11/10/2020
_*TATIZO LA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI (FALLOPIAN TUBES)*_
_Mirija ya uzazi kitaalamu inajulikana k**a Fallopian tubes. Hii ni mirija midogo iliyopo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke ambayo husaidia kupitisha yai lililopevuka hadi kufika kwenye mji wa mimba._
_Mirija hii inapoziba inazuia yai kusafiri baada ya kuachiliwa na mfuko wa mayai pia inazuia mbegu za kiume kulifikia yai.Tatizo hili ni moja kati ya sababu za ugumba kwa wanawake._ _ambapo Asilimia 40 ya wanawake wenye matatizo ya ugumba inasababishwa na tatizo la mirija kuziba._
_Mara nyingi wanawake wenye tatizo hili hua hawaoneshi dalili zozote zile._
_*KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI KUNASABABISHA VIPI UGUMBA?*_
_Kila mwezi yai la mwanamke linapopevuka huachiliwa kutoka kwenye mfuko wa mayai na kusafiri kupitia mirija ya uzazi kuelekea kwenye mji wa mimba._ _Mbegu za kiume pia husafiri kutokea kwenye shingo ya kizazi na kulifata yai kwenye mirija ya uzazi ili kulirutubisha tuelewe kwamba urutubishwaji wa yai unafanyika kwenye mirija ya uzazi wakati yai linasafiri kuelekea kwenye mji wa mimba._
_Mirija inapokuwa imeziba inazauia yai kusafiri kufika kwenye mji wa mimba na inazuia mbegu za kiume kulifikia yai hivyo kusababisha ugumba._
_Mbali na hayo mirija hii inaweza isizibe yote kabisa na kuacha upenyo unaoruhusu mbegu za kiume kupita na kulifikia yai na kupelekea mimba kutunga nje ya kizazi._
_*DALILI ZA MIRIJA YA UZAZI KUZIBA*_
_Sio watu wote wenye tatizo hili huonesha dalili.Asilimia kubwa ya wanawake wenye tatizo hili hawaoneshi dalili zozote._
_Aina ya tatizo hili inayojulikana kitaalamu k**a HYDROSALPINX ndo huwa na dalili za maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kutokwa na maji maji mengi ukeni._
_Hydrosalpinx ni aina ya tatizo la mirija kuziba ambapo mirija inaziba na kujaa maji._
_pia mwanamke huweza kupata dalili k**a maumivu makali wakati wa tendo la ndoa na maumivu makali wakati wa hedhi_
_*VISABABISHI VYA TATIZO LA MIRIJA KUZIBA*_
_Kisababishi kikubwa cha mirija kuziba ni tatizo la maambukizi kwenye viungo vya uzazi (PID)_
_Na mara nyingi PID husababishwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa japo sio kila mwenye PID imetokana na magonjwa ya zinaa._
_Sababu nyingine ni k**a_
_Magonjwa ya zinaa mfano Kisonono na Chylamidia_
_Maambukizi kwenye kizazi baada ya mimba kuharibika (abortions) _
_Historia ya tatizo la kidole tumbo (Appendicitis)_
_Historia ya Mimba kutunga nje ya kizazi_
_upasuaji ambao unahusisha mirija ya uzazi_
_VIPIMO GANI VYA KUONESHA TATIZO HILI?_
_Tatizo hili upimwa kwa kipimo maalumu cha X ray ambacho kinajulikana kitaalamu k**a Hysterosalpingogram (HSG) ambapo unawekewa kimiminika fulani ambacho ni salama kwenye kizazi na kupigwa X ray._
_Kimiminika hicho kikiingia kwenye kizazi kinaenda hadi kwenye mirija kikishndwa kupita kwenye mirija basi inaonesha mirija imeziba.Aina nyingine ya kipimo hiki ni kwa kuwekewa kifaa chenye camera ambacho kinapitishwa ukeni hadi kwenye mirija. Vipimo vingine ni vile vya kupima ute (High vaginal swab) kuangalia k**a kuna maambukizi._
_MATIBABU_
_K**a mirija imeziba kwa makovu madogo madogo basi huzibuliwa kwa vifaa maalumu au upasuaji wa kutoa makovu hayo._
_Endapo mirija imeziba kwa kujaa maji kwa sababu ya maambukizi (hydrosalpinx) basi unahitaji matibabu ya maambukizi hayo kwanza._
_UWEZEKANO WA KUPATA UJAUZITO_
_Mirija ikishazibuliwa unaweza kushika mimba kawaida. k**a una matatizo ya kupevusha mayai daktari anaweza kukuongezea dawa za kusaidia kupevusha mayai._
_Endapo mirija imeziba hata unapotumia dawa za kupevusha mayai haziwezi kukusaidia._
_Mwisho_
_Ni vyema unapofikilia kupata ujauzito ufanye vipimo vinavyosaidia pia kuona mirija yako k**a iko katika hali nzuri.Unapoona dalili zozote ambazo huzielewi kwenye mwili wako basi hakikisha unafika hospitali kwa ajili ya matibabu_