09/04/2026
🔴 VIJUE VYAKULA MUHIMU KWA AFYA YA MIFUPA NA MAUNGIO
Mifupa imeundwa kwa madini mbalimbali ikiwemo madini ya calcium na phosphorus kwa kiasi kikubwa hvyo ili uweze kuwa na mifupa imara unahitaji kula vyakula vyenye calcium na phosphorus kwa wingi.vyakula hvyo ni k**a ifuatavyo
⚫Samaki.
samaki wana madini k**a calcium ambayo ni muhimu katika mifupa pia mafuta ya samaki (omega 3 fatty acids) yana umuhimu sana katika afya ya mifupa pamoja na mfumo wa damu.
⚫Mboga za majani.
tunapata calcium na vitamin mbalimbali ambavyo vinaweza kuimarisha mifupa na viunga pia zina uwezo wa kuzuia vimeng’enya hatari vinavyoweza kusababisha kuvimba na maumivu katika viunga.
⚫Matunda.
baadhi ya matunda yana lycopene na anthocyanins na vitamin C ambazo huepusha madhaifu ya mifupa matunda hayo ni k**a machungwa, nyanya,limao, strawberries, ndizi mbivu nk
⚫Mafuta.
vyakula vyenye kiasi kikubwa cha omega 3 mfano mafuta ya parachichi na mafuta ya mzeituni
⚫Maharage.
baadhi ya maharage ni mazuri katika afya mifupa mfano maharage ya
soya,maharage meusi nk haya virutubisho ambavyo vinaweza kuimarisha mifupa.
⚫Maziwa.
maziwa yana calcium na vitamin mbalimbali ikiwemo vitamin D ambayo husaidia ufyonzaji mzur wa calcium.
⚫Mayai.
Haya yana madini mbalimbali ikiwemo calcium na vitamins kwa wingi hvyo husaidia kuwa na mifupa imara.
⚫Vyakula vyenye phosphorus ni k**a ndizi mbivu,apples, broccoli,maharage nk
Tumekuandalia virutubisho lishe vya asili vimeandaliwa kwa kiasi ambacho kinahitajika na mwili kwa ajili ya kuimarisha mifupa vina uwezo wa kumsaidia mtu anayesumbuliwa na mifupa na kusuluhisha tatizo lake. Kwa maelezo zaidi na kupata virutubisho lishe wasiliana nasi kwa namba 0672441815