Afya Kwanza.

Afya Kwanza. Elimu kwa Umma na Ushauri juu ya masuala ya Kiafya na Urembo.!

KWANINI NI MUHIMU KUZINGATIA KUNDI LA DAMU WAKATI WA UCHUMBA? Ungana nami kujua zaidKuna vitu vingi vya kuzingatia unapo...
12/06/2022

KWANINI NI MUHIMU KUZINGATIA KUNDI LA DAMU WAKATI WA UCHUMBA? Ungana nami kujua zaid

Kuna vitu vingi vya kuzingatia unapomchagua mtu kuwa mwenza wa maisha yako. Jambo mojawapo la kuangalia ni kundi la damu.

Sio kitu kinachozingatiwa na watu wengi wakati wa uchumba lakini fahamu kuwa utofauti wa makundi ya damu unaweza kusababisha matatizo kwenye ndoa. Matatizo hayo yanaweza kutokea wakati wa ujauzito na kumuweka mtoto ambaye hajazaliwa katika hatari.
Mfumo wa Makundi ya Damu

Tunapokutana au kujuana na wapenzi wetu, aina ya damu ni miongoni mwa vitu tunavyoshirikiana. Unaweza kusema nina kundi la damu A+ au B-. Lakini unafahamu alama hizo zinamaanisha nini?

Hizo alama ni viashiria vya makundi ya damu zetu. Ni Mfumo wa makundi ya damu tunayomaanisha wakati tukisema ‘A+’ au ‘B-‘ ni mfumo wa ABO na Rh. Zaidi ya hapo tuna mifumo 30 mingine ya makundi ya damu ambayo hutokana na antijeni 300 (seli ndogo ndogo) ambazo zinaunda kinga ya mwili.
Mfumo ABO wa makundi ya damu

Mfumo ABO unatokana na kuwepo au kutokuwepo kwa antijeni A au B kwenye tabaka la seli za damu. K**a una kundi A la damu, ina maana una antijeni A na hivyohivyo kwa kundi B la damu. Lakini vipi k**a una kundi AB au O la damu? Kundi AB la damu linaashiria kuwa una antijeni zote za A na B na kundi O linaashiria kuwa huna antigeni yoyote kati ya A na B.

Jambo linalofuata ni kwanini hatuhamishi damu kutoka baadhi ya makundi kwenda kundi jingine?

Kimsingi, k**a una kundi A la damu, mwili wako utatambua seli za kundi B la damu k**a kitu kigeni na kutengeneza kingamwili (anti-A) dhidi yake. Vile vile kwa watu wenye kundi B watatengeneza kingamwili (anti-A) dhidi ya seli za kundi A la damu.

Hizi kingamwili anti-A na anti-B zitatambua antijeni A na B na zitapingana au kupishana na kusababisha seli kufa. Kwa kesi ya kundi AB la damu, hakuna kingamwili ikiwa na maana kuwa mtu yeyote mwenye kundi lolote la damu anaweza kumpa mtu mwenye kundi AB.
Kwa upande mwingine, mtu mwenye kundi la O la damu anaweza kutengeneza kingamwili zote mbili ikiwa atakutana na kundi lolote la damu, lakini upungufu wa antijeni yoyote inarahisisha kuchangia.

Mfumo wa kundi Rh la damu

Mfumo wa Rh una zaidi ya antijeni 50. Zinazopatikana kwenye mwili wa binadamu ni 5: D, C, c, E na e. Kati ya hizi antijeni D ni muhimu sana kwenye mfumo wa Rh. Kuwepo au kutokuwepo kwa antijeni D kunawakilishwa na alama za chanya (+) au hasi (-).

Ikiwa mtu mwenye damu yenye Rh hasi (Rh-) atakutana na mtu mwenye damu yenye Rh chanya (Rh+), mwili utatengeneza kingamwili ambazo zinataangamiza seli. Hata hivyo, ikiwa damu ya Rh hasi ikihamishiwa kwa mtu mwenye damu ya Rh chanya, hakuna mgongano utakaotokea kwenye antijeni au kingamwili.

Sasa ukisema una AB+, ina maana una antijeni A, B na D, lakini ukisema una O hasi, inaashiria kuwa hauna antijeni yoyote na kingamwili zote.

Kwanini ni muhimu kulinganisha makundi ya damu na mwenza wako?

Hata k**a kuna utofauti wa makundi ya damu hauathiri wanandoa, unaweza kuwa tatizo wakati wa kupata mtoto. Utofauti wa mfumo wa ABO sio jambo kubwa, lakini sio kwa mfumo wa Rh. Kutofautiana au kutoingiliana kwa Rh ni tatizo kubwa ambalo linaweza kumuathiri mama na mtoto.

Wanasayansi wanaeleza, kuwa kutokuingiliana kwa Rh kunatokea wakati mama ana Rh hasi na kichanga kina Rh chanya. Ikiwa damu ya kichanga (yenye Rh chanya) ikivuja na kukutana na mzunguko wa uzazi wa mama (ambao una Rh hasi), seli za kichanga zitatambulika k**a ni za kigeni.

Matokeo yake mama atatengeneza kingamwili inayoitwa Rh immunoglobulin G. Hizi kingamwili zitapita kwenye mfuko wa uzazi na kushambulia seli nyekundu za damu za kichanga kilichopo tumboni. Na seli nyekundu za damu zikiharibika zinatengeneza ‘bilirubin’ ambazo zinasababisha mtoto apate ugonjwa manjano (jaundice).

Kesi k**a hizo za kuvuja kwa damu ya kichanga kwenye mzunguko wa uzazi hutokea zaidi wakati wa kujifungua/kuzaa. Kwasababu hiyo, mama hatengenezi kingamwili za kutosha, mtoto wa kwanza hawezi kudhurika.

Kutokea kwa hali hiyo kutaendelea kuongezeka kwa mimba zinazofuata k**a kichanga kitakuwa na Rh chanya. Na matukio mabaya zaidi kusababisha upungufu wa damu mwilini (Anemia) na kuzaliwa kwa mtoto aliyekufa (stillbirth).

Jinsi ya kutibu

Ikiwa mtoto atazaliwa na Anaemia, ataongezewa maji na huduma ya mionzi ya (bilirubin lights) ili kumtibu na maradhi hayo. Mionzi hiyo inatoa miale (emitting rays of 420-470 nm) inayobalisha bilirubin kwenye mfumo ambao unarahisisha kuondolewa mwilini. Ikihusishwa na kuongezewa maji kunafanya mchakato ufanikiwe kwa haraka.

K**a mtoto atakuwa ana hali mbaya anaweza kuongezewa damu akiwa kwenye mfuko wa uzazi. Sindano inaingizwa kwenye mfuko wa uzazi kwa kutumia mashine ya ultrasound. Uongezaji wa damu unafanyika mara kwa mbili au tatu kabla mtoto hajazaliwa.

Hata k**a matibabu ya Anaemia ni mazuri na yanaweza kuleta matokeo chanya, kinga au uzuiaji ni chaguo zuri. Matibabu ya ‘Rho (D) immune globulin’ yanaweza kutumika kumtibu mama mwenye upungufu wa chembechembe za damu wakati wa ujauzito.

Ikiwa kuna dalili kuwa seli za Rh-chanya zinaweza kuingia kwenye mzunguko wa uzazi, matibabu hayo yanaweza kufanyika katika wiki ya 28 hadi 32 ya ujauzito na saa 72 wakati wa kujifungua.

Uzuiaji wa kutoingiliana kwa Rh ni rahisi sana kuliko maumivu na ugumu unaotokea wakati wa matibabu. Wanandoa wanatakiwa kupima ili kubaini uwezekano wowote wa kutofautiana kwa damu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi.

*FAHAMU TATIZO LA KUUMWA KICHWA KWA MUDA MREFU/MARA KWA MARA  NA SULUHU ZAKE* Tatizo hili la kuumwa na kichwa limegawany...
12/06/2022

*FAHAMU TATIZO LA KUUMWA KICHWA KWA MUDA MREFU/MARA KWA MARA NA SULUHU ZAKE*

Tatizo hili la kuumwa na kichwa limegawanyika katika sehemu kuu nyingi sana japokuwa 1% yake ni ashirio la matatizo ya kiafya ambayo yameadvance sana km vile concusion of brain, meningitis, encephalitis na stroke. Kuumwa na kichwa inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi, vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate. Sehemu ambazo huuma ni k**a mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa, badhi ya neva za fahamu zilizoko usoni.

Yafuatayo ni baadhi ya maumivu ya kichwa....

1. NERVOUS TENSION HEADACHES
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo, kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia Vitamin B2 na C. Punguza au acha matumizi ya sukari, kahawa, chakula chenye kukusababishia mzio, misongo ya mawazo na ufanye mazoezi ya kutosha.

2. CLUSTER HEADACHES
Kichwa kuumwa hasa upande mmoja wa kichwa hasa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na mak**asi kwa mbali. Kitu cha kwanza kufanya ni kutumia chakula chenye protin ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio wako

3. HANG OVER HEADACHES
Hii ni hali ya kuumwa kichwa kutokana na matumizi makubwa ya vinywaji vikali hasa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kisogoni au shingoni, kunywa maji mengi na juice ya matunda fresh au uache kabisa pombe

4. EXERTION HEADACHES
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na hasa kwenye NGONO, Weka barafu eneo linalouma, kula mlo kamili na ufanye mazoezi

5. CAFFEIN HEAD ACHES
Hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa/Energy drinks kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa/energy drinks kuondoa maumivu na upunguze matumizi ya kahawa/energy drinks kidogokidogo mpaka utakapoacha kabisa

6. SINUS HEADACHES
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vyakula vya Vitamin C kwa wingi na umuone mtaalamu wa Afya maana saa zingine hutokana na maambukizi

9. EYES RAM HEADACHES
Hutokea maumivu kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo inaweza kuwa sababu, lakin chanzo chake hasa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha k**a ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuona mtaalam aangalie k**a lensi zimepoteza nuru au laa..

10. MENSTRAL HEADACHES
Hii hutokea kwa akinamama kipindi yai limepevuka. Hutokana na mabadiliko au mvurugiko wa homoni. Hali hii inaweza kuambatana na maumivu ya tumbo. Tumia Virutubisho vya REFINED YUNZHI ESSENSE na FEMICARE humaliza kabisa tatizo hilo.

11. ARTHRITIS HEADACHES
Haya ni maumivu ya kichwa yanayos**ika mpaka shingoni na wakati mwingine mgongoni ambayo busababisha maumivu hasa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo(tatizo la mifupa)Tumia ZAMINOCAL/ANTHROEXTRA humaliza kabisa tatizo hilo

12. HYPERTANTIONS HEADACHES
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu kwa kutumia MICRO2 CYCLE na tatizo hili litaisha kabisa..

📞📲📲✍️ *CALL/WHATSAPP 0758-202801*

🇹🇿✍️ *Afya Kwanza kwa Afya yako*

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿 *UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO - PEPTIC ULCERS*  👉🏿 Vidonda Vya Tumbo ni nini? • Vidonda vya tumbo (Pept...
12/06/2022

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
*UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO - PEPTIC ULCERS*

👉🏿 Vidonda Vya Tumbo ni nini?

• Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) ni ugonjwa unaompata mtu ambapo kunatokea vijitundu au michubuko katika kuta za ndani za viungo vya mfumo wa uyeyushaji chakula.

• Michubuko hiyo huweza kutokea katika eneo la mfuko wa tumbo, katika duodenum au katika eneo la koo. Inakadiriwa kuwa asilimia 5 hadi 10 ya watu hupatwa na ugonjwa huu angalau mara moja katika maisha yao.

• Huu ni ugonjwa ambao unaweza kumrudia mtu baada ya kupona endapo chanzo chake hakikudhibitiwa.

• K**a ugonjwa huu utamrudia mgonjwa , mtu huyu atakuwa amejiweka kwenye hatari kubwa ya kupata madhara makubwa zaidi k**a kutokwa na damu au kutokea tundu kubwa katika kuta za mfuko wa tumbo.

👉🏿 Dalili za Ugonjwa huu.
• Kuchoka choka sana bila sababu maalum.
• Kuuma mgongo au kiuno..
• Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
• Kizunguzungu.
• Kukosa usingizi.
• Usingizi wa mara kwa mara.
• Maumivu makali sehemu ya mwili.
• Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. • Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma k**a sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali
• Kichefuchefu.
• Kiungulia.
• Tumbo kujaa gesi.
•Tumbo kuwaka moto.
• Maumivu makali sehemu kilipo kidonda.
• Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika k**a cha mbuzi
• Kutapika nyongo.
• Kutapika damu au kuharisha.
• Sehemu za mwili kupata ganzi.
• Kukosa hamu ya kula.
• Kula kupita kiasi.
•Kusahahu sahau na Hasira bila sababu.

👉🏿 Chanzo Cha Vidonda vya tumbo ?

• Linapokuja suala la nini husababisha vidonda vya tumbo unaweza ukapata stori nyingi bila idadi, lakini kwa kifupi kabisa; vidonda vya tumbo ni ishara za mwili kupungukiwa maji na k**a matokeo ya asidi kuzidi mwilini kuliko alkaline. Vinaweza pia kuletwa na bakteria ajulikanaye k**a H.Pyroli.

👉🏿 Vitu vifuatavyo vinahusika katika kuleta vidonda vya tumbo mwilini:

• Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu.
• Uvutaji wa sigara.
• Unywaji wa pombe.
• Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha.

👉🏿 Madhara ya Vidonda vya tumbo.

• Uvujaji wa damu ndani ya utumbo:

• Hali hii yaweza kusababishwa na vidonda kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya damu kuanza kuvuja.

• Hali hii ni hatari sana na inahitaji tiba ya dharura.

• Vidonda vya tumbo huweza kusababisha tundu (kutoboka kwa ukuta wa tumbo) na kufanya vitu vilivyo ndani ya utumbo kutapakaa katika tumbo (abdomen) Hali hii huitwa peritonitis na ni hatari sana na inahitaji matibabu ya dharura.

• Aidha, kuenea huko kunaweza pia kuathiri tezi kongosho na kusababisha madhara katika tezi hiyo, ugonjwa unaojulikana k**a pancreat**is.

• Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani k**a vile ini au kongosho (pancrease).
• Kuvimba kwa kuta za tumbo pamoja na makovu yanayosababishwa na vidonda hivi huweza kusababisha kuziba kwa njia ya kupitishia chakula kutoka kwenye tumbo (stomach) kwenda sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenum) hali ambayo kitaalamu huitwa gastric outlet obstruction.

• Iwapo vidonda vya tumbo vimesababishwa na H. pylori, kuna uwezekano wa kati ya mara tatu hadi ya sita ya mgonjwa kupata kansa ya tumbo (stomach cancer).

• K**a wewe ni mmoja wa wanaosumbuliwa na tatizo hili, tafadhali wasiliana nami.

Kupata Tiba isiyo na athari za kikemikali (Tibalishe na virutubisho) na kuweza kumaliza kabisa tatizo hili.

🇹🇿✍️📲📲📲📞📞📞 *CALL/TEXT ME*0758 202801*
Afya Kwanza- Jua afya yako kwa Faida yako.

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

*Habari za muda huu wapendwa🙋🏼‍♀️🙋🏼‍♀️**NAOMBA NIWAKUMBUSHE KITU*📌Ni kuhusu Matumizi holela ya madawa hasa ya antibiotic...
12/06/2022

*Habari za muda huu wapendwa🙋🏼‍♀️🙋🏼‍♀️*

*NAOMBA NIWAKUMBUSHE KITU*
📌Ni kuhusu Matumizi holela ya madawa hasa ya antibiotic k**a wengi walivyozoea kujinywea, sio mazuri kwa afya yako hasa *Afya ya uzazi*

📌Antibiotic zinaua bakteria wabaya na vilevile zinaua bakteria wazuri na walinzi katika uke wako na mwili kiujumla.

📌Yaani inaamaniisha unapomaliza kutumia antibiotic yoyote, unakua katika hatari ya kupata maambukizi kuliko hata kabla hujaanza dozi,*kitaalamu inachukua hadi miezi sita kurudisha jamii ya bakteria wazuri katika mwili mf katika matumbo, uke n.k baada ya matumizi ya dozi moja ya antibiotic, wengine hupata hata tatizo la choo kigumu wakiwa katika dozi hizi, ni kwa ajili mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na bakteria wake unaathiriwa na madawa haya🤔🤔* je k**a umekua ukitumia kwa miezi hadi miaka mfululizo uko kwenye hali gani??🤔🤔

📌 *Chukua jitihada za ziada na umakini wa kujikinga, kula mbogamboga na matunda kwa wingi, kunywa mtindi kwa wingi na chai za mchaichai na tangawizi ukiwa ndani ya dozi na baada ya kumaliza ili kurudisha jamii ya bakteria walinzi katika uke wako (wanawake)ili usipate maambukizi tena kirahisi*

📌 Na ndyo maana tunashauri k**a umekua katika maambukizi sugu kwa mda mrefu miezi kadhaa hadi mwaka na zaidi na umekua katika matumizi ya madawa mda wote huo *HIYO NI HATARI KWA AFYA YAKO YA UZAZI*, geukia tiba tibalishe kupitia package yetu ya Afya ya uzazi itaondoa maambukizi bila madhara huku ikiimarisha kinga yako ya mwili ikiwemo ya uzazi kuongeza nafasi yako ya kushika ujauzito bila kuhangaika.

DONDOO KWA MAMA ANAYENYONYESHA. Maziwa ya mama yana chembechembe nyeupe za damu pamoja na kinga ambayo husaidia kulinda ...
12/06/2022

DONDOO KWA MAMA ANAYENYONYESHA.

Maziwa ya mama yana chembechembe nyeupe za damu pamoja na kinga ambayo husaidia kulinda mtoto asipate mzio (allergy) na maambukizi kwa kuiongezea nguvu kinga ya mtoto. Pia ndicho chakula safi kwa ajili ya mtoto wako, kwani hakiitaji chombo ili kuyafanya kuwa salama.

Zifuatazo ni ndondoo kwa kina mama wanaonyonyesha:

1) Epuka Kuumwa chuchu: Ni muhimu sana unaponyonyesha kutumia mbinu sahihi, ili kuepuka chuchu kupata vidonda. Hii inahusisha sehemu ya chini ya ziwa na chuchu, ambapo chuchu hukutana na midimo ya juu ya mtoto ambayo huchochea unyonyaji

2) Namna ya kunyonyesha:zingatia namna bora za kumweka mtoto kwenye ziwa. Hivi ndivyo unavyopaswa kumweka mtoto kwenye nyonyo..!

Sasa unapomweka mtoto kwenye nyonyo hakikisha amefungua mdomo wote k**a mtu anayepiga mwayo, hii ni tofauti na gepu dogo analofanya mtoto anapokuwa ananyonya kwenye chupa au nyonyo bandia... Na anapoweka nyonyo mdomoni sehemu ya ule weusi unaozunguka t**i (ar**la) iwe inaonekana nje ya mdomo wa mtoto wakati weusi wa chini uwe umefunikwa wote na midomo ya mtoto.. mtoto akiwa hivyo atanyonya vizuri na wewe utakuwa haus**ii maumivu..!

3)Muda wa Kunyonyesha: Kamwe huhitaji kuangalia saa kuona ni muda gani mtoto wako anyonye. Fuata hisia zako. Mnyonyeshe mwanao kila anapolia hata baada ya kumnyonyesha.

4) Msaidie mtoto kutoa hewa: Baada ya kunyonyesha mweke mtoto kwenye bega kisha mpige pige. Hii itamsaidia mtoto kutoa hewa hivyo kupunguza maumivu ya tumbo.

5) Zingatia Usafi: Suuza mat**i na chuchu kwa maji safi. Epuka kutumia sabuni au dawa za kuuwa wadudu kwenye chuchu zako zinaweza kusababisha chuchu kuwa kavu na kuongeza hatari ya kupata vidonda.

Kwa kawaida miili yetu huzalisha mafuta ambayo husaidia kulinda chuchu. Kupaka kiasi kidogo cha maziwa baada ya kunyonyesha husaidia kulainisha chuchu. Muone daktari iwapo chuchu zako zinauma au zinavidonda.

Kwa ushauri zaidi kuhusu mambo ya Kiafya.
Piga/WhatsApp 0758202801

25/05/2022

LISHE

1. Badilisha chakula chako kila mlo, lakini usile vyakula vya aina
nyingi sana katika mlo mmoja. Iweke milo yako na chakula chako
unachopakua kuwa rahisi.

2. Tumia zaidi nafaka zisizokobolewa kwa mashine k**a mkate wa ngano
isiyokobolewa na mchele usiokobolewa kwa mashine. Tumia kwa nadra sana
chakula kilichotayarishwa kutokana na unga mweupe wa ngano na mchele
mweupe.

3. Punguza kula vyakula vitamu sana. Utumie kiwango kidogo sana cha
sukari, chumvi na mafuta ya kila aina. Epukana na viungo vinavyonukia,
mafuta ya mgando{grease} hasa mafuta ya nguruwe, hamira,
mgadiyanayotumika kwa kupikia na s**i.

4. Ule kwa wakati uleule uliowekwa kwa milo kila siku, na acha
anagalau masaa matano yapite kutoka mlo mmoja hadi mwingine. Mfumo wa
kuyeyusha chakula unafanya kazi yake vizuri sana ukiwekewa ratiba
linganifu na uile milo usiku sana.

5.Usile katikati ya milo. Kula katikati ya milo kunapunguza kasi ya
tumbo kukitoa chakula kilichomo na kusababisha chakula hiki kuchachuka
kikiwa bado tumbani.

6. Ule chakula cha kutosha hasa asubuhi. Hicho ndicho kingekuwa mlo
wako mkubwa kuliko yote kila siku. Ule chakula chako cha jioni angalau
masaa mawili au matatu hivi kabla ya kwenda kulala.

7. Ule chakula unachohitajiili kuhifadhi afya yako, nawe ukifurahie
ila usile chakula kupita kiasi. Kula chakula kingimno huipumbaza
akili, huleta uchovu, huongeza magonjwa na kupunguza maisha yako.

8. Kula polepole na kukitafuna chakula chako vyema kutaongeza furaha
yako na manufaa ya virutubisho vya lishe hiyo mwilini mwako. Wakati wa
mlo uwe wa furaha na usiharakishwe, usitafune chakula kwa muda mfupi
sana, usileusile haraka harakr na usiweke chakula kingi mno
kinywani.

9 Unywe maji ya kutosha kila siku ili kuufanya mkojo wako kuwa mweupe,
lakini usinywe maji pamoja na milo yako ama muda mfupi tu kabla au
baada ya milo yako. Maji au kinywaji kingine chochote kinachonywewa
wakati wa milo huchelewesha uyeyushaji na utoaji wa chakula
kilichoyeyushwa tumboni. Kukaa kwa chakula tumboni kwa muda mrefu
hukichachusha na hiyo ni mojawapo ya sababu za kawaida sana zinazoleta
vidonda vya tumbo na ugonjwa wa tumbo{gastritis}

10. Ruka mlo mmoja mpaka mine kila baada ya kipindi Fulani kupita.
Kufunga ni msaada wa kuidabisha hamu ya kupenda sana kula chakula na
tena ni mazoezi ya kuitawala nafsi yako. Kufunga ni dawa bora sana ya
magonjwa mengi sana, hasa kwa watu wale wasiofanya kazi nyingi na
ngumu za mikono.

11. katika mlo wako epuka:
{a} Pilipili kali zote na viungo vinavyonukia{tangawizi, dalasini,
karafuu, basibasi}
{b} s**i au kitu chochote kilichotengenezwa kwa s**i {achali, mchuzi
wa mayai uliotiwa mafuta na s**i [mayonnaise], kachumbari[catsup].
Haradali na kadhalika}
{c}Vyakula ambavyo vinachachuka, vinatoa uvundo, ama vinakuwa katika
hali ya kuoza wakati wa kuvitayarisha, k**a vile, mchuzi mchungu wa
kabeji iliyokatwakatwa k**a kachumbari na kutiwa chumvi ya maji ya
bahari [sauerkraut], jibini, mchuzi wa soya na vitu vingine k**a
hivyo.
{d} Magadi, hamira na aina zake zote hasa pamoja na mikate myembamba
migumu, biskuti, maandazi na vitu vingine vilivyopokwa.
{e} Kafini [kahawa, majani ya chai, vinywaji vya kola] na chokolet

12. Usile vyakula vizito sana. Hivi ni pamoja na vyakula vyenye sukari
nyingi, mafuta yaliyosafishwa sana kwa mashine, vitamini na madini
zilizotengenezwa ama protini [concentrated proteins] nzito k**a nyama
na vitu vingine vitokavyo na wanyama k**a maziwa, mayai na kadhalika.

13. Matunda na mboga za majani visiliwe katika mlo uleule mmoja na
usile matunda mabichi sana ama yaliyoiva sana.

14. Vyakula visiliwe vikiwa bado ni vya moto sana ama vya baridi sana
na visiliwe mapema zaidi kabla masaa yaliyopangwa kufika.[masaa matano
kati ya milo]

2.MAZOEZI YA VIUNGO

KANUNI ZA MAZOEZI YALETAYO AFYA
1. Mazoezi lazima yawe ya kuendelea [ya kila siku] ili yaweze kuleta
manufaa mwilini angalau zitumike dakika 30 kwa siku.

2. Mazoezi ya viungo hayana budi kuwa mepesi na yasiwe ya kutumia
nguvu nyingi [kupita kiasi].

3. Mazoezi ya viungo shart yawe ya aina mbalimbali[k**a vile kulima
bustani] ili misuli yote ya mwili ipate kutumika vizuri.

4. Mazoezi ya viungo hayana budi fufurahiwa ili yaweze kuleta manufaa
ya kutosha mwilini.

FAIDA YA MAZOEZI YA VIUNGO

1. Mazoezi ya viungo huimarisha mifupa na misuli.

2. Mazoezi ya viungo yanaharakisha MZUNGUKO wa damu kwenda katika
sehemu zote za nyama ya mwili wetu

3. Mazoezi ya viungo huoneza utendaji bora wa moyo

4. Mazoezi ya viungo huongeza utendaji bora wa mishipa ya damu.

5. Mazoezi ya viungo yanasaidia kudhibiti ugonjwa wa shinikizo la damu
[blood pressure]

6. Mazoezi ya viungo yanasaidia uyeyushaji wa chakula wakati mtu
anapotembea mara tu baada yam lo akiwa ameinua kichwa chake juu na
kuyaweka mabega yake nyuma

7. Mazoezi ya viungo yanachelewesha kuzeeka

8. Mazoezi ya viungo yanausaidia mwili kuwa na uzito wake unaofaa si
mnene kupita kiasi wala mwembamba kupita kiasi

9. Mazoezi ya viungo yanapunguza msongo[stress] unaoleta
unyong`onyevu[depression] au magonjwa ya akili. Yanamfanya mtu
ajis**ie ameburudika

10. Mazoezi ya viungo yanauimarisha mfumo mzima wa kujikinga na
maradhi kwa njia hiyo kuusaidia mwili kutopatwa na magonjwa ya
kuambukiza pamoja na mafua

11. Mazoezi ya viungo yanaboresha utendaji wa akili na kukuza fikra
safi

3. MAJI
Mwili unahitaji theluthi zaidi ya majiyanayohitajika wakati wa kiu.
Utaratibu wa kudumu ufuatao utakusaidia kukidhi mahataji ya maji

mwilini. Kunywa maji bilauri 2 za maji mara tu unapoamka asubuhi,
bilauri 2 kati ya asubuhi na adhuhuri na bilauri 2 kati ya masaa ya

mchana. Unywe maji mengi ya kutosha kuufanya mkojo wako ufanane na
maji safi. Kumbuka kwamba hali zinazosababisha kupotea kwa maji mengi
mwilini zinahitaji kufidiwa kwa kunywa maji mengi sana .

MATUMIZI YA MAJI NDANI YA MWILI

Mwili uanapendelea maji ya moto kidogo kuliko yale ya uvuguvugu.maji
yakiwa ya baridi sana yanasimamisha kazi ya kuyeyusha chakula
tumboni[k**a yamenywewa wakati wa mlo] na tena yanazipunguza ishara

zilizomo mwilini mwetu zinazotujulisha tunapokuwa na kiu. Wakati bora
wa kunywa maji na ule ulio katikati ya milo. Epuka kunywa maji katika
dakika 30 kabla ya mlo na saa 1-2 baada kumaliza mlo. Kunywa maji

pamoja na milo hupunguza nguvu ya uyeyushaji chakula mwilini [enzymes]
na kuchelewesha uyeyushaji wa chakula hicho. K**a mwili unapungukiwa
na maji basi mkondo wake wa damu utakwenda polepole na mwili wote
utaadhirika. Nmatumizi mengine ya maji ni k**a ifuatavyo:

1. Hutengeneza mate kinywani

2. Hutengeneza machozi katika macho

3. Hurekebisha joto la mwili kuwa katika kiwango kinacholeta afya
mwilini na yanasaidia kutelemsha homa

4. Hulainisha viungo vya mwili[joints] pamoja na misuli

5. Huzuia na kupunguza uchovu wa mwili
6. Huzuia na kupunguza uchovu na unyong`onyevu wa mwili

Vilevile kuoga kila siku na maji ya uvuguvugu au yaliyopoa kuna
manufaa yafuatayo kiafya:

1. Kunauimarisha mwili ili uweze kujikinga na mafua na magonjwa
mengineyo
2.Kunauboresha mzunguko wa damu mwilini
3.Kunaburudisha na kuutia nguvu mwili
4. Kunatia nguvu ubongo, kunauchangamsha akili na kuzituliza neva
5. Kunaongeza uwezo wa misuli kunyumbuka
6. Kunavisaidia viungo vinavyoyeyusha chakula [tumbo la chakula, ini
na matumbo]

4. MWANGA WA JUA

FAIDA ZA MWANGA WA JUA
1. Unaongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini

2. Unaongeza wingi wa damu inayotoka Moroni

3. Unaongeza uwezo wa damu kusafirisha oxgen

4. unasaidia kuratibisha mwilini shinikizo la damu [blood
pressure] kubakia pale kinapohitajiwa

5. unaongeza idadi ya chembechembe nyeupe za damu na uwezo wao
wa kupigana na maambukizo

6. unaongeza protini iitwayo 'gamma globulin' inayosaidia mwili
kupigana na maambukizo

7. unaongeza utendaji kazi wa ini na kuriharikisha kutengeneza
dawa ya kuyeyusha chakula. Pia inaongeza uwezo wa mtu kustahimili
mazingira yasiyo safi

8. unaimarisha viwango vya sukari katika damu mwilini.
9. unapunguza kiwango cha mafuta katika damu. Mwanza wa jua
unaweza kupunguza kiwango cha kolestero kwa zaidi ya asilimia 30

10. Mwanga wa jua unaigeuza kolestero na egestero katika ngozi kuwa
vitamina D

11. unaongeza nguvu ya misuli na kuiwezesha kudumu

12. unaongeza uyeyushaji wa chakula mwilini

13. ni tiba inayofaa kwa ugonjwa wa manzano wa ngozi na macho
unaowapata watoto wachanga

14. unaboresha mtizamo wa kiakili na afya mwilini. Unasaidia kuzuia au
kuufanya unyong`onyefu wa akili kuwa nafuu zaidi

15. unapunguza msongo [stress] kwa kufanya kazi kupitia katika neva
zinazopokea ambazo zimo katika ngozi ya mwili wetu na pia kupitia
katika mambo ya kisaikolojia yanayochangia

16. unaendeleza uponyaji. Elekeza sehemu za mwili zilizoambukizwa
kwenye Mwanza wa jua. Kuota jua kwa muda mfupi mara cada kwa situ
kunaweza kuua vijidududu vya magonjwa na kusaidia kupona kwa majeraha

17. unasaidia kuviondoa vijidudu viletavyo magonjwa katika nyumba
zetu.

JINSI YA KUYAEPUKA MADHARA YA JUA

1. pata jua kwa kiwango kidogo kinachoongezeka taratibu. Epuka
kuunguzwa na jua k**a unavyoepuka sumu

2. punguza kujianika juani wakati wa kiangazi hadi wakati wa
adhuhuri[ saa4 hadi saa 9]

3. unapokuwa nje vaa nguo zinazokuhifadhi na kofia pana, nguo
nyepesi zinaweza kunyonya baadhi ya mionzi ya jua

5. KIASI

Kiasi au kujinyima maana yake ni kujikana nafsi, kutumia kwa kiasi
[sio kupita kiasi kile ambacho ni kizuri na kutotumia kabisa kile

kinacholeta madhara mwilini. Kiasi kiwe mazoea katika maisha yetu ya
kila siku :lishe, kazi, kulala usingizi, kujifunza, na kuvaa vizuri.

Epukana kabisa na nyma iliyo najisi na vitu vyote vinavyoleta madhara
mwilini k**a alkoholi, tumbako[sigara] na vitu vyote vilivyo na

kafini[caffeine] k**a majani ya chai, kahawa na vinywaji vya kola.
Kuvunja kanuni hii ya afya kuna athari kubwa sana. Kutokuwa na kiasi
ndio msingi wa maovu yote katika ulimwengu wetu.

6. HEWA SAFI

Mwanadamu angeweza kuishi majuma 5 mpaka 6 pasipo kula chakula siku
chache bila kunywa maji lakini kwa dakika chache tu bila hewa. Hewa

safi inaburudisha mwili na akili. Mwili unanufaika zaidi kutokana na
mazoezi yanayofamyika nje ya nyumba kuliko ndani ya nyumba. Hewa safi
kotoka nje inanufaisha mwili na akili kwa njia zifuatazo:

1. inafanya damu kuzunguka mwilini na kuleta afya

2. inaburudisha mwili—inasaidia kuwa na nguvu na afya

3. inazituliza neva—inafanya akili itulie na kuwa na ukunjufu

4. inaamsha hamu ya kula chakula na kukisaidia chakula kuyeyushwa
kikamilifu

5. inaleta usingizi mzito na mtamu

KUVUTA PUMZI IPASAVYO
1. jizoeze kusimama au kukaa vizuri. Simama na kukaa wima na kwa
urefu. Weak mabega yako nyuma na kuyaelekeza chini. Mitulinga iytakuwa
imevutwa karibu pamoja jambo ambalo hukisaidia kiwambo cha moyo
[diaphragm] kufanya kazi yake kwa uhuru

2. kusoma kwa sauti kubwa humsaidia mtu kuitoa hewa nje ipasavyo

3. kupanda ngazi za nyumba au vilima humsaidia mtu kuvuta pumzi. Vuta
hewa ndani kwa hatua mbili, kasha itoe nje kwa hatua mbili zinazofuata
na kadhalika

7 PUMZIKO
Pumzio ni la muhimu kabisa katika maisha yetu- kwa afya ya mwili na
akili. Badala ya kupumzika na kuacha kazi zote badiliko katika aina ya

kazi linaweza kuleta manufaa katika afya ya mtu. Kwa mfano kuacha kazi
ya kutumia akili kwenda kazi ya kutumia mikono inweza kuwa na manufaa
kwa mwanafunzi. Karibu theluthi ya maisha yetu inatumika kwa kulala

usingizi. Wakati wa kulala nguvu zaakili hurejeshwa upya. Usingizi
unaofaa sana ni ule unaopatikana kabla ya usiku wa manane. Kwa
usingizi bora saa ya kwenda kulala isiwe baada ya saa 4 usiku.

Tumalala vizuri sana k**a tumbo letu pia linaweza kupumzika kutopkana
na kazi yake ya kuyeyusha chakula angalau masaa 3 baada ya kula

chakula. Usingizi unaoleta pumziko la mwili unasaidiwa na:
• chumba kitulivu, cha giza, chenye hewa ya kutosha wakati wote
• tumbo tupu [angalau saa 3 baada ya kula chakula]
• kufanya shughuli za mwili za wastani kabla ya kwenda kulala
• dhamiri safi—moyo ulio na amani na Mungu.

Address

Gongo La Mboto
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Kwanza. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya Kwanza.:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram