
#❤️❤️❤️ #