Liwaya Herbal Clinic

Liwaya Herbal Clinic Naitwa Dr, Liwaya na wasaidia wahanga wa magonjwa mbalimbali kupona magonjwa kwa kutumia tiba asilia

Liwaya Herbal Clinic: TATIZO LA KUZIDI KWA KIWAGO CHA ACID TUMBONI (ACID REFLUX-GERD)Dr.Liwaya(0687435280)Liwaya herbal ...
24/03/2023

Liwaya Herbal Clinic: TATIZO LA KUZIDI KWA KIWAGO CHA ACID TUMBONI (ACID REFLUX-GERD)

Dr.Liwaya(0687435280)
Liwaya herbal clinic

Gastroesophageal reflux disease (GERD).
-Ni hali inayotokana na kuzid kwa kiwango cha Acid tumboni (Hydrochloric Acid) ambapo hupelekea kupanda kwa acid kutoka tumboni kuelekea katika koo la Chakula (Oesophagus) na kupelekea kudhurika kwa mfumo wa chakula upande wa juu ambao unahusisha koo la chakula na mdomo pia.

Watu wengi sana wanasumbuliwa na tatzo hili bila wao kujua wanasumbuliwa na tatzo hili na hufikia hatua wengine kudhani wamerogwa kutokana na dalili ya tatzo hili. Tutaangalia dalili ambazo mtu anaweza kugundua kuwa anasumbuliwa na tatzo hili.

DALILI ZA MTU ANAYESUMBULIWA NA KUZID KWA ACID TUMBONI (GERD-Acid Reflux
-Zipo dalili nyingi ambazo huashiria mtu kusumbuliwa na tatizo la kuzidi kwa Acid tumboni,dalili hizo ni zifuatazo:⤵️⤵️

1.🖇️ Kuwaka moto kifuani(Kiungulia) hasa wakati wa usiku au unapolala,hali hii hutokea pia mara baada ya kula.
2.🖇️ Mapigo ya moyo kwenda mbio/kushtuka kwa moyo baadhi ya nyakati.Hali hii hupelekea baadhi ya watu kuhisi wana matatizo ya moyo.
3.🖇️ Kuhisi k**a kichwa kimevurugika na kuhusi kuchanganyikiwa.
4.🖇️ Kusahau mara kwa mara hata vitu vya kawaida kabisa/Kupungua kwa kumbukumbu.
5.🖇️ Kujisaidia choo kigumu k**a cha mbuzi.
6.🖇️ Kuwa na wasiwasi na khofu kubwa na hufikia hatua hata ukipigiwa simu hasa nyakati za usiku moyo huanza kwenda mbio na kujawa na wasiwasi mkubwa.
7.🖇️ Kukosa usingizi ama kushtuka mara kwa mara kutoka usingizini.
8.🖇️ Kupumua kwa tabu baadhi ya nyakati.
9.🖇️ Kupata maumivu ya kichwa ya mara kwa mara kwa baadhi ya watu wenye tatizo hili.
10.🖇️ Kupata kikokozi kisichoisha
11.🖇️ Kuvimba Tonsillitis/mafidofido mara kwa mara.
12.🖇️ Mdomo kuwa mchachu na huwez kupelekea kutoa harufu mbaya ya kinywa.
13.🖇️ Kuhisi k**a kuna kitu kimekwama kooni lakin kila unavyojaribu kukitoa hakitoki
14.🖇️ Kupata fangasi mdomoni(mdomo huanza kutoa ute mweupe ambao una harufu mbaya).
15.🖇️ Huweza kupelekea ukaanza kuota ndoto za kutisha pindi ulalapo na kuhisi umerogwa.
16.🖇️ Kupata maumivu ya mgongo hasa sehemu ya mabega,maumivu makali kana kwamba umenyanyua vitu vizito.
17.🖇️ Mwili kuwa na uchovu usioisha utadhani unafanyakaz ngumu kila siku.
18.🖇️ Macho kupunguza uwezo wa kuona vizuri.
19.🖇️ Kupungua uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
20.🖇️ Mwili kupata baridi na wakat mwingine kuhisi homa kabisa.
21.🖇️ Maumivu ya tumbo kati ya kifua na tumbo.
22.🖇️Kichefuchefu na kutapika.

MAMBO YANAYOWEZA KUCHOCHEA TATIZO LA KUZIDI KWA ACID TUMBONI
1.🖇️ Uvutaji wa sigara
2.🖇️ Unywaji wa pombe
3.🖇️ Utumiaji wa vyakula au vinywaji vywenye Caffeine k**a vile Kahawa,Chocolate, Soda nk
4.🖇️ Kula vyakula vyenye mafuta mengi/vyakula vilivyokaangwa
5.🖇️ Kula chakula kingi kupita kiasi ama kula usiku sana.
6.🖇 Kutumia baadhi ya Madawa k**a vile ASPIRIN
7.🖇️ Ngiri ya kifua pia husababisha GERD lakin pia GERD huweza kisababisha Ngiri ya Kifua(Huatal hernia)
8.🖇️ Kuwa Mjamzito
9.🖇️ Uzito kupita kiasi (Obesity)
10.🖇️ Matatzo ya mmeng'enyo wa chakula au kuchewa Kujisaidia pindi uhisipo haja kubwa.

MATIBABU YA TATIZO LA KUZIDI KWA ACID TUMBONI-GERD
-Matibabu ya KUZIDI kwa Acid tumbon yamegawanyika katika aina mbili k**a ifuatavyo:⤵️⤵️

1️⃣ MATIBABU YA KISASA
-Matibabu haya yanahusisha utumiaji ya njia za hospital katika matibabu ikiwemo utumiaji wa PPIs(Proton pump inhibitors),Antacids,Histamine, H-2 Blockers k**a vile Cimetidine (tagament HB),famotidine (Pepcid AC),Nizatidine (Axid AR)
-esomeprazole (Nexium), lansoprazole (Prevacid), omeprazole (Prilosec), pantoprazole (Protonix), rabeprazole (Aciphex) and dexlansoprazole (Dexilant) .Magnesium nk.
Dawa hizi zimekuwa zikitumiwa sana na watu wenye changamoto za Acid nying tumboni na miongoni mwa changamoto ni kwamba dawa hizi zimekuwa zikionesha msaada mdogo sana kwa asilimia kubwa ya wagonjwa na hutoa naafuu ya muda tu.

2️⃣ MATIBABU KWA TIBA ASILI/TIBA MBADALA.
-Njia hii inahusisha matibabu kwa kutumia mimea tiba na imeonekana kuwa na ufanisi mkubwa kutokana na uwezo mkubwa wa mimea mingi katika kupambana na magonjwa mbalimbali kwasababu mimea kutibu kiini cha tatzo kwa kuzifanya kuwa mpya seli za mwili hivyo kuufanya mwili kuwa na uwezo mpya katika kufanyakazi zake.

-Ziko dawa nyingi asilia zenye uwezo mkubwa wa kupambana na matatzo ya ACID nying tumboni,mfano wa dawa hizo ni PEPTICOL POWDER Nk.

Wasiliana nami kwa msaada zaidi wa kitaalamu katika kupambana na tatizo hili na mengine.

LIWAYA HERBAL CLINIC
ILALA-DAR ES SALAAM
PANGANI-STREET
+255687435280
+255755162724

🚭ACHA UVUTAJI SIGARA NI HATARI KWA AFYA
24/03/2023

🚭ACHA UVUTAJI SIGARA NI HATARI KWA AFYA

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA)Nimekuwa nikipokea swa...
24/03/2023

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA)

Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?."

Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?"

Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya s*x lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?"

Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya s*x, wengine wanatumia vidonge vya kizungu k**a Vi**ra, wengine mkongo nk.

Lakini swali linakuja je kuna madhara yoyote?

Jibu ni ndiyo kuna madhara makubwa sana kiafya.

Wanaume wengi ninaozungumza nao wanasema kinachowavuta kutumia dawa hizo ni
- Wanakosa hamu ya tendo la ndoa. Hata mwanamke akiwepo hamu inapotea
- Wanawahi sana kumaliza. Dakika moja,mbili tatu umemaliza.
- Uume unasimama vizuri ila unakuwa legelege
- Wanakosa uwezo wa kurudia bao la pili, la tatu na kuendelea
- Wanakosa nguvu za kiume kwa ujumla

Madhara yenyewe ni haya hapa👇👇

1️⃣ UNAPOTUMIA DAWA HIZO UNATENGENEZA UBONGO NA MWILI WAKO KUWA TEGEMEZI.

Ubongo ndio huongoza mwili na kuratibu shughuli zote za mwili ikiwa ni pamoja na s*x. Kwahiyo ubongo ukizoea kuongoza mwili wako ufanye s*x ukiwa umetumia dawa hizo za kuboost, maana yake ni kwamba miaka yote wewe bila kutumia dawa huwezi.

Pia unakuwa na woga sana, kwamba usipotumia dawa huwezi. Unaanza kujidharau, na kukosa furaha , wengine mashahidi humu kuna wanawake wengine wakikugundua kuwa unatumia hizo dawa kabla ya kufa mapenzi wanakuonesha dharau,matusi hadi kuachana kabisa.

2️⃣ UNAPOTUMIA VIDONGE HIVYO UNAKUSANYA WINGI WA KEMIKALI MWILINI MWAKO AMBAZO KADIRI ZINAVYO RUNDIKANA HULETA MADHARA MAKUBWA KIAFYA.

Zile dawa hutengenezwa kwa kutumia formula za kikemikali,ambazo hupelekea matatizo mengine k**a vile ganzi, na kupooza upande mmoja wa mwili.

Hii husababishwa na zile kemikali au mabaki ya dawa, ambazo husafirishwa kwa damu na kwenda sehem za mikono, miguu na kichwani.

Kwahiyo kupoteza fahamu ,miguu kuuma na kufa ganzi, nk ni moja kati madhara ya kutumia dawa hizo.

3️⃣ UNAUA KABISA UWEZO WAKO WA KUFANYA TENDO LA NDOA. KUNA WAKATI HUTOWEZA HATA KUSIMAMISHA UUME.

Hamu ya tendo la ndoa ni mchakato mrefu, tutajifunza hapa.
Hivyo kwa kutumia dawa hizo unaharibu mwili kabisa na kupoteza uwezo wa kufanya mapenzi bila kutumia dawa,

mwisho hupelekea kukosa nguvu kabisa hata k**a utatumia dawa hutaona uume hauna nguvu wala haupati hamu ya tendo la ndoa.

4️⃣ UNAHARIBU UBORA WA MBEGU AU MANII HIVO HUPELEKEA UGUMBA.

Mbegu za kiume ili zianguliwe zikiwa bora hutegemea kile kinachoingia.

Na dawa hizi hufanya kazi kwenye mfumo mzima wa uzazi yaan korodan, mishipa yote ya uume, na tezi dume ambalo huhusika kutoa ule ute mlainii mweupe kabla ya kufanya mapenzi na wakati wa kutoa mbegu.

Sasa k**a korodan zitaathirika, tezi dume, na mishipa basi mbegu pia hutoka zikiwa hazina ubora , chache, nyepesi k**a maji maji, na hivyo ukipimwa utaambiwa hauna mbegu nzuri za kutungisha mimba. Unakaa ndani ya ndoa miaka mingi mtoto hakuna jiulize.

5️⃣ UNAHARIBU MISULI YA UUME WAKO, HIVYO KUNA WAKATI HATA UTUMIE DAWA MISULI HAITAWEZA KUWA NA NGUVU KABISA

Wakati unafanya mapenzi muda mrefu bila kumwaga kwa kusaidiwa na dawa unaona ni ufahari, lakini ukweli ni kwamba mishipa Ile ya uume Mungu aliiumba iweze kufanya kazi kwa muda sahihi ambao hauna madhara kwenye mishipa.

6️⃣ IKIWA MTUMIAJI ANA MAGONJWA MENGINE HUPELEKEA KIFO. HASA MAGONJWA SUGU K**A MAGONJWA YA MOYO, PRESSURE, SUKARI.

Tendo la ndoa huhusisha mzunguko wa damu. Ikiwa utalazimisha damu izunguke kwa nguvu kuzidi uwezo wa mwili wako maanayake moyo utashindwa kufanya kazi k**a inavyotakiwa.

Mwisho hupelekea mwili hukosa nguvu ghafla, hali ambayo hupelekea kifo cha ghafla.

7️⃣ MATUMIZI YA DAWA HIZO HUPELEKEA MATATIZO YA MACHO NA MASIKIO.

Mzunguko wa damu hupelekea kupekea zile sumu za dawa kufika mpaka kichwani kwenye mishipa ya masikio na macho. Hivyo husababisha kuathiri ubongo na mishipa inayopeleka taarifa sehem zote za kichwa , masikio na macho.hivyo maumivu ni hali ya hatari

8️⃣ MAUMIVU YA KICHWA YA MARA KWA MARA.

Kichwa kuuma kitaalam huashiria mambo mawili, moja ni kichwa kuuma kinatoa taarifa kuwa sehem flan kwenye mwili wako kuna tatizo la kiafya , inawezekana kwenye mfumo wa mzunguko wa damu au moyo au magonjwa mengine nje na magonjwa yatokanayo ma shida za moyo kushindwa kufanya kazi vizuri.

Pili kichwa kuuma ni kwamba kuna magonjwa yanayohusu kichwa chenyewe. K**a nilivoelezea kwenye dondoo #7

Kwahyo unapotumia dawa hizo tegemea kupata hali hiyo.

Ok
Kwahiyo kitaalam haishauriwi kutumia dawa hizo bila kuhusiwa na daktari, ni mpaka utakapopimwa na kupewa maelekezo sahihi ya kutumia, ikiwa ni pamoja na muda gani wa kutumia, na namna sahihi ya kutumia,na nini hupaswi kufanya ikiwa unatumia dawa hizo,

Pia kuna baadhi ya watu ambao hawaruhusiwi kabisa kuzitumia kwa namna yoyote ile.

Kwahiyo, daktari atakwambia utumie ikiwa kuna kuna ulazima kulingana na afya yako kwa ujumla. Pamoja na makatazo mengine atakayokupa ili uwe salama.

Ndani ya group hapa tutajifunza na masomo mengine nimekwisha anza kuwafundisha hapa tangu jana na leo njia rahisi za kutibu tatizo hilo.

kwa wale watakaofuatilia hatua kwa hatua na kuchukua hatua kufanyia kazi watapona kabisa kwasababu mmeona baadhi ya shuhuda za wanaume wachache waliozingatia.

Kutatua changamoto hiyo, tengeneza dawa ninatakazofundisha hapa tumia ukiwa nyumbani kwako.

Pia ikiwa unahitaji dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja ipo, ninauza Ni dawa iliyotengenezwa kwa mimea tiba kwaajili ya kutatua changamoto hiyo moja kwa moja. waweza kuwasiliana nami kunifafanulia tatizo lako kwa kina zaidi

Dr Liwaya
+255687435280
+255755162724

Dar es salaam, Ilala boma Mtaa wa Pangani.

PID,SABABU ZAKE,DALILI ZAKE,KUJIKINGA KWAKE NA MATIBABU YAKE____________________________________________________________...
24/03/2023

PID,SABABU ZAKE,DALILI ZAKE,KUJIKINGA KWAKE NA MATIBABU YAKE

_____________________________________________________________________
PELVIC INFLAMMATORY DISEASE (PID)

-Ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke.Na maambukizi haya kutokea ikiwa bacteria wanaoambukiza kwa njia ya kujamiiana watasambaa kutoka kwenye Uke kwenda kwenye mji wa mimba (Uterus),Mirija ya uzazi na kwenye O***y (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana).

-Maambukizi ya PID mara nyingi husababishwa na Bacteria wanaosababisha Ugonjwa wa Kisonono na Chlamydia.Hivyo wanawake wenye Kisonono wapo hatarini zaid Kupata PID

DALILI ZA MWANAMKE MWENYE PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)
-Zifuatazo ni dalili za mwanamke Mwenye PID:
⏬⏬⏬⏬

▶️ Maumivu ya kawaida ama makali chini ya kitovu.
▶️ Kutokwa Uchafu usio wa kawaida Ukeni ambao ni mzito wenye HARUFU MBAYA wenye rangi ya maziwa ama njano.
▶️ Maumivu makali wakati wa kujamiiana.
▶️ Hupata homa(joto laweza kupanda mpaka 110 F (38.3 °C).
▶️ Maumivu makali wakati wa kukojoa na hupelekea Kupata ugumu wakati wa kukojoa.
▶️ Hupatwa na kichefuchefu.
▶️ Kutapika
▶️ Miwasho sehemu za
siri
▶️ Uchovu
▶️ Uke kuwa mlaini sana
▶️ Kizunguzungu
▶️ Kutokwa na maji maji ukeni kupita kiasi.
▶️ Kuvurugika kwa Hedhi.

ATHARI ZA PID
⚫ Ugumba kwa wanawake
⚫ Kupata Kansa ya shingo ya Uzazi.
⚫ Kutunga mimba nje ya kizazi kutokana na yai kushindwa kufika katika mji wa mimba kutokana na madhara ya PID katika mirija ya Uzazi.
⚫ KUSABABISHA majeraha nje na ndani ya mirija ya uzazi na hii hupelekea kuziba kwa mirija ya Uzazi.
⚫ Maumivu ya tumbo /ngonga mara kwa mara baada ya tendo la ndoa na kipindi cha uchavushwaji mayai (Ovulation).

JINSI YA KUEPUKA/KUJIKINGA NA PID

⚫ Epuka kuvaliana nguo za ndani.
⚫ Kuwa na tabia ya kupima mara kwa mara mfumo wako wa Uzazi.
⚫ Kuwa msafi wa mwili na nguo zako za ndan
⚫ Kula lishe bora.
⚫ Epuka kufanya tendo la ndoa na mwenza wako mara baada ya kugundua ana magonjwa ya kujamiiana (STDs)

Tumia dawa Asili iitwayo UROGETIX 5 kwa matibabu ya haraka na uhakika ya PID.

TIBA NA USHAURI
⏬⏬⏬⏬⏬⏬

Dr.Liwaya
Tiba Asili
Tanzania
PANDEX HERBAL CLINIC

+255687435280
+255755162724
liwayaherbal@gmail.com

MVURUGIKO/KUTOKUWA SAWA MFUMO WA HORMONE KWA WANAWAKE (HORMONAL IMBALANCE)-Tatizo hili hutokea pale ambapo kuna kiasi ki...
24/03/2023

MVURUGIKO/KUTOKUWA SAWA MFUMO WA HORMONE KWA WANAWAKE (HORMONAL IMBALANCE)

-Tatizo hili hutokea pale ambapo kuna kiasi kingi au kidogo zaidi cha hormone kupita kiasi katika mishipa ya damu.Kutokana na umuhimu wa kazi ya hormones katika mwili,mabadiliko kidogo ya hormones hupelekea madhara katika mwili wote.

HORMONES NI NINI?
-Hormones ni Kemikali ambazo huzalishwa na Tezi katika mfumo wa Hormone.Hormones husafirishwa kwa njia ya damu kutoka kwenye Tezi mpaka kwenye viungo mbalimbali vya mwili (tissues & Organs) kwaajili ya kupeleka taarifa ya nini kifanyike kwa wakati husika.

DALILI ZA MABADILIKO YA MFUMO WA HORMONES KWA WANAWAKE

1.🖇️ Kukosa raha kiakili
2.🖇️Kupata Choo kigumu au Kuharisha mara kwa mara.
3.🖇️ Mvurugiko wa mzunguko wa hedhi.
4.🖇️ Maumivu ya tumbo(chini ya kitovu),mgongo na kiuno wakati wa hedhi.
5.🖇️ Kukosa/kupungua hamu ya tendo la ndoa na kupelekea kukosa ladha la tendo la ndoa
6.🖇️Kushindwa kupata ujauzito.
7.🖇️Kukosa usingizi.
8.🖇️ Kupungua uzito au kuongezeka uzito kusikoeleweka.
9.🖇️Kuota nywele mwilini kupita kiasi
10.🖇️Miwasho kwenye Ngozi
12.🖇️ Kuwa mchovu mara kwa mara
13.🖇️ Kuhisi kiu mara kwa mara
14.🖇️ Kukojoa mara kwa mara
15.🖇️ Kuhisi njaa mara kwa mara.
16.🖇️ Kutokwa jasho mara kwa mara.
17.🖇️ Ngozi kuwa kavu.
18.🖇️

SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KUVURUGIKA KWA MFUMO WA HORMONES

1.🖇️Ulaji duni
2.🖇️ Msongo wa mawazo
3.🖇️ Kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi
4.🖇️Kupata uvimbe kwenye Tezi ya Pituitary.
5.🖇️ Kutanuka kwa O***y na kuwa na vivimbe kwenye O***y/mfuko wa mayai (PCOS).
6.🖇️Kunyonyesha (Breastfeeding)
7.🖇️Kutumia njia za kuzuia kuzaa k**a vile vidonge(P2),kuweka vijiti nk.
8.🖇️Kufikia umri wa kukoma kupata ujauzito (Menopause)

Dr Liwaya (0755162724)

Address

Ilala Pangani Street
Dar Es Salaam
12345

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Liwaya Herbal Clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Liwaya Herbal Clinic:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram