08/02/2022
CHANGAMOTO Ya Tezi Dume
MAWASILIANO; +255743562868
Wanaume wote wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya tezi dume na hasa wanapofikia umri wa miaka 50. Hapa chini tutapitia baadhi ya matatizo yanayowasumbua zaidi wanaume:
Benign Prostatic Hyperplasia (BPH) au Prostate Enlargement
Hii ni hali ambapo tezi dume huongezeka ukubwa. Zaidi ya theluthi ya wanaume wote walio juu ya miaka 50 wana dalili za kuvimba kwa tezi dume. Haijajulikana kwa uhakika ni kwa nini tezi dume huwa kubwa zaidi kadri umri unavyoongezeka, lakini kukua huku si dalili ya kansa na wala hakuongezi uwezekano wa kupata kansa. Hili si tatizo kubwa sana la kiafya.
Tezi dume iliyoongezeka ukubwa huleta msukumo juu ya mrija wa mkojo na kibofu cha mkojo hali ambayo inaweza kuathiri namna mkojo utakavyotoka.
DALILI YA TEZI DUME ILIYOVIMBA.
1.Shida katika kuanza kukojoa au kuubana mkojo
2.Mtiririko dahifu wa mkojo
3.Kukojoa kwa shida
4.Kujisikia kuwa hujamaliza mkojo
5.Mkojo kuendelea kudondoka kwa muda mrefu baada ya kumaliza
6.Hali ya kujisikia kukojoa mara kwa mara au ghafla
7.Kuamka mara nyingi zaidi usiku kwa ajili ya kwenda haja ndogo
Kwa baadhi ya wanaume, dalili zinaweza kuwa ndogo ambazo hazihitaji tiba. Kwa wengine, zinaweza kuwa kubwa na kuathiri maisha yao. Wanaume hupatwa hofu kuwa kuvimba kwa tezi dume kunasabihiana na upataji wa kansa ya tezi dume. Hii siyo kweli kwani uwezekano wa kupata kansa wa mtu mwenye tez i iliyovimba hauzidi ule wa mtu asiye na tatizo hili la tezi.
Sababu ya kuongezeka ukubwa wa tezi dume haijajulikana, lakini wataalamu wengi wanaamini kuwa inahusiana na mabadiliko katika homoni yanayotokea umri wa mtu unapokuwa mkubwa.
Tiba ya Tezi Iliyokua
Tiba ya tezi hutolewa kulingana na hali iliyofikiwa. Utashauriwa kubadili mtindo wako wa maisha, k**a kupunguza utumiaji wa kahawa na pombe, na kufanya mazoezi ya mwili. Pamoja na kubadili mtindo wa maisha,
Madhara yanayoweza kutokea kutokana na benign prostate enlargement ni; maambukizi kwenye njia ya mkojo – UTI, kutokana na kuwa wadudu k**a bakteria waliomo kwenye njia ya mkojo hawataweza kusukumwa nje wakati wa kukojoa, .