26/09/2024
Zijue Sababu, Madhara na Tiba ya Kukosa Choo/Choo Kigumu ‘Constipation’
✍🏻Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi sana katika dunia, watu wamekuwa wakiteseka bila kujua nini chanzo cha tatizo hili na vipi kuliondoa tatizo hili na wengine wamekuwa wakilipuuzia bila kujua madhara ambayo wanaweza kuyapata kutokana na tatizo hili.
✍🏻Kukosa choo hutokea pale mtu anakula vizuri lakini unakata siku tatu hadi nne bila kupata choo. Ukiona unakula kutwa mara tatu na unakaa siku mbili hadi tatu huendi chooni au unatoa choo kigumu k**a mbuzi hilo ni tatizo kwako.
✍🏻Tafiti zinaonyesha mtu anaweza kupoteza maisha k**a atakosa choo kwa siku tano hadi saba mfululizo. Watu wengi hulidharau tatizo hili lakini linamadhara makubwa tofauti na wanavyofikiria.
Sababu za Kukosa Choo/Choo Kigumu
👉🏿Kupenda kula sana vyakula vilivyokobolewa k**a vile ugali wa sembe, mikate.
👉🏿Ukosefu wa mbogamboga za majani na matunda ya nyuzi nyuzi/faiba k**a machungwa huongeza tatizo hili. Kila mtu unatakiwa kula matunda aina mbili na mboga za majani aina mbili kila siku.
👉🏿Matumizi makubwa ya pombe na sigara.
👉🏿Unywaji mdogo wa maji, Kila mtu anapaswa kunywa maji kwa kiwango cha chini lita 3 kila siku na usinywe maji wakati unakula, kunywa maji nusu saa kabla au baada ya kula.
👉🏿Matumizi mabaya ya madawa. Mfano dawa za presha, aleji n,k.
👉🏿Kuugua kisukari au ugonjwa wa misuli.
👉🏿Kansa ya utumbo mpana.
👉🏿Msongo wa mawazo: watu wanaopata msongo mkubwa wa mawazo huharibu mpangilio wa homone zao pamoja na kuathiri uzalishaji wa visambaza taarifa kwenye mwili na hivo kusababisha shida kwenye misuli, kupata mcharuko/mpambano ndani ya mwili (inflammation) nakuathiri ufanyaji kazi wa enyzmes ambazo husaidia kumeng’enya chakula.
👉🏿Kutoshughulisha mwili: mazoezi yanasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mfumo wa chakula na kuimarisha misuli na hivo kurahisisha utolewaji wa kinyesi. Utafiti unasema watu wanaotumia mda mwingi wakiwa wamekaa hasa maofsini wanaongoza kwa kuapata matatizo ya kukosa choo kwa mda mrefu.
👉🏿Matumizi ya baadhi ya vidonge: baadhi ya vidonge husababisha kukosa choo kwa muda mrefu na kupata choo kigumu, mfano dawa za kupunguza maumivu, dawa za kuconrtol stress, dawa za kulevya, virutubisho vya calcium na magnesium na antiacids.
👉🏿Ukuaji wa bacteria wabaya kwenye mfumo wa chakula: bacteria wazuri/normal flora waliopo kwenye mfumo wa chakula tunawaita probiotics husaidia kwenye uchakataji wa chakula. Ndio maana kuna umuhimu wa kula vyakula vye kambakamba kwa sababu ni mbolea nzuri kwa bactetia wazuri kukua na kufanya kazi.
👉🏿Matatizo ya tezi ya Thyroid na matatizo mengine ya homoni: matatizo k**a kisukari, kukoma hedhi, maumivu kabla ya hedhi na ufanyaji kazi hafifu wa tezi ya Thyroid huweza kusababisha kupata constipation. Magonjwa mengine ni k**a Pakinson disease, ajali ya uti wa mgongo na matatizo mengine ya neva yanaweza kusababisha Constipation.
Madhara Yatokanayo na Kokosa Choo
➡️Unaweza kuugua saratani ya utumbo mpana.
➡️Unaweza kupata tatizo la tumbo kujaa gesi.
➡️Figo yako inaweza isifanye kazi vizuri.
➡️Unaweza sababisha magonjwa ya moyo.
➡️Unaweza pata tatizo la kukak**aa mishipa ya damu ambapo utasababisha miguu kuwaka moto na ganzi miguuni au mikononi
➡️Unawezasababisha magonjwa ya ini
➡️Unawezapata kisukari
➡️ Upungufu wa nguvu za kiume na kulegea uke baada ya Msuli wa Pelvic kulegea
Tiba Ya Lishe Kwa Tatizo La Constipation
➡️Vyakula vyenye kambakamba/fibers kwa wingi; karanga, nafaka isiyokobolewa, maharage, mboga za majani, na mbegu. Parachichi, broccoli, apple na viazi vitamu
➡️Mbogamboga za kijani: zina madini mengi ya magnesium ambayo husaidia katika ufanyaji kaz mzuri wa misuli na hivo kupunguza tatizo la constipation.
➡️Tumia kinywaji cha uvuguvugu: k**a una tatizo la constipation jaribu kutumia chai ya moto asubuhi, au tumia maji yaliyochanganywa na limau.
Vyakula vya Kuacha Kabisa Kutumia kwa Mgonjwa wa Constipation ni pomoja na:
👉🏿Vyakula vilivyokaushwa kwenye mafuta
👉🏿Pombe
👉🏿Vyakula na vinywaji vilivyopikwa kwenye joto kali sana mfano maziwa yaliyosindikwa
👉🏿Unga uliokobolewa na kusafishwa kupita kiasi
👉🏿Vinjwaji vyenya caffeine kwa wingi k**a kahawa na baadhi ya chai.
✍🏻 Tatizo Hili linatibika kabisa. K**a utalizembea, utakaribisha Ugonjwa wa Bawasiri na utakusumbua. Nipigie / WhatsApp
0684 899 587