18/04/2025
YAJUE MAAMBUKIZI YA KWENYE NJIA YA MKOJO (Urinary tract infection -UTI).
UGONJWA WA UTI (Urinary Tract Infection)
Mfumo wa mkojo wa mwanamke (Female urinary system)
UTI ni Maambukizi kwenye njia ya mkojo katika sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo yaani figo, ureter, kibofu na urethra(mrija wa kutoa mkojo). Maambukizi mengi huhusisha sehemu ya chini yaani kibofu na urethra.
Wanawake wako kwenye hatari kubwa kupata UTI kuliko wanaume, Maambukizi yaliyo kwenye kibofu yanaweza kusababisha maamivu makali au kero, Ingawa, tatizo la UTI linaweza kutokea ikiwa maambukizi yatasambaa mpaka kwenye figo zako.
Madaktari hutibu UTI na dawa za kuua bacteria yaani (Antibiotics), Lakini unaweza kupunguza nafasi kwako wewe kupata UTI katika nafasi ya kwanza.
Ishara na Dalili (Signs and Symptoms).
Maambukizi njia ya mkojo mara zote hayaoneshi ishara na dalili, lakini yanapoonesha dalili huwa ni pamoja na;
-Mkojo kuunguza au kuwasha.
-Kuojoa kwa shida.
-Kukojoa mkojo kidogo sana .
-Mkojo uliochanganyikana na weupe ndani yake .
-Mkojo wenye rangi nyekundu au pinky ishara ya damu ndani ya mkojo.
-Mkojo wenye harufu kali.
-Maumivu chini ya kitovu hasa kwa wanawake. au maumivu yanayotokea eneo la kinena.
UTIs ikiachwa au isipotibiwa husababisha madhara zaidi.
Aina za maambukizi ya kwenye njia ya mkojo (Types of urinary tract infection)
Kila aina ya UTI inaweza kuja na dalili zake, kutegemeana na eneo lililoathirika.
Ishara na dalili (Signs and symptoms).
-Maambuikzi kwenye Figo (Kidneys −acute pyelonephritis.
-Homa ya juu (High fever).
-Kutetemeka.
-Kutoka damu puani (Nausea).
-Kutapika (Vomiting).
-Maambukizi kwenye kibofu (Bladder —cystitis).
-Eneo la chini ya kitovu kukaza.
-Maumivu ya chini ya kitovu.
-Maumivu ya mara kwa mara wakati wa kukojoa (Frequent, painful urination).
-Mkojo wenye damu (Blood in urine).
-Maambukizi kwenye mrija wa mkojo Usaha/ majimaji kutoka kwenye uume/uke, vipele au miwasho hali ijulikanayo k**a (Urethra −urethritis).
-Mkojo kuwasha/kuunguza ( Burning with urination).
-Kutoka usaha au uteute (Discharge).
Kumuona daktari ( to see a doctor)
Muone daktari endapo una ishara au dalili za UTI s
Sababu za UTIs (Causes)
UTIs hutokea pale bacteria wanapoingia kwenye njia ya mfumo wa mkojo kupitia urethra (mrija wa mkojo) na kuanza kuongezeka kwenye kibofu cha mkojo. Ingawa mfumo wa mkojo umetengezwa kujiendesha kuwazuia bacteria (microscopic), wakati mwingine ulinzi huu hushindwa . hali hiyo mara itokeapo, bacteria huingia na kuanza kukua na kupelekea maambukizi ndani ya mfumo wa mkojo.
Sehemu kubwa UTI hutokea kwa wanawake na kuathiri kibofu na urethra (mrija wa mkojo).
Maambukizi ya kwenye kibofu (Infection of the bladder −cystitis), Aina hii ya maambukizi ya njia ya mkojo husababishwa na Escherichia coli (E. coli), ni aina ya bacteria wanaopatikana kwenye mfuko wa tumbo (gastrointestinal −GI). Ingawa wakati mwingine Bacteria wengine huhusika.
Kujamiiana kunaweza kupelekea maambukizi ya kwenye kibofu (cystitis), huhitaji kujamiiana ili uendeleze maambukizi, Wanawake wote wapo kwenye hatari kubwa kupata maambukizi ya kwenye kibofu (cystitis) kwa sababu ya maumbile yao (anatomy — specifically), umbali mfupi uliopo kati ya urethra (mrija wa mkojo ) na njia ya kutolea kinyesi (Mkundu ) na mrija unaofungua kwenye kibofu huongeza hatari ya maambukizi.
Maambukizi kwenye mrija wa mkojo (Infection of the urethra −urethritis).
Aina hii ya maambukizi hutokea pale bacteria wanaposambaa kutoka kwenye utumbo (GI) kupitia kwenye njia ya kutolea kinyesi (Mkundu ) mpaka kwenye urethra (mrija wa mkojo). Pia kwa sababu wanawake mrija wao wa mkojo (urethra) uko karibu sana na uke, maambukizi ya magonjwa ya ngono k**a HERPES, KISONONO, KASWENDE na MYCOPLASMA, zinazeza kusababisha maambukizi kwenye mrija wa mkojo (urethritis).
Vihatarishi (Risk factors)
Maambukizi ya njia ya mkojo ni mengi kwa wanawake, na kila mwanamke anao uzoefu zaidi ya mara moja wa maambuki ya UTI katika maisha yao. Hatari za maambukizi ya UTI kwa wanawake ni pamoja na;
Maumbile ya Mwanamke (Female anatomy).
Mwanamke ana urethra (mrija wa mkojo) fupi kuliko mwanaume, hupunguza pia umbali wa bacteria kusafiri mpaka kufika kwenye kibofu.
Kufanya Mapenzi (Sexual activity).
Wanawake wanaofanya mapenzi mara kwa mara wako kwenye hatari zaidi ya kupata UTI kuliko wanawake wasiojihusisha na mapenzi. Kuwa na mpenzi mpya hukuweka katika hatari zaidi.
Baadhi ya vizuia mimba (birth control).
Wanawake wanaotumia vitanzi kupanga uzazi wako kwenye hatari kubwa, vile vile na wanawake wanaotumia vizuia mbegu.
Kukoma hedhi (Menopause),
Baada ya kukoma hedhi, kupungua kwa mzunguko wa estrogen husababisha mabadiliko katika mfumo wa mkojo na kuongeza hatari ya maambukizi.
Sababu nyingine zinazochochea kupata UTIs ni pamoja na;
Maumbile ya mfumo wa mkojo yasiyo kawaida.
Watoto waliozaliwa na hali isiyokawaida ya mfumo wa mkojo ambao hauruhusu mkojo kutoka nje ya miili yao na kuurudhisha kwenye urethra wana hatari ya kupata UTIs.
Kuharibika kwa mfumo wa mkojo. Mawe kwenye figo au kuvimba kwa tezi dume kunaweza kuzuia/kubakiza mkojo kwenye kibofu na kuongeza hatari ya kupata UTIs.
Kushuka kwa kinga za mwili.
Kisukari na magonjwa mengine ambayo hupunguza kinga za mwili yanaweza kuongeza hatari ya kupata UTIs.
Matumizi ya Catheter.
Watu ambao hawawezi kukojoa na wanatumia mrija (catheter) kukojoa wanaongeza hatari ya kuapata UTIs. Hii inaweza kuhusisha na watu walolazwa hospitalini, watu wenye matatizo ya mfumo wa mishipa ya fahamu inayowapa ugumu wa uwezo wa kujidhibiti kukojoa na watu waliopararaizi.
Upasuaji.
Upasuaji katika mfumo wa mkojo au shughuli inayohusu uwekaji wa vifaa kwenye mfumo wa mkojo zote zinaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi njia ya mkojo —UTIs.
Madhara ya UTIs
Unapotibiwa kwa uhakika, maambukizi ya sehemu ya chini hupona, k**a haitatibiwa, maambukizi ya mfumo wa mkojo hupelekea tatizo kuwa baya zaidi.
Athari za UTIs ni pamoja na;
-Maambukizi kurudi tena, hasa kwa wanawake ambao wameshapata maambukizi zaidi ya mara mbili ndani ya miezi sita au nne ai zaidi ya mwaka.
-Uharibifu wa kudumu wa figo au maambukizi sugu ya kwenye figo (pyelonephritis) kutokana na UTIs ambayo haijatibiwa.
-Kuongeza hatari ya wanawake wajawazito kujifungua mapema au mtoto mwenye uzito mdogo.
-Kuziba kwa miriija ya mbegu kwa mwanaume kutokana na uwepo wa maambukizi ya njia ya mkojo (urethritis).
-Tatizo la Maambukizi sugu, hasa maambukizi yanayotokea kwenye figo.
Njia za kuzuia UTIs (Prevention)
Unaweza kuchukua hatua hizi kupunguza hatari za maambukizi kwenye mfumo wa mkojo.
Kunywa maji mengi.
Kunywa maji mengi husaidia ku-dilute mkojo na kuhakikisha unakojoa mara kwa mara, huruhusu bacteria kutoka kwenye mfumo wa mkojo kabla ya maambukizi kuanza.
Kunywa juisi ya cranberry. Ingawa juisi hii ya cranberry haijathibitishwa kabisa kuwa inazuia UTIs, haina madhara.
Tawaza kutoka mbele kwenda nyuma.
Kufanya hivyo baada ya kukojoa au haja kubwa husaidia kuzuia bacteria kuhama kutoka sehemu ya haja kubwa (mkundu) kuja kwenye uke au urethra.
Safisha kibofu chako baada tu ya kufanya mapenzi. Pia kunywa glasi iliyojaa ya maji kusaidia kuondoa bacteria.
Zuia matumizi ya bidhaa za kemikali zinazotumika kupuliziwa ukeni. Matumizi ya urembo k**a sprays au urembo mwingine k**a vile wa kuoshea uke (douches) na poda (powders), katika eneo la uzazi inaweza kuathiri urethra.
Badilisha njia zako za kupanga uzazi (Change your birth control method). Vitanzi na kondomu zenye vilainishi, zote hizi zinaweza kuendelea kuzidisha kuongezeka kwa bacteria.
Kwa huduma za matibabu, kwa wenye changamoto za kiafya, Wasiliana nasi namba zipo kwenye ukurasa huu lakini pia hata kwenye post hii. Zingatio la muhimu kuwa makini epuka kutapeliwa, hakikisha namba zinatoka kwenye kurasa zetu rasmi,
Piga/SMS au WhatsApp:0688757052