07/12/2020
FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO, SABABU ZAKE, TIBA NA DALILI.
Vidonda vya tumbo Ni matokeo ya kuharibika na kulika kwa kuta za mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Kuta ambazo hushambuliwa na vidonda ni
Kuta za tumbo
Kuta za sehemu ya kwanza ya utumbo mwembamba.
Kuta za sehemu ya chini ya koo la chakula.
Kuna sababu kuu mbili ambazo hupelekea mtyu kupata vidonda vya tumbo.
Mambukizi ya bacteria aina ya Helicobacter pylori—bacteria huyu husambaa kwa njia ya maji na chakula, katika mwili wa binadamu. Bacteria huyu hupenda kuishi sana tumboni na kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mwembamba akiwa hapo huzalisha vimeng’enya vitwavyo urease ambavyo hupunguza kiwango cha tindikali tumboni . Kupungua kwa tindikali tumboni kuna sababisha nyongo kuzalisha tindikali nying zaid ya uwezo wa tumbo kuzimudu ambazo hupelekea tumbo kutoboka na kuchubuka.
Kumeng’enywa na kulika kwa kuta za mfumo wa chakula hii husababishwa kwa namna zifuatazo
Matumizi ya dawa za kutuliza maumivu kwa muda mrefu(analgesic) pasipo kumuona dactar au mtaalamu yoyote ule wa afya. Dawa k**a Asprin, ibuprofen, nifenamite, paracetamol na nyinginezo. Matumizi ya dawa hizi huzuia utengenezaji wa ute wa ulinzi wa kuta za tumbo dhidi ya vimeng’enya na tindikali hivyo kulifanya tumbo kuwa na ulinzi dhaifu. Pia dawa hizi hupunguza kiwango cha damu kinachofika tumbon, jambo hili kusababisha tumbo kutengeneza seli hai za tumbo ambazo ndiyo msingi wa ulinzi wa tumbo.
Sababu nyengine zinazoweza kusababisha vidonda vya tumbo ni pamoja na;
Ulevi wa pombe
Msongo wa mawazo
Uvutaji wa sigara
Tiba za miale katika maeneo ya mfumo wa tumbo mfano x ray
Kansa ya tumbo.
Dalili za vidonda vya tumbo
>maumivu ya tumbo toka chini ya tumbo hadi kifuani
>kutapika damu
>kinyesi kinakuwa na rangi nyeusi au cha kijivu
>kukosa hamu ya kula
>kupungua uzito
>kichefu chefu na kutapika
K**a vidonda vya tumbo havitatibiwa kwa wakati vinaweza kusababisha matatizo makubwa ambayo tiba yake itahitaji mangalizo makubwa sana. K**a utaona dalili nilizo elekeza juu hapo ni vyema kumuona dactar.
Jinsi gani unaweza kujikinga na vidonda vya tumbo;
Badili baadhi ya mifumo yako ya maisha k**a
>Acha au punguza matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara
>weka mazingira yako safi kuepuka mambukiz ya bacteria
>usichanganye pombe na aina yoyote ile ya dawa
>usitumie ovyo dawa za kupunguza maumivu bila ushauri wa wataalamu wa afya
>Epuka kukaa na njaa, pata chakula kwa wakati
Kwa ushauri zaidi ni chek kupitia no 0625665898 or 0789107266
NB: afya ni jukumu langu uliza chochote kuhusu afya.