Afya Herbs

Afya Herbs Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Afya Herbs, Medical and health, Dar es Salaam.

FAHAMU ZAIDI KUHUSU MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA MKOJO (U.T.I)Mfumo wa mkojo huundwa na figo, njia ya mkojo inayotoka kweny...
17/08/2022

FAHAMU ZAIDI KUHUSU MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA MKOJO (U.T.I)

Mfumo wa mkojo huundwa na figo, njia ya mkojo inayotoka kwenye figo hadi kwenye kibofu(yureta),kibofu cha mkojo na njia ya mkojo inayotoka kwenye kibofu hadi nje ya mwili(yurethra).Maambukizi ya bacteria huweza kuathiri sehemu yoyote ya mfumo huu. Maambukizi ya mfumo wa mkojo ni ya pili ukiangalia maambukizi yote ya mwili.

Dalili za maambukizi ya mfumo wa mkojo ni zipi?

Dalili hutofautiana kulingana na ukali wa maambukizi,umri na sehemu iliyoathirika.

Dalili zinazojitokeza mara nyingi pakiwa na maambukizi (UTI):

Uchungu au kuwashwa unapokojoa.
Kuhisi kukojoa mara nyingi.
Homa na uchovu .
Mkojo wenye harufu mbaya na si safi (cloudy).
Dalili zinazotokana na maambukizi ya kibofu

Maumivu katika upande wa chini wa tumbo.
Kukojoa mkojo kidogo , wenye maumivu na mara nyingi.
Dalili za homa kidogo. Bila maumivu ya mbavu.
Damu kwenye mkojo.
Dalili zinazotokana na maambukizi ya upande wa juu wa njia ya mkojo

Maumivu ya upande wa juu wa mgongo na mbavu.
Kuwa na homa na kuhisi kibaridi. Kichefuchefu, kutapika, uchovu na kujihisi mgonjwa kwa ujumla.
Kuchanganyikiwa kwa wazee.
Maambukizi haya ni hatari sana yasipotibiwa vyema na haraka. Aidha yanaweza hata kuhatarisha maisha.

Kuwashwa na kukojoa mara nyingi ni dalili za maambukizi ya sehemu za mfumo wa mkojo.
Chanzo
Nini kinachosababisha maambukizi ya mara kwa mara ya njia ya mkojo?

1. Kuziba kwa njia ya mkojo.

2. Maumbile ya k**e Kwa sababu njia ya yurethra ya wanawake ni fupi kuliko ya wanaume,basi huwezekano wa kupata maambukizi ni mkubwa zaidi kuliko wanaume.

3. Maingiliano/ Kujamiiana: Wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa huweza kupata maambukizi mengi zaidi kuliko wenzao wasioshiriki tendo hilo.

4. Mawe Mawe kwenye figo, njia ya kuelekea kwenye kibofu cha mkojo (ureta) au ndani ya kibofu chenyewe yanaweza kuzuia mtiririko wa mkojo na hivyo kusababisha maambukizi.

5. Mpira wa katheta Watu waliowekewa katheta wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi kirahisi.

6. Kasoro za kimaumbile Watoto wenye kasoro za kimaumbile k**a mkojo kurudi nyuma k**a kwenye kibofu na hivyo kwenda kwenye yureta ( vesicoureteral reflux) au k**a njia ya yurethra valve inafungukia nyuma, hupata maambukizi kwa urahisi sana.

7. Kuongezeka ukubwa wa tezi dume Wanaume walio na umri wa miaka zaidi ya sitini wanaweza kupata maambukizi kwa sababu ya kukua kwa tezi dume.

8. Kinga ya mwili iliyodhoofika Wagonjwa wa kisukari,UKIMWI au saratani.

9. Sababu nyingine: k**a njia za yureta na yurethra kuwa nyembamba,tibi (TB) kwenye njia ya mkojo, neurogenic bladder,diverticulumnk.

Kuziba njia ya mkojo ni sababu kuu ya maambukizi ya njia ya mkojo.
Utambuzi
Je,maambukizi ya mara kwa mara hudhuru figo?

Maambukizi ya mara kwa mara kwa watu wazima hayawezi kudhuru figo . Kitu muhimu cha kuangalia ni hali iliyosababisha maambukizi hayo, k**a mawe, kuziba au njia kuwa nyembamba, tibii ya mfumo wa mkojo havijatibiwa ipasavyo.

kwa upande mwingine,maambukizi kwa watoto yasipotibiwa kwa haraka na kwa njia ifaayo,figo zao changa zinaweza kuharibika kabisa. Madhara haya yanaweza kufanya uwezo wa figo wa kufanya kazi upungue na mtoto kupata shinikizo la damu. Kwa hiyo maambukizi haya ni hatari zaidi kwa watoto kuliko watu wazima.

Kwa vipimo, ushauri na matibabu zaidi ya U.T.I wasiliana na mimi sasahivi
Piga simu/whatsapp 0789717023

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255789717023

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Herbs posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram