24/04/2025
TIBA YA MAUMIVU YA VIUNGO/JOINTS ZA MIGUU,MIKONO, MGONGO,MAGOTI NA KIUNO.
CHANZO CHA MAUMIVU YA MIFUPA NA VIUNGIO/JOINTS
Hii inajumuisha maumivu katika maeneo mbali mbali ya Mwili inaeza kuwa shingo, mgongo, joint za mikono ,joint za miguu ,magoti na Misuli Kuvuta,
WATU GANI WANAKUA KATIKA HATARI HII
1:wenye umri mkubwa
2:wana michezo
3:uzito mkubwa
4:wanaoenda sana gym
5:watoto wenye upungufu wa madini chuma na vitamini
SABABU YA MAUMIVU HAYO
Umri unavyozidi kusogea au kukosa madini flani ya kuimarisha mifupa hupelekea mwili hushindwa kuzalisha ute ute (synovial fluid) katika viungo vya mifupa hivyo kupelekea msuguano wa viungo na kusababisha maumivu makali kushindwa kukaa,kuinuka,kukimbia na kutembea
KWANINI KUTOKEA MAUMIVU
1.kulika kwa cartilage(Gegedu)
2.upungufu wa synovial fluid(ute ute)
3.maambukizi ya vijidudu katika viungo k**a (bacteria,fangasi na virusi
4.uzito kua mkubwa
Hivyo basi kwakua umri umeenda au kufanya mazoezi kwa wingi kuna madini yanakua yanapungu au kukosekana kabisa hasa madini Chuma, Calcium,zinc boron, copper, magnesium, potassium, phosphorus na Vitamin D ambayo haya yanahusika katika utengezwaji na uimarishwaji wa mifupa
Dalili za kawaida za maumivu haya ni:
1.Maumivu makali au ya muda mrefu kwenye viungo au mifupa
2. Uvimbe kwenye viungo
3. Ugumu wa kusonga viungo
4. Uchovu
5. Homa
Nini cha kufanya:
1. Wasiliana na daktari: Daktari atafanya uchunguzi na kukupa utambuzi sahihi na matibabu.
2. Pumzika: Epuka kufanya shughuli zinazosababisha maumivu.
3. Fanya mazoezi mepesi: Mazoezi ya kawaida yanaweza kusaidia kuimarisha misuli na kupunguza maumivu.
4 Tumia joto au baridi: Kutumia joto au baridi kwenye eneo lenye maumivu kunaweza kusaidia kupunguza maumivu.
Ni muhimu kutambua kuwa maumivu ya viungo na mifupa yanaweza kutibiwa, na kwa kufanya mabadiliko madogo kwenye maisha yako, unaweza kuondoa maumivu na kuboresha ubora wa maisha yako.
TIBA NA USHAURI.
Unashauriwa kula vyakula ambavyo vina kiwango kingi Cha madini na Vitamini ili kukusaidia kuimarisha mifupa ,kuzalisha Ute Ute na kuondoa maumivu, unaeza kula parachichi, ndizi, zabibu ,maeple, broccoli, nafaka jamii ya kunde, viazi vitamu , matumizi ya nyanya, nafaka zisizokoborewa,kula mbegu za maboga, Kula Uyoga, Nyama ,maini, samaki ,mayai, kunywa maziwa ama maziwa mtindi "yoghurt", kunywa maji magumu ,kula matunda yenye acid, pia kula mboga za majani kwa wingi ikiwemo Bamia,nyanya chungu, matembele, majani ya maboga,mlenda nk, pia tunazo dawa za virutubisho lishe, ambavyo zimesheheni viini lishe ambavyo vinasaidia kuimarisha mifupa,kuzalisha Ute Ute na Gegedu na kuondoa uchakavu wa mifupa na maumivu.
Mawasiliano +255 628403826