
14/07/2025
🏆 Tumeshinda tena! Kwa mwaka wa tatu mfululizo, Smiles Dental Clinic imetunukiwa Mshindi wa Tatu wa Banda Bora katika sekta ya afya kwenye Maonesho ya 49 ya Sabasaba!
Tuzo hii imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Selemani Jafo (.selemani_jafo)Asante kwa kutambua juhudi zetu za kutoa huduma bora za afya ya kinywa na meno kwa jamii yetu.
Kwenye banda letu, tulitoa elimu, ushauri, na uchunguzi wa awali wa afya ya kinywa, tukiwahudumia mamia ya wananchi kwa moyo mmoja na tabasamu.
Asante kwa kila mmoja aliyejitokeza, kwa kutuamini, kutusapoti na kuwa sehemu ya safari yetu.
Tunaendelea kujivunia kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika afya ya Watanzania.