
24/03/2023
ZITAMBUE ISHARA NA DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA).
Mara nyingi watu wenye shinikizo la damu hawana ishara yeyote na huwa inagunduliwa baada ya kufanya uchunguzi wa kiafya au presha kubwa kwa muda mrefu inapokuwa imefanya uharibifu mkubwa ndani ya mwili.
Changamoto ya shinikizo la damu (presha) huambatana na dalili zifuatazo:-
➡️ Maumivu ya kichwa hasa nyakati za asubuhi.
➡️ Kuhisi kizunguzungu
➡️ Mapigo ya moyo kwenda kwa kasi
➡️ Maumivu ya kifua
➡️ Kupoteza hamu ya kula
➡️ Kupumua kwa shida sana
➡️ Kujisikia uchovu usiokwisha
➡️ kutokuona vizuri
➡️ Kukohoa mara kwa mara
➡️ Kuhisi kelele masikioni n.k
SABABU/VYANZO VYA SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA).
➡️ Kuwa na umri mkubwa
➡️ Msongo wa mawazo (stress)
➡️ Matumizi ya chumvi nyingi kwenye chakula
➡️ Ulaji mbovu usiofaaa
➡️ Ulevi uliokithiri
➡️ Kuwa na unene uliopitiliza
➡️ Ujauzito
➡️ Kutumia vyakula vyenye mafuta mengi
➡️ Mkusanyiko wa sumu nyingi mwilini
➡️ Kusinyaa kwa mishipa ya damu
MADHARA YA KUENDELEA KUISHI NA SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA) KWA MUDA MREFU.
➡️ Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure)
➡️ Moyo kutanuka (Cardiomegaly)
➡️ Shambulio la moyo (Heart attack)
➡️ Kiharusi/Kupooza (Stroke)
➡️ Kuharibu figo na figo kushindwa kufanya kazi
➡️ Kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
➡️ Hatimae KIFO.
ZINGATIA HILI
Licha ya uwepo wa dawa mbali mbali za kukabiliana na tatizo hili bado huendelea kuwatesa na kuwaua wengi kila mwaka.
Pamoja na jitihada mbali mbali bado utasikia kila mwaka watu mpaka milioni 8 hufa kutokana na changamoto hii.
Huku watu bilioni moja duniani kote wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu likiwapelekea kupata shambulio la moyo, kupooza na moyo kutanuka (WHO).
MUHIMU
Changamoto ya shinikizo la damu (Presha) Ni hatari k**a mgonjwa atatumia dawa kiholela inaweza kumuathiri zaidi na hata kumsababishia KIFO.
K**a una changamoto hii au una ndugu mwenye changamoto hii wasiliana na mimi sasahivi kwa vipimo sahihi vya shinikizo la damu, ushauri na matibabu sahihi kwa changamoto ya shinikizo la damu(PRESHA).
Dr John Bugota
0789426770
Whatsapp 0789 426 770