15/04/2026
Unaweza kuishi na ugonjwa wa Figo kwa miaka 10-20 bila kujua hasa katika hatua za awali (hatua ya 1 hadi ya 3), kwa sababu dalili zake mara nyingi hazijitokezi hadi pale uharibifu unapokuwa mkubwa.
Katika hatua za mwanzo, ugonjwa huu hugundulika kwa vipimo vya kawaida vya damu au mkojo, kwani figo huendelea kufanya kazi yake kwa kiwango kinachokaribia kawaida licha ya kuwepo kwa uharibifu wa kiwango cha chini hadi cha kati.
Hali hii inachangia watu wengi kutokujua mpaka
Pale hatua Mbaya zinapofika baada ya kuanza kuona dalili K**a miguu kuvimba, mkojo kupungua, uchovu wa bila sababu n.k
Aidha ni vyema kujenga Tabia ya kufanya uchunguzi wa Mara kwa Mara na muhimu zaidi kuepuka mambo yanayoweza kusababisha ugonjwa wa figo!
Don’t forget to drink a plenty of water health farmers
ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!
🇹🇿