Afya yangu

Afya yangu Hii ni page ambayo inatoa elimu juu ya magonjwa mbalimbali ya wanawake,watoto na wanaume kwa ujumla.

Pia Doctor anatoa huduma kwa bei nafuu zaidi Pindi mgonjwa atakapo hitaji matibabu.

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUWAHI KUFIKA KILELENI NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOATunapozungumzia upungufu wa nguvu z...
21/09/2020

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUWAHI KUFIKA KILELENI NA KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA

Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume.
Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani.
Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni KUKOSA MSISIMKO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA KUKOSA KABISA NGUVU, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia k**a pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume, ingawa na wanawake wanakabiliwa na sehemu ndogo ya tatizo hili.

Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni uliowahusisha wanaume wanaofika kliniki au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume umeonesha kuwa, sio wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo wahusika wanaweza kujiponya nayo bila hata kutumia vidonge wala dawa za miti shamba.
Ingawa Matabibu wanataja magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya zinaa, unene wa kupita kiasi, umri mkubwa kuwa ndiyo chanzo cha wanaume kupungukiwa na nguvu za kiume, lakini imebainika kuwa idadi kubwa ya wanaume wanaofika hospitalini kutafuta nguvu za kiume hawana magonjwa hayo
Huu ni ushahidi kuwa wanaokabiliwa na janga hili wamebeba tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kimawazo zaidi kuliko hali halisi.

Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini kuwa, wale wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na kwamba wanaishi kwa kusikia zaidi ya kujitambua.

Katika hali ya kawaida kila mwanadamu ameumbwa kwa njinsi yake na inapotokea kushabihiana basi ni bahati, lakini mara nyingi usawa hupatikana kwa mmoja kujifunza au kusaidiwa kufikia kiwango cha mtu anayemuhitaji kuwa nae katika maisha hasa ya kimapenzi. Jambo hili wataalamu wanasema kuwa miili iko tayari kutii mafunzo na kubadilisha tabia zake kulingana na utashi wa mhusika.
Tatizo kubwa lililopo kwa wapenzi wengi wanaolalamikia upungufu wa nguvu ni kwamba maisha yao wanayachezea kwenye viwanja vya wenzao wanaokutana nao katika vijiwe na sehemu za kazi.

Usikivu wa mazungumzo toka kwa wanaume wengine wenye uwezo wa kwenda mara nne hadi saba katika tendo au wanatumia dakika arobaini kufika kileleni umewafanya wanaume wengi kujihisi tu kuwa wao wanakasoro eti kwa kuwa huishia mara mbili au moja katika kufanya tendo.
Dhana ya kujiona ni mwenye kasoro inapojengeka akilini mwa mwanaume, huchipua hofu na hatimaye kumfanya ashindwe kabisa kusisimka anapofikiria au kukutana na mwanamke. Matokeo ya hangaiko la akili hushusha uwezo wa mwili na kumuongoza mtu kwenye kuwaza ugonjwa kisha kukimbilia hospitali au kwa waganga kutafuta tiba ya ugongwa ambao kimsingi hanao.

Lakini ukweli uko wazi kwamba kukimbilia kutafuta uwezo wa kufanya mapenzi mara sita au saba hakumfanyi mwanaume awe mlinganifu mwenye kusifiwa na wanawake wengi, kwani si wanawake wote wana uwezo wa kufanya mapezi kwa raundi hizo na si wote wanapenda kutumia takika 30 kucheza mpira wa kikubwa, wengine hukinai mapema na huona kero kuwa na wanaume ving’ang’anizi wenye sifa za kuganda wanapopewa.

Kuna vitu vitatu ambavyo mwanaume unahitaji kuvifahamu ili uweze kuwa imara katika tendo la ndoa kabla ya kuanza kufikiria kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume

1. Fahamu sehemu ambayo inaongeza hisia katika mwili wako
Kila mwanadamu amepewa sehemu moja au mbili au zaidi ambapo sehemu hizo k**a zitatumika vizuri basi zitamfanya mwanadamu apate hisia .
Tambua sehemu hiyo au hizo kasha hakikisha uyo mpenzi wako anazifahamu pia. Ni lazima utapata hamu ya kufanya mapenzi pindi mwanamke wako atakapo chezea sehemu hizo.
Pia k**a unatatizo la kushindwa kurudia tendo basi hakikisha baada ya tendo la kwanza uyo mwanamke wako aendelee kuchezea sehemu ambazo zinaongeza hisia kwako, k**a hazifahamu basi mwambie ili azielewe, usimfiche mwanamke wako juu ya sehemu hizo ambazo zinaongeza hisia kwako.
Hakikisha unazitambua sehemu hizo.

2. Mawazo ni kitu kikubwa sana ambacho kinawafanya wanaume wengi washindwe kurudia tendo au wafike kileleni mapema
Mawazo hayo yapo ya aina mbili
i. Mawazo juu ya mambo ya binafsi ya kimaisha
Mawazo yako juu ya maisha yako ni chanzo kikubwa sana cha wewe kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa au kufika kileleni haraka au kushindwa kurudia tendo.jaribu sana kupunguza mawazo wakati unafanya tendo la ndoa au wakati unataka kwenda kufanya tendo la ndoa
ii. Mawazo juu ya mtu unayekutana naye kimwili
Kuna ile tabia ya kupania tendo, unakuta mtu anawaza siku nzima juu ya tendo ambalo anaenda kulifanya. Kwa ufupi tunasema mtu huyu anafanya tendo la ndoa akiwa peke yake na anapokutana na mwenzake anaenda kumalizia tendo , ndio maana anawahi kufika kileleni mapema na mwisho wa siku anashindwa kurudia tendo.
Hupaswi kumfikiria sana mtu unayekwenda kukutana nae kimwili kwani itakujengea mihemko ya karibu na mikali sana kitu ambacho hakifai, chukulia kawaida na usiwe na papala sana juu ya tendo

3. Kujiona kuwa unamapungufu, ukishajiona kuwa wewe huwezi kurudia tendo au huwezi kufikisha dakika 20 bila kufika kileleni na ukakubaliana na hiyo hali basi jua hutoweza kamwe.
Ondoa hizo fikra za kujiona kuwa unamapungufu, hizo ndizo zinazokumaliza.

Jambo la mwisho ni kuzingatia vyakula na mazoezi, kuna vyakula ambavyo ukitumia kwa wingi vinaongeza hamu na nguvu ya kufanya mapenzi pia kuna vyakula ambavyo ukivitumia kwa wingi vinapunguza hamu na kuondoa nguvu ya kufanya mapenzi.
Kitu kingine ni kupenda kuangalia videos za mambo ya kikubwa pia inasababisha kuleta hilo tatizo kwani linakufanya uwe namawazo ya muda wote juu ya tendo hilo na kukufanya ufike kileleni mapema na kushindwa kurudia tendo.

Naomba niishie hapo lakini kipindi kijacho nitaelezea nijinsi gani video za ngono zinasababisha matatizo ya kushindwa kurudia tendo la ndoa mara ya pili au mara ya tatu na kuendelea.
Asante

0683317836 call/sms for service

SABABU ZA KUKOROMA WAKATI WA KULALA Kukoroma ni kupumua kukiambana na kelele wakati umelala kunakotokana na kutingishika...
19/09/2020

SABABU ZA KUKOROMA WAKATI WA KULALA

Kukoroma ni kupumua kukiambana na kelele wakati umelala kunakotokana na kutingishika kwa tishu zilizopo kwenye eneo la juu la njia ya hewa.

Ni tatizo la kawaida ambalo karibu kila mtu limempata wakati fulani katika maisha yake.

Wanaume wanaonekana kuwa na tatizo la kukoroma zaidi ya wanawake.

Kukoroma hakuna madhara, na kuna njia au mazoezi unayoweza kuyafanya nyumbani kwako ili kuondoa tatizo hili la kukoroma.

Aghalabu, kukoroma huweza kuwa ni ishara ya tatizo kubwa la kiafya k**a:
Obstructive sleep apnea (OSA) Kisukari – type 2 diabetes ugonjwa wa moyo au mishipa ya moyo (cardiovascular disease) Unene wa kupindukia Matatizo ya njia za hewa na pua

Ni Nini Kinachosababisha Kukoroma?

Kukoroma kunaweza kusababishwa na vitu vingi, k**a maumbile ya mdomo na matundu ya hewa, unywaji wa pombe, mzio ((allergies), baridi, na uzito(unene) wa mwili.
Wakati umelela na kutoka kwenye usingizi mwepesi na kuingia kwenye usingizi mzito, misuli ya upande wa juu wa mdomo soft palate, ulimi na koo hujilegeza.
Tishu za kwenye koo zinaweza kijilegeza hadi kufikia kuziba sehemu ya njia ya hewa kwa kiwango fulani na kusababisha kutingishika kwa baadhi ya viungo – kutingishika kwa uvula na soft palate.

Njia inapokuwa imezibwa zaidi, hewa husababishwa kupita kwa nguvu zaidi.

Hii husababisha mitingishiko, na kumfanya mtu akorome kwa sauti zaidi.

Hali zifuatazo zinaweza kuathiri njia ya hewa na kusababisha kukoroma:
Muundo (anatomia ya) wa mdomo.
Misuli ya upande wa juu wa mdomo ikiwa chini na minene inaweza kuipunguza njia ya hewa.

Watu wanene wanaweza kuwa na tishu za ziada upande wa nyuma wa koo zao ambazo zinaweza kupunguza njia ya hewa. Na iwapo kimeo (tishu yenye umbo la pembe tatu inayoning’inia kwenye misuli ya juu ya mdomo-“uvula”) kimerefuka, hewa inaweza kuzuiwa kupita na mitingishiko kuongezeka.
Utumiaji wa pombe.
Kukokroma kunaweza kusababishwa na utumiaji wa pombe kupita kiasi kabla ya kulala. Pomba hulegeza misuli ya koo na kupunguza njia ya hewa.
Matatizo kwenye pua.
Kuziba kwa pua kwa muda mrefu au kuwa na ngozi inayotenganisha matundu ya pua iliyopinda vinaweza kuchangia katika ukoromaji. Kukosa usingizi.
Ukosefu wa usingizi kunaweza kusababisha misuli ya koo kulegea zaidi.
Namna ya kulala.
Kulala kwa kutumia mgongo kunasababisha ukorome mara nyingi na kwa sauti kubwa zaidi. Njia ya hewa nyembaba.
Watu wengine wana tishu ya juu ya mdomo iliyo ndefu, au findo (tonsils) kubwa ambavyo vinaweza kupunguza njia ya hewa na kusababisha kukoroma.
Urithi.
Kuzaliwa kwenye familia yenye historia ya kuwa na tatizo la OSA – obstructive sleep apnea.
Obstructive sleep apnea
Sleep apnea husababisha namna ya kukoroma ambapo mtu ataonekana kutopumua katikati ya kukoroma, na huweza kutoa sauti za mtu anayekabwa pumzi au kutweta.
Pamoja na kukoroma kwa sauti, sleep apnea inaweza kuonyesha dalili zifuatazo: kusinzia mchana kukosa usingizi maumivu ya kichwa asubuhi kushindwa kutuliza fikra au kukosa kumbukumbu kukosa hamu ya tendo la ndoa
Yafaa kumwona daktari endapo unapata dalili hizi kwani sleep apnea inaweza kuambatana na magonjwa mengine, k**a ya high blood pressure, hypothyroidism, na acromegaly.

Mambo Ya Kuyafanya Wewe Mwenyewe Ili Uache Kukoroma

1. Jaribu kuacha Pombe.
Pombe hutuliza ubongo. Yafaa kuacha kutumia pombe angalau saa 4 kabla ya kwenda kulala.

2. Kuondoa Vitu Vinavyoziba Pua
Kuna dawa na njia nyingine za kuondoa madhara na uvimbe kwenye pua. Hivi ni pamoja na: matone ya kuweka puani spray za kuiweka pua iwe na unyevu antihistamines chombo cha kudhibiti unyevu wa chumba

3. Badilisha Ulalaji Wako
Ulalaji unaweza kukufanya ukorome zaidi. Kulalia mgongo kunaufanya ulimi uliolegea kuziba njia ya hewa.
Ulalaji mwingine unaoweza kuujaribu ni: kulala kiubavu nyanyua kitanda upande wa kichwani inchi chache tumia “anti-snore pillow” kuboresha ukaaji wa shingo yako
Unaweza kushonea mpira wa tennis au kitu kingine laini nyuma ya nguo unayovaa wakati wa kulala ili kukuzuia usirudi kulalia mgongo.

4. Kupunguza Unene
Mtu mnene anaweza kuwa na tishu za mafuta zinazozunguka na kupunguza njia ya hewa, na hivyo akapata tatizo la kukoroma.
Kupunguza uzito kunaweza kusaidia kupunguza tatizo la kukoroma.

5. Vifaa Maalumu
Kuna vifaa maalumu vilivyotengenezwa ili kuacha njia ya hewa wazi kwa kusogeza ulimi na taya mbele kidogo.

6. Mazoezi Ya Koo
Mazoezi ya koo yanaweza kusaidia kuimarisha misuli ya koo iliyolegea na kuifanya isilegee wakati ukiwa usingizini.
Jaribu kuyafanya mazoezi haya 10 kwa dakika 30 kila siku kwa angalau miezi 3.

1. Toa ulimi wako wote nje ya mdomo kadiri unavyoweza, upeleke upande mmoja kisha mwingine baadaye juu na chini bila bila kuupindisha.

2. Chezesha taya juu na chini k**a unatafuna kitu kwa dakika moja au mbili. Fanya zoezi hili bila kitu mdomoni.

3. Tamka kila vaweli ukirudiarudia angalau mara 20 hadi 30 kabla ya kuingia kitandani kulala.

4. Imba “la,la, la, la” ukipanda juu na kueremka chini kufuata noti, kabla kuimba “fa,fa,fa,fa” na mwisho “ma, ma, ma, ma.”
5. Panua mdomo wako kadiri unavyoweza na uuache wazi kwa sekunde 10.

6. Weka ncha ya ulimi wako kwenye sehemu ya juu ya mdomo kisha sugua ukirudi nyuma mara 20.

7. Tumia kidole cha shahada kusukuma shavu mbali na meno mara 10 kila upande.

8. Funga mdomo wako, unda umbo la mviringo kutumia midomo yako. Shikilia kwa sekunde 30.

9. Ukiwa umeacha mdomo wazi, peleka taya upande wa kulia, shikilia kwa sekunde 30. Fanya vivyo hivyo upande wa pili.

10. Nyanyua sehemu ya juu ya mdomo na kimeo mara 20.
Mazoezi haya yanatakiwa kufanywa bila kukosa ili kuona mafanikio.

7. Kuacha Uvutaji Wa Sigara
Moshi wa sigara huweza kusababisha kuvimba kwa tishu. Njia ya juu ya hewa huwa ni nyembamba, hivyo hata uvimbe kidogo tu huzuia upitaji wa hewa.

8. Fuata Mpango Mzuri Wa Kulala
Jijengee mpango mzuri wa kulala kwa kulala kila siku kwenye kitanda chenye starehe, ndani ya chumba cheusi, kisicho na joto. Kukosa usingizi wa kutosha kunahusishwa na kunenepa ambako kunasababisha kukoroma.
Dondoo nyingine za kupata usingizi mzuri ni: kuwa na utaratibu wa kulala na kuamka muda ule ule, hata siku za wikendi
kutumia vitu vya kufunika macho au mapazia mazito kuondoa mwanga
kuacha matumizi ya luninga au simu za kiganjani muda mfupi kabla ya kulala, na kuviweka vitu hivi vyote nje ya chumba cha kulala.

ASANTE NA ENDELEA KUJIFUNZA

call/sms : 0683317836
kwa ushauri na kupata huduma
napatikana kimara, dar es salaam
karibu sana

MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA KWA MWANAMKENi kawaida kwa wanawake kuhisi   maumivu wakati wa kujamiiana. Katika matuki...
19/09/2020

MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA KWA MWANAMKE

Ni kawaida kwa wanawake kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana.
Katika matukio mengi hali k**a hizo, hutokana na mwanamke kutolainika sawasawa, hali hii inaweza kutatuliwa kwa urahisi kwa kuongeza muda wa kumchezea mwanamke(foreplay) au kutumia vilainishi vya ziada.
Hata hivyo, iwapo maumivu hayakuweza kupungua, hizi hapa ni baadhi ya sababu, ambazo husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa:

Kukak**aa kwa misuli ya uke (Vaginismus): hali hii inasababishwa na mkazo katika misuli ya uke inayotakana na hofu ya maumivu au majeraha.

Matatizo ya shingo ya kizazi: Wakati mwingine uume unaweza kuingia ndani zaidi hivyo kugusa shingo ya kizazi. Iwapo mwanamke ana maambukizi huisi maumivu mara shingo ya kizazi inapogusana na uume.

Matatizo katika mfuko wa uzazi: Matatizo k**a fibroids yanaweza pia kuwa sababu ya maumivu wakati wa ngono.

Maambukizi ya uke: aina yoyote ya maambukizi ya uke k**a vile maambukizi ya fangasi inaweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana.

Kuumia uke: majeraha kutokana na sababu kadhaa mfano kuchanika wakati wa kujifungua au kuongeza njia katika msamba wakati wa kujifungua.

Endometriosis: Hii ni hali ambayo inasababisha tishu za mji wa mimba kukua nje ya mfuko wa uzazi, na hivyo kuchochea maumivu wakati wa kukutana kimwili.

Maambukizi kwenye funga nyonga(PID): Viungo kwenye nyonga vinaweza kupata maambukizi hivyo kusababisha maumivu wakati wa ngono.

Matatizo ya ovari: Matatizo haya ni pamoja na uvimbe kwenye mfuko wa mayai (ovarian cyst)

Wanakuwa waliokoma siku(Menapause): Wakati wanapokuwa wamekoma siku zao maumbile yao yanasinyaa na kuwa kavu, hivyo kuchochea maumivu wakati wa tendo la ndoa

Magonjwa ya zinaa: magonjwa ya zinaa k**a malengelenge (herpes), masundosundo n.k, yanaweza kusababisha maumivu wakati wa ngono.

ASANTE NA ENDELEA KUJIFUNZA

call/sms : 0683317836
kwa ushauri na kupata huduma
napatikana kimara, dar es salaam
karibu sana

TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOANdugu zangu leo napenda tulijadili tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo ...
19/09/2020

TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA

Ndugu zangu leo napenda tulijadili tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Tutajadili sababu zinasababisha mwanamme kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, madhara yanayotokana na hali hiyo na kisha kuona ni nini cha kufanya ili kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Bahati nzuri ni kwamba kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa.
Watu wengine wanamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadri umri wa mwanamme unavyoongezeka.
Wakati ni kweli kwamba hilo huwatokea wengi, SIYO LAZIMA kwamba hamu ya kufanya mapenzi ipungue umri unapoongezeka.
Kuna idadi kubwa tu ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa.
Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili.

Ukubwa Wa Tatizo La Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

Wanaume wengi hawapenzi kulizungumzia tatizo hili waziwazi na hata wanawake pia.
Pamoja na kwamba tatizo hili halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake, inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili, kwa lugha nyepesi kuna mwanamme mmoja mwenye tatizo hili baina ya kila wanaume sita au saba.
Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume. Tatizo hili huwakera zaidi wanaume kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia urijali k**a sehemu ya ukamilifu wa mwanamme na hunyongea wanapoona wana mapungufu kuhusu mambo ya mapenzi, tofauti kabisa na wanawake.
Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake.
Hata hivyo tatizo la mwanamme kukosa hamu ya kufanya mapenzi limebainika kuwa ndilo linaloongoza katika kuleta migogoro ya unyumba kuliko matatizo mengine yote.
Utajuaje K**a Una Tatizo La Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa?

Tatizo hili halitokei ghafla k**a vile umelala halafu ghafla asubuhi unaamka una mafua, la hasha.
Ni kitu kinachotekea pole pole na pengine mwenyewe usijigundue.
Sanasana pima mwenendo wako wa masuala ya mapenzi kwa mwaka uliopita au miezi kadhaa iliyopita.
Vile vile kutofanya tendo la ndoa kwa kipindi fulani haimaanishi kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi, pengine una hamu thabiti lakini mazingira hayakukuruhusu.
Lakini iwapo hakuna kikwazo chochote na upo na mwenzi wako halafu inapita wiki bila kufanya tendo la ndoa au unalifanya tendo hilo mara moja au mbili tu kwa mwezi, inabidi uanze kujiuliza maswali.
Lakini ieleweke pia kuwa kuhesabu umefanya tendo la ndoa mara ngapi katika kipindi fulani si kipimo pekee cha tatizo hili.
Mawazo yako kwa ujumla kuhusu tendo hili ni muhimu pia jinsi unavyolichukulia na kuliwazia tendo hili kabla, wakati wa tendo na baada ya kumaliza tendo ni muhimu katika kujipima.
Viashiria vingine vyaweza kuwa: kumtomasa mkeo mkiwa ndani tu – chumbani na si penginepo.
Iwapo tendo hili unalifanya pale tu mwezi wako anapokuanza na huwa unalifanya k**a mazoea bila kuwa na mawazo ya kushiriki kikamilifu.
K**a humwazii mpenzi wako anapokuwa hayupo kwamba angekuwapo ungeweza kufanya naye tendo la ndoa.
Vitu hivi k**a vinakutokea basi kuna dalili za kuwa unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na kwamba inabidi utafute suluhisho.
Sababu Za Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamme linaweza kusababishwa na vitu vingi sana.
ababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili.
Hebu tuone baadhi ya vyanzo vya tatizo hili.
Mahusiano Baina Ya Mwanamme Na Mwanamke
Matatizo ya mahusiano kati ya mwanamme na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya mapenzi.
Jee, unapata raha na una amani katika mahusiano yako na mpenzi wako?
Huna wasiwasi wo wote na mahusiano yenu kwamba labda mkeo ana mahusiano na mwanamme mwingine? Haya ni maswali ya msingi ya kujiuliza.
K**a mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.
K**a kuna mambo yanasababisha tendo la ndoa lisifanyike kwa urahisi, ufanisi na kufurahia, hamu ya kufanya tendo hilo inaweza kupungua.
Kwa mfano, k**a mwanamme unawahi kufika kileleni au una matatizo ya jongoo wako kupanda mtungi, tendo zima la ndoa halitakuwa la kukufurahisha sana hivyo unaweza kupoteza hamu ya kulifanya.
Hebu fikiria tunda linalokufurahisha sana ukilila, ukilikosa kwa siku kadhaa, utalikumbuka na kulitafuta lakini ambalo halikufurahishi sana ukilila hutalikumbuka na kulitafuta.
Mawazo Mengi Na Uchovu
Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vyaweza kuchangia.
K**a unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au k**a unachoka sana kazini unaweza pia kukosa hamu ya kufanya mapenzi urudipo nyumbani.
Kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa.
Mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.
Msongo Wa Mawazo
Msongo wa mawazo (depression) unatofautiana na kukosa raha au kujisikia si mtu wa thamani kwa kipindi kifupi.
Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha kutokana na kujisikia si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo zamani.
Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na matamanio yako ya kimapenzi.
Matumizi Ya Madawa Na Pombe
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na:
– madawa ya high blood pressure
– madawa ya kuondoa msongo wa mawazo
– madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine, finasteride na cyproterone
– na mengineyo
Umri Kuwa Mkubwa
Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa testosterone.
Kwa mwanamme homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari.
Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Kiwango cha testosterone katika mwili wa mwanamme hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanamme anvyozidi kuwa na umri mkubwa.
Kiwango cha testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanamme huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.
Matatizo Katika Mfumo Wa Homoni
Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili. K**a thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo.
Tatizo hili linaweza kutokea pale homoni zinapozalisha kitu kinachoitwa prolactin kwa kiwango kikubwa mno na kukisambaza ndani ya mfumo wa damu. Hali hii kiutaalamu huitwa hyperprolactinaemia.
Matatizo Ya Kiafya
Matatizo ya kiafya ya muda mrefu husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Matatizo ya moyo ya muda mrefu, kuwa na kisukari kwa muda mrefu, kansa ya muda mrefu na hali ya kuwa na unene wa kuzidi kiwango ni baadhi tu ya matatizo yanayochangia tatizo hili.
Tiba Za Tatizo La Kukosa Hamu Ya Kufanya Mapenzi Kwa Mwanamme

Sasa tutazame mambo ambayo unaweza kuyafanya kuongeza na kudumisha hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Tatizo hili halijapatiwa dawa za kwenye mahospitali isipokuwa pale unapogundulika kuwa una kiwango kidogo cha testosterone ambapo utaandikiwa namna ya kukiongeza kiwango chako.
Fanya yafuatayo kuongeza hamu yako ya kufanya mapenzi.
1. Tafuta mchezo ambao unaweza kushiriki au fanya mazoezi k**a vile ya kutembea au kukimbia. Kila siku ufanyapo mazoezi yako jaribu kila siku kufikia kiwango cha juu zaidi ya kile ulokwisha kifikia.
2. Inasaidia kufahamu kuwa ni asilimia 40 hadi 50 ya matendo ya ndoa mnayoyafanya yatawaridhisha wote wawili. Kukosa kumridhisha mwenzio iwe changamoto ya kukufanya ufanye utafiti na utundu wa kuboresha tendo mtakapokutana tena.
3. K**a nilivyodokeza hapo juu, jaribuni kwa pamoja kujadili jinsi ya kuboresha namna yenu ya kushiriki katika tendo la ndoa kila mmoja akieleza kile ambacho angependa afanyiwe.
Inasaidia kusoma maandishi kutoka sehemu mbalimbali na kutazama mikanda mbalimbali.
4. Kufanya tendo kwa kush*tukiza inapendeza wakati fulani.
Lakini hili kidogo linaweza kuwa si zuri ukizingatia majukumu ya kila siku ya maisha ya sasa, si rahisi kupata muda wa kutosha wa kustarehe na mpenzi wako.
Kuwa na mpango na ratiba ni bora zaidi na inasaidia kuleta hamu mtu anapokisubiri kitu kilichopangwa siku fulani na muda fulani – fikiria unaposubiri mechi kubwa ya timu yako. Mletee zawadi mpenzi wako, weka muziki mororo uliokuwa unaupenda siku zile, zimisha simu na hakikisha kuna mazingira ya utulivu na ukimya.
5. Hamu huongezeka inapoona kitu kipya. Ukienda na mwenzi wako kwenye sherehe nje ya nyumba yenu, utapata fursa ya kumwona mkeo kwa namna nyingine. Utaweza kuuona uzuri wake na yeye pia atakuona wewe kwa namna nyingine. Wote mtakumbuka vitu ambavyo kila mmoja wenu vilimvutia kwa mwenziwe.
6. K**a umejaribu haya yote na hukupata matokeo mazuri, jaribu kutumia chakula kinachosidia kuongeza hamu .
7. Kuna kampuni zinazosambaza virutubishi mbalimbali vya mwili. Virutubishi hivi ukivitumia vinafanya kazi mara moja na kuponya kabisa tatizo hili. K**a umeshindwa kupata kampuni bora ya kukupatia virutubisho hivi, wasiliana nami muda wowote.

ASANTE NA ENDELEA KUJIFUNZA

call/sms : 0683317836
kwa ushauri na kupata huduma
napatikana kimara, dar es salaam
karibu sana

Wanawake wengi hupatwa na hali ya tumbo kuuma k**a vichomi fulani kabla,baada au wakati wanapokuwa katika mzunguko wa he...
19/09/2020

Wanawake wengi hupatwa na hali ya tumbo kuuma k**a vichomi fulani kabla,baada au wakati wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi.

Hali ya tumbo kuuma wakati wa hedhi huitwa dysmenorrhea.

tumbo kuuma ni jambo la kawaida kwasababu mishipa ya damu ambayo iliandaliwa kubeba mimba inapasuka kwa kuwa mimba haijatungika.

Zipo aina mbili za hali hii.

Aina ya kwanza ni maumivu yanayoanza tangu umri wa kuvunja ungo.

Katika aina hii huwa hakuna ugonjwa unaosababisha uwepo wa haya maumivu.

tumbo kuuma katika aina hii ni jambo la kawaida kwasababu mishipa ya damu ambayo iliandaliwa kubeba mimba inapasuka kwa kuwa mimba haijatungika.

Hali hii hupona hata bila matibabu baada ya mizunguko kadhaa ya hedhi au baada ya kujifungua.
Aina hii inaitwa primary dysmenorrhea (tuiite maumivu ya awali).

Aina ya pili mara nyingi hutokea miaka kadhaa baada ya kuvunja ungo.

Aina hii husababishwa na ugonjwa wa viungo vya uzazi.

Iwapo ugonjwa huo utatokea kabla msichana hajavunja ungo basi maumivu yanaweza kuanza kuanzia umri wa kuvunja ungo.

Maumivu yaliyosababishwa na uwepo wa ugonjwa hayaponi bila kuutibia ugonjwa ulioyasababisha.

Je, Unaweza Kuyahisi Vipi Maumivu?

Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi mara nyingi husikika maeneo ya tumbo la chini na mgongoni.

Unaweza ukahisi maumivu pia kwenye maeneo ya nyonga na mapajani.

Hali ya maumivu haya inaweza kuambatana na kichefuchefu na maumivu ya kichwa pia.

Pia unaweza ukahisi tumbo kujaa gesi, kukosa choo au kuharisha.

Maumivu yanaweza kuwa makali na yakaendelea kwa muda mrefu kuliko maumivu ya kawaida yanayojitokeza wakati wa hedhi.

Je, Nini Husababisha Maumivu Haya?

Wakati mwingine maumivu wakati wa hedhi huwa sio makali sana.

Lakini k**a una maumivu yasiyo koma yanayodumu muda mrefu kuliko mzunguko wako wa hedhi, basi inaweza ikawa ishara au dalili kwamba una tatizo mwilini mwako.

Hapa nitapenda nielezee visababishi mbalimbali vya maumivu makali au maumivu yasiyo ya kawaida yanayompata mwanamke wakati akiwa katika kipindi cha hedhi:

1. Ngozi Ya Ndani Ya Tumbo La Uzazi(Endometriosis)

Endometriosis ni ugonjwa ambao hujitokeza wakati ngozi ya juu ya tumbo la uzazi inapovimba .

Hali hii inaweza kusababisha maumivu kabla, au baada ya kipindi cha hedhi.

Maumivu haya yanaweza kuambatana na uvimbe au maumivu ya nyonga.

Maumivu yanaweza yakawa makali, na yanaweza kujitokeza pia wakati unapofanya tendo la ndoa au baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa au wakati unapojisaidia haja kubwa au haja ndogo.

Maumivu haya endelevu unaweza kuyahisi maeneo ya tumbo la chini au mgongoni.

Dalili za ugonjwa wa Endometriosis huwa k**a ifuatavyo:

• Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa
• Maumivu wakati unapojisaidia haja kubwa au ndogo
• Kushindwa kubeba ujauzito(ugumba)
• Kuhisi uchovu
• Kuhara au kukosa choo
• Tumbo kujaa gesi
• Kichefuchefu
• Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja
• Maumivu ya tumbo kabla, au wakati wa hedhi au baada ya hedhi ambayo yanaweza kuambata na maumivu ya tumbo la chini au mgongoni.

2. Uvimbe Katika Mlango Wa Kizazi(Adenomyosis)

Adenomyosis ni uvimbe usababishwao na kuota kwa tishu zisizo za kawaida katika mlango wa uzazi.
Dalili zake huwa k**a ifuatavyo:
• Kutokwa na damu muda mrefu wakati wa hedhi
• Kuhisi maumivu makali ya nyonga wakati wa hedhi
• Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa
• Damu kuganda wakati wa hedhi
• Kuhisi kitu kigumu maeneo ya tumbo la chini

3. Uvimbe Kwenye Tumbo La Uzazi(Uterine Fibroid)

Uvimbe kwenye kizazi huwa sio saratani bali huwa ni vivimbe vinavyoota kwenye tumbo la uzazi. Wanawake wenye uvimbe mara nyingi huwa hawaonyeshi dalili zozote zile mpaka pale uvimbe unapokuwa mkubwa.

Dalili za uvimbe kwenye tumbo la uzazi huja kutokana na maeneo ulipo, ukubwa wake na idadi ya vivimbe. Dalili zinapojitokeza huwa k**a ifuatavyo:

• Maumivu makali ya tumbo
• Vipindi vya hedhi kubadirika badirika
• Kutokwa na damu nyingi ya hedhi kwa muda mrefu
• Kukojoa mara kwa mara
• Maumivu sehemu za nyonga
• Kukosa choo
• Kutopata ujauzito(ugumba)
• Kichwa kuuma au miguu kuuma

Matibabu
Zipo njia nyingi za kutibia maumivu ya hedhi.
Mojawapo ni kuweka chupa au mfuko wenye maji ya moto kwenye sehemu ya chini ya tumbo (isiwe moto mkali wa kuunguza ngozi).

Dawa za kutuliza maumivu k**a ibuprofen, mefenamic acid, naproxen.

Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango pia husaidia kupunguza maumivu ya hedhi. K**a ilivyo kwa dawa nyingine, ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam kabla ya kuanza kutumia dawa hizi.

Iwapo njia hizi hazifanikiwi kutuliza maumivu ya hedhi, vipimo zaidi vinahitajika ili kugundua chanzo cha maumivu hayo.
Miongoni mwa vipimo vinavyohitajika ni vipimo vya magonjwa ya infection ya njia ya uzazi pamoja na upasuaji ili kuona uwepo wa endometriosis na kuiondoa (picha zinaonyesha jinsi upasuaji huo unavyofanyika kwa matundu madogo na kamera bila kafungua tumbo).

Iwapo maumivu ni makali sana na hayatibiki kwa dawa, mgonjwa asiyekuwa na mpango wa kupata mtoto hushauriwa kuondoa kifuko cha uzazi.

asante na endelea kujifunza.

call/sms : 0683317836 kwa ushauri na msaada

SABABU YA KUWA NA HEDHI NDEFU(menorrhagia.)Mwanamke akianza hedhi, kwa kawaidia humaliza katika siku tatu hadi tano. Hed...
18/09/2020

SABABU YA KUWA NA HEDHI NDEFU(menorrhagia.)

Mwanamke akianza hedhi, kwa kawaidia humaliza katika siku tatu hadi tano.
Hedhi inayochukua zaidi ya siku saba tunasema ni hedhi ndefu.
Kitaalamu, hedhi inayozidi siku saba huitwa menorrhagia.

Asilimia tano ya wanawake wana menorrhagia.
Katika ukurasa huu, tutalijadili tatizo la kutoka damu siku nyingi au kwa lugha nyingine, tatizo la kuwa na period ndefu.

Hedhi ndefu ni dalili ya tatizo la kiafya, k**a matatizo ya:
mabadiliko ya mpangilio wa homoni matatizo ya nyumba ya kizazi Saratani

Hedhi ndefu huweza kusababisha kukosa raha wakati wa hedhi au hata kuvuruga shughuli za kawaida.

Hedhi ndefu yaweza pia kuvuruga usingizi wako.
Hedhi ndefu huweza kusababisha upungufu wa madini ya chuma, na hasa hedhi hizo zikiwa nzito.

Nini Kinasababisha Kuwa Na Hedhi Ndefu?

Hedhi ndefu ni matokeo ya hali nyingi zinazotokana na afya yako, umri wako na staili yako ya maisha.
Baadhi zikiwa:

Mabadiliko Ya Homoni Na Utolewaji Wa Yai

K**a homoni zako haziko kwenye viwango vizuri au k**a mwili wako hauachii yai katika mzunguko wako wa hedhi, ngozi laini (uterine lining) inayotanda juu ya nyumba ya uzazi huwa nene sana.
Mwili wako baadaye unapoondoa utando huu, unaweza ukaona unapata siku nyingi zaidi za hedhi.

Madawa

Unaweza ukaingia period kwa siku nyingi kwa sababu ya dawa unazozitumia. Dawa hizi ni pamoja na:
dawa za kuzuia mimba aspirin na blood thinners Anti-inflammatories.

Ujauzito

Kutoka damu kwa muda mrefu kunaweza pia kuwa ni ishara ya matatizo ya mimba, k**a mimba iliyotungwa nje ya kizazi (ectopic pregancy) au kuharibika kwa mimba (miscarriage).

Unaweza kuwa na hedhi ndefu kwa sababu ya tatizo la placenta previa, placenta ya mtoto kuziba kwa kiasi fulani au kuziba kabisa cervix.
Placenta previa inaweza kusababisha kutoka damu kwa wingi wakati wa ujauzito au wakati wa kuzaa.
Ukiwa na placenta previa unaweza kutoka damu mfululizo kipindi chote cha ujauzito.

Uvimbe (fibroids) au Polyps

Uvimbe kwenye kizazi (fibroid na polyps) huweza kusababisha hedhi ndefu, na wakati mwingine kutoka damu kwa wingi.

Fibroids ni kujenga kwa tishu za misuli kwenye kuta za nyumba ya uzazi (uterus).

Polyps ni matokeo ya kujenga kusiko kwa kawaida kwa tishu ndani ya nyumba ya uzazi na kusababisha uvimbe mdogo.

Kwa kawaida, fibroids na polyps si uvimbe wa saratani.

Adenomyosis

Adenomyosis ni aina nyingine ya kujijenga kwa tishu.
Hali hii hutokea pale endemetrium, au ngozi laini ya juu ya nyumba ya uzazi, inapoungana na misuli ya uterus.
Hii huweza kusababisha kupata hedhi ya muda mrefu.

Tezi ya Thyroid

Unaweza kupata hedhi kwa muda mrefu k**a tezi yako ya thyroid inatenda kazi chini ya kiwango chake.
Hali hii huitwa hypothyroidism.

Kutokwa damu

Unaweza kuwa na hali ambayo imeathiri uwezo wa mwili wako kuifanya damu yako igande, na kukusababishia hedhi ndefu.
Mbili katika hali hizi ni hemophilia na von Willebrand’s disease.

Unene

Unene uliozidi unaweza kukusababisha kuingia period kwa muda mrefu.
Hapa ni kwa sababu tishu za mafuta zinaweza kusababisha mwili kutengeneza estrogen nyingi zaidi. Estrogen hii ya ziada inaweza kukuletea mabadiliko ya hedhi yako.

Ugonjwa wa PID

Pelvic inflammatory disease (PID) hutokea pale bakteria wanaposhambulia viungo vyako vya uzazi. Pamoja na kubadlisha mzunguko wako wa hedhi, PID inaweza kusababisha kutoka uchafu usio wa kawaida pamoja na dalili nyingine.

Saratani

Kutoka damu kwa muda mrefu wakati wa hedhi inaweza kuwa ni ishara ya saratani katika nyumba ya uzazi au shingo ya kizazi. Kwa baadhi ya wanawake, hii inaweza kuwa ndiyo dalili ya kwanza ya saratani hizi.

endelea kujifunza jinsi ya kufupisha siku zako za hedhi

0683317836 call/sms kwa ushauri

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya yangu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya yangu:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram