04/02/2026
Huu ni mwaka wa pili wa kampeni mpya ya โUnited by Uniqueโ, inayolenga mbinu ya huduma za saratani inayomweka mtu mbele (people-centred approach). Mbinu hii inalenga kuwaweka watu binafsi, familia, na jamii katika moyo wa mifumo ya afya. Inamaanisha si tu kutibu ugonjwa, bali pia kuzingatia mitazamo na uzoefu wa watu binafsi, walezi, familia na jamii k**a washiriki pamoja na wanufaika wa mifumo ya afya inayoaminika, inayojibu mahitaji na mapendeleo yao kwa njia jumuishi (holistic).
Baada ya mwaka wa kwanza uliolenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa huduma zinazomweka mtu mbele, UICC sasa inaelekeza msisitizo wa mwaka 2026 kwenye uzoefu wa maisha halisi. Watu walioathiriwa na saratani โ wale waliowahi kuugua saratani wenyewe, walezi wao, na wataalamu wa afya โ wako katika nafasi nzuri ya kusaidia kubainisha nini kinakosekana katika mifumo ya huduma, na nini hasa kinafanya kazi kwa vitendo katika mazingira mbalimbali.
๐๏ธ
**********************************************
Tunapatikana Ubungo-Makuburi
mkabara na Barabara ya Mandela-kituo cha daladala Gereji
Mkabara na Barabara ya Majichumvi kituo cha Makuburi uwanjani
**********************************************
wasiliana nasi 0687522222