Ushauri_wa_mahusiano_na_maisha

Ushauri_wa_mahusiano_na_maisha Ushauri &Tiba kuhusu​�
�Maisha
�Mahusiano
�uchumba&Ndoa
�Malezi
�Stress
�Gharama Tsh 20,000 kwa simu 50,000 face 2 face
�MACHOZI

CONFESSION 😔Nilikuwa na mwanaume mmoja, alinipa wakati mgumu sana mpaka ikafika siku akaniambia anataka “open relationsh...
21/03/2026

CONFESSION 😔
Nilikuwa na mwanaume mmoja, alinipa wakati mgumu sana mpaka ikafika siku akaniambia anataka “open relationship”… yaani yeye aendelee na mwanamke wake, na mimi nitafute mwanaume wangu halafu bado tuendelee 😳
Siku hiyo ndio niligonga muhuri… nikajua kabisa huyu sio mtu wangu.
Nilimuambia: “Nimevumilia mengi, lakini leo umenithibitishia sina thamani kwako.”
Nikaondoka… na safari hii sikurudi nyuma.
Cha ajabu, baada ya k**a wiki moja tu, mwanaume mwingine akanifuata. Sijawahi hata kuwa naye kwenye mahusiano, lakini akasema ananipenda tangu muda na anataka kunioa.
Leo hii mimi ni mke wa mtu… nashukuru Mungu kwa hilo ❤️
LAKINI… maisha hayako perfect k**a nilivyodhani.
Mume wangu: Ananilipia kodi ✔️
Anatoa pesa ya kula kila siku ✔️
Analipa umeme na maji ✔️
Lakini mimi k**a mke wake… sina matunzo kabisa.
Hajawahi kuninunulia hata mafuta ya kupaka.
Hajawahi kuninunulia hata pedi.
Kila kitu najinunulia mwenyewe.
Nikiuliza thamani yangu iko wapi, anaishia kusema nina gubu 💔
Kuna muda namuuliza kitu anakaa kimya kabisa, mpaka nirudie tena ndipo ajibu kwa hasira.
Anasema hana pesa…
Lakini najiuliza, kweli mwanaume unashindwa hata 5,000 ya kumjali mke wako?
Mpaka nimefikia hatua nimejinyoa nywele zangu nzuri kwa sababu sina hela ya kuzihudumia mara kwa mara… na yeye hajali 😔
Nawaza sana… nachoka.
Je, hii ndio ndoa kweli?
Au nimeolewa ili niwe mfanyakazi wa ndani tu?
Nisaidieni mawazo… 😭

Ninaandika hii confession kwa maumivu makubwa moyoni. Mimi ni mwanamke mwenye ndoa ya miaka 6 sasa. Tulioana kwa mapenzi...
10/03/2026

Ninaandika hii confession kwa maumivu makubwa moyoni. Mimi ni mwanamke mwenye ndoa ya miaka 6 sasa. Tulioana kwa mapenzi makubwa sana. Mwanzoni maisha yalikuwa mazuri, mume wangu alikuwa mtu wa kunijali, kunipa muda na kuniheshimu.
Kila mtu aliyetuona alisema sisi ni couple ya mfano. Nilijivunia ndoa yangu.
Lakini kadiri miaka ilivyokwenda mambo yakaanza kubadilika polepole.
Mume wangu alianza kuchelewa kurudi nyumbani. Simu yake ikawa siri kubwa sana. Zamani alikuwa anaacha simu mezani hata nikiishika hakujali, lakini ghafla akawa anaweka password na hata nikiiangalia tu anakuwa mkali.
Nilianza kupata hisia kuwa kuna kitu kinaendelea lakini sikuwa na ushahidi.
Siku moja nilimuuliza kwa upole: “Mbona siku hizi unachelewa sana kurudi nyumbani?”
Alijibu kwa hasira kidogo: “Kazi zimekuwa nyingi, acha kunichunguza kila kitu.”
Nilinyamaza. Lakini moyo wangu haukuwa na amani.
Wiki kadhaa baadaye tukawa tumelala usiku. Ghafla simu yake ikaita saa 2 usiku. Alikuwa usingizini sana hivyo hakuweza kuisikia haraka.
Nilipoangalia screen niliona jina lililoandikwa “Baby ❤️”.
Mapigo ya moyo wangu yaliongezeka ghafla.
Nilihisi k**a dunia imenisimama.
Sikumwamsha. Nilikaa kimya mpaka simu ilipoacha kuita. Lakini sikuweza kulala tena usiku ule.
Asubuhi alipoamka nilijifanya kawaida, lakini kichwani nilikuwa na maswali mengi sana.
Siku hiyo nilifanya kitu ambacho sikuwahi kufanya katika ndoa yetu. Nilipoona anaoga nilichukua simu yake na kujaribu kuifungua.
Kwa bahati mbaya password ilikuwa tarehe yangu ya kuzaliwa.
Nilipofungua WhatsApp niliona mazungumzo mengi sana na mwanamke mmoja. Maneno yao yalikuwa ya kimapenzi sana… yale yale ambayo zamani alikuwa akiniambia mimi.
Lakini kilichoniumiza zaidi ni pale nilipoona ujumbe mmoja ukisema:
"Nimekosa sana kulala na wewe, mke wangu huwa hashtuki hata nikirudi usiku sana."
Nilianza kutetemeka.
Sikujua k**a nilie au nipige kelele.
Nilifunga simu nikairudisha mezani. Nilikaa kitandani nikijiuliza maswali mengi:
Je ndoa yangu ilikuwa uongo ?

📌 “Wakati mwingine maumivu makubwa kwenye ndoa si kukosa mapenzi… bali kukosa kusikilizwa.”🗣️ Ndoa si kuishi pamoja tu,n...
27/02/2026

📌 “Wakati mwingine maumivu makubwa kwenye ndoa si kukosa mapenzi… bali kukosa kusikilizwa.”
🗣️ Ndoa si kuishi pamoja tu,
ni kusikilizana.
Ni kuelewana.
Ni kuheshimiana.
💭 K**a sauti yako haisikiki,
hisia zako hazipewi nafasi,
mawazo yako hayathaminiwi…
❓ Bado unaweza kuiita ndoa yenye amani?
❤️ Ndoa ya kweli hujengwa kwa mawasiliano,
sio kimya cha maumivu.

Mimi ni mwanaume wa miaka 29.Miaka mitatu iliyopita nilikuwa kwenye mahusiano ya miaka minne na msichana niliyempenda kw...
24/02/2026

Mimi ni mwanaume wa miaka 29.
Miaka mitatu iliyopita nilikuwa kwenye mahusiano ya miaka minne na msichana niliyempenda kwa dhati. Tulikuwa na mipango mingi — ndoa, watoto, maisha ya pamoja.
Lakini maisha yalibadilika ghafla.
Kampuni niliyokuwa nafanya kazi ilifunga tawi lake. Siku moja niliitwa ofisini na kupewa barua ya kuachishwa kazi.
Nilirudi nyumbani nikiwa nimevunjika moyo. Nilimwambia mpenzi wangu kwa matumaini angenipa faraja.
Mwanzoni alinionyesha kunielewa.
Lakini kadri miezi ilivyopita bila mimi kupata kazi, alianza kubadilika.
Alianza kunifananisha na wanaume wengine.
Alianza kuniuliza, “Una mpango gani na maisha yako?”
Alianza kunidharau mbele ya marafiki zake.
Siku moja aliniambia wazi kabisa:
"Mimi siwezi kuolewa na mwanaume asiye na mwelekeo."
Maneno yale yaliniumiza kuliko kufukuzwa kazi.
Wiki chache baadaye, alinieleza kuwa anahitaji “nafasi ya kufikiria.” Nafasi hiyo haikuisha — alienda kwa mwanaume mwingine ambaye alikuwa na kazi nzuri na gari.
Nilibaki peke yangu.
Sikuwa na kazi.
Sikuwa na mpenzi.
Na nilikuwa nimepoteza kujiamini.
Lakini hapo ndipo chanzo cha mabadiliko kilipoanza.
Nilikaa chini nikajiuliza —
Je, nitamruhusu aondoke na pia aondoke na ndoto zangu?
Nilianza kujifunza ujuzi mpya mtandaoni. Nilifanya vibarua vidogo. Nilikubali kuanza chini kabisa.
Haikuwa rahisi.
Kulikuwa na siku nilikataliwa interview.
Kulikuwa na siku nilikosa hata nauli.
Lakini sikurudi nyuma.
Mwaka mmoja baadaye nilipata kazi ndogo. Kutoka hapo nikapandishwa cheo. Nikaanza biashara yangu pembeni.
Leo hii nina kazi nzuri. Nina kipato kinachonitosha. Nimejenga heshima yangu upya.
Wiki iliyopita alinipigia simu.
Sauti yake ilikuwa ya upole kuliko kawaida.
Akasema,
"Nimekuwa nikikufuatilia… naona umebadilika. Naomba tuanze upya. Nilifanya makosa."
Nilikaa kimya kidogo.
Nikakumbuka siku alivyoniambia siwezi kuwa mwanaume wa kumuoa.
Nikamuuliza swali moja tu:
"Unanirudia kwa sababu unanipenda… au kwa sababu sasa nina mafanikio?"
Hakujibu moja kwa moja.
Na hapo nikajua

💘 Siku ya Wapendanao isikukute unalia kimya…Mahusiano yanapaswa kuleta furaha, sio maumivu.K**a unapitia changamoto kwen...
14/02/2026

💘 Siku ya Wapendanao isikukute unalia kimya…
Mahusiano yanapaswa kuleta furaha, sio maumivu.
K**a unapitia changamoto kwenye ndoa au mahusiano, usikae kimya.
❤️ Chukua hatua leo.
Usibebe mzigo peke yako.
📍 Face to Face – Tsh 50,000
📱 Simu/WhatsApp – Tsh 20,000 (malipo ya mara moja, msaada hadi ujisikie vizuri)
📞 0715 387 809
📍 Oysterbay – Dar es Salaam
Machozi sasa basi… 💕

Karibu sana ndugu!* Naitwa *Dennis Dessiny M*, mshauri wa kisaikolojia (Counselor Psychologist). *Gharama za ushauri ni ...
11/12/2025

Karibu sana ndugu!*
Naitwa *Dennis Dessiny M*, mshauri wa kisaikolojia (Counselor Psychologist).

*Gharama za ushauri ni k**a ifuatavyo:*
- *Tsh 50,000* kwa ushauri wa *face to face* (ukija ofisini).
- *Tsh 20,000* kwa ushauri kwa *njia ya simu/WhatsApp*.

*Faida:*
Malipo haya ni ya mara moja tu kwa ushauri wa simu—utaendelea kupata msaada wakati wowote hadi utakapopona au kujisikia vizuri.
Kwa ushauri wa ana kwa ana, utalipia kila unapokuja ofisini.

*Malipo:*
- *Lipa namba (Airtel Money):* 13128282
- *Jina:* Ushauri wa Maisha na Mahusiano

*Wasiliana nami kwa simu/WhatsApp:*
📞 *0715 387 809*

*_Machozi sasa basi..._*

Uzuri wa maisha unatengenezwa na wawili walio mapenzini. Suala la kudumisha upendo halitakiwi kuachiwa mtu mmoja huku mw...
22/11/2025

Uzuri wa maisha unatengenezwa na wawili walio mapenzini. Suala la kudumisha upendo halitakiwi kuachiwa mtu mmoja huku mwingine ametulia tuu. Kila mmoja anapaswa kuridhika na uwepo wa mwenzake ili upendo uwe wenye maana. Ukiona kila siku mwenzako anakukumbusha majukum yako au analalamika kuhusu mambo yale yale basi tambua unapaswa kujichunguza na kubadilika.

Usikubali uwe kikwazo kwenye mapenzi yenu sababu mmetoka mbali na tambua ukimpoteza huyo mwenye upendo wa kweli basi utakuja jutia pale utakaposhindwa kumpata mwingine atakayejitoa kwa ajili yako. Tumeagizwa upendo. Tuuishi bila hata chembe ya unafika ili kutimiza malengo.

Karibu sanaa ndugu Gharama za ushauri ni Tsh 50,000 kwa face to face ukija ofisini. Na Tsh 20,000 kwa njia ya simu. Kwahio unachagua njia ipi ni rahisi kwako.

Gharama hizi hutatoa tena endapo ukihitaji ushauri utapewa mda wowote hadi ukikaa sawaa. Isipokuwa kw ushauri wa face to face utalipa kila ukija ofisini.
Tupigie/Whatsapp 0715387809

09/11/2025

Mkizidisha mazoea, mnaweza kwazana bila kutegemea. Unaweza ukawa huru kupita kiasi na kujikuta unasema au kufanya matendo ambayo mwenza wako akayatafsiri tofauti. Urafiki udumishwe lakini mazoea yasizidi.

JE?
Hali yako ikoje ndugu rafiki. Una hali gani hapo ulipo? Una amani ya moyo au umeteseka kwa muda mrefu na misongo kichwani pamoja na mizigo moyoni? Unahisi huwezi tena kuipata furaha ya kudumu sababu changamoto nyingi zimekuandama?

Hebu nisikilize. Hata wale ambao walikua wamesha kata tamaa waliweza kusaidika na kurudi kwenye hali ya kawaida. Hawakutoka huko bila juhudi yoyote hapana! Waliweka nia ya dhati na kutumia njia sahihi za kupona maumivu yao. Hata kwako pia inawezekana.

Usiendelee kung'ang'ana na changamoto. Nipo hapa kwa ajili yako. Unaweza zungumza nami na kila kitu kikawa sawa. Karibu ujipatie Ushauri Tiba na Mwongozo wa Kisaikolojia na hakika maisha yako hayatokua k**a yalivyo kua mwanzo.

By counselor psychologist Dennis Dessiny M.

🌹 LOVE CONNECT TANZANIA 🌹Kila mtu anastahili kupendwa kwa dhati… lakini si kila mtu ana bahati ya kukutana na yule sahih...
15/10/2025

🌹 LOVE CONNECT TANZANIA 🌹
Kila mtu anastahili kupendwa kwa dhati… lakini si kila mtu ana bahati ya kukutana na yule sahihi kwa urahisi.
Hapa Love Connect Tanzania, kazi yetu ni kuunganisha mioyo 💞 — wale wanaotafuta upendo wa kweli, uaminifu, na mahusiano yenye heshima na thamani.

Tunaamini kuwa kila uhusiano mzuri huanza kwa ujasiri wa kuchukua hatua moja tu — hatua ya kuamini kuwa upendo bado upo.
Hapa tunakuongoza, tunakushauri, na tunakusaidia kupata mwenza anayekufaa, si kwa bahati tu, bali kwa kuelewana, maombi, na maadili. 🙏🏽

❤️ Unatafuta mwenza wa maisha?
💬 Unataka mtu wa kuelewana naye kwa heshima na mapenzi ya kweli?
📞 Tuma ujumbe WhatsApp sasa: 0715 387809

✨ Love Connect Tanzania – Tunagusa mioyo, tunaunda familia. ✨



















Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ushauri_wa_mahusiano_na_maisha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Ushauri_wa_mahusiano_na_maisha:

Share