20/10/2025
👉🏽 SABABU (CHANZO) 10 ZA MAUMIVU YA KIUNO, NYONGA AU CHINI YA KITOVU KWA MWANAMKE.
Maumivu haya yanaweza kutokana na matatizo kwenye:
✔ Mfumo wa uzazi
✔ Njia ya mkojo
✔ Mfumo wa chakula
✔ Misuli na mifupa ya nyonga/kiuno
1️⃣ Pelvic Inflammatory Disease (PID) – Maambukizi kwenye mfumo wa uzazi
Huanzia kwenye uke, husambaa kwenye kizazi, mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari. Husababisha maumivu ya muda mrefu, usaha uke, homa na maumivu wakati wa tendo la ndoa.
2️⃣ Fibroids – Vivimbe kwenye mji wa uzazi
Husababisha tumbo kujaa, presha kwenye nyonga, maumivu ya kiuno, hedhi nzito au isiyoisha kwa wakati.
3️⃣ Endometriosis – Tishu za uzazi kuota nje ya eneo lake
Husababisha maumivu makali kabla au wakati wa hedhi, uchovu, maumivu ya tendo la ndoa na tumbo kuchoma upande mmoja.
4️⃣ Dysmenorrhea – Maumivu makali ya hedhi
Maumivu yanayokuja kila mwezi kabla au wakati wa hedhi, yanaweza shuka hadi kiunoni au kwenye mapaja.
5️⃣ Ovarian Cyst – Uvimbe wenye maji kwenye ovari
Huleta maumivu upande mmoja wa tumbo, tumbo kuuma ghafla, kichefuchefu na hata maumivu makali yanayoleta kizunguzungu.
6️⃣ UTI – Maambukizi ya njia ya mkojo
Huleta maumivu ya chini ya tumbo, kiuno, kuchoma wakati wa kukojoa, mkojo kunuka au kuwa na damu.
7️⃣ Maambukizi ya zinaa (Chlamydia, Gonorrhea n.k.)
Husababisha maumivu ya nyonga, ute usio wa kawaida ukeni, maumivu ya tendo la ndoa na PID ikiwa hayajatibiwa.
8️⃣ Adhesions – Vishikizo baada ya upasuaji au maambukizi
Tishu za ndani hushikana na kusababisha maumivu ya nyonga ya muda mrefu, hasa baada ya operation au mimba kuharibika.
9️⃣ Matatizo ya mfumo wa chakula (constipation, gesi kushik**ana, IBS)
Kuchelewa kupata choo, tumbo kujaa gesi, pressure chini ya kitovu na maumivu yanayokuja na kuondoka.
🔟 Matatizo ya misuli na mifupa ya nyonga/kiuno (Musculoskeletal Pain)
Yanayotokana na kukaa muda mrefu, mkao mbaya, misuli ya nyonga kuwa dhaifu, au majeraha ya mgongo/kiuno.
WASILIANA NASI KWA
WHAT'SAPP/PIGA
0769287659