24/09/2022
Kutokwa damu kipindi cha ujauzito ni hali hatarishi, inawezekana ni dalili ya kutaka kuharibika kwa mimba au complications za mimba tu. Mama aidha hutokwa damu kwa kiasi kidogo (matone) au kiasi kikubwa, haswa kipindi cha miezi 3 ya kwanza ya mimba (first trimester) mpaka miezi 3 ya mwisho( third trimester).
~ Damu inapotoka kiasi kidogo cha matone (spotting) hapo inaweza matatizo k**a ya infection au dalili ya kuharibika kwa mimba ila damu inapotoka kwa wingi hiyo inakuwa hali nyingine kabisa.
Complication nyingine zinazoweza sababisha mama kubleed damu kwa wingi ni:-
1. Kuharibika kwa mimba. Mjamzito anapotokwa damu kwa wingi yenye madonge makubwa au madogo kidogo hiyo ni ishara kubwa ya kuharibika kwa mimba.
2. Kuharibika kwa placenta(kondo) kunachangia mama kutokwa damu.
3. Yai kutungwa nje ya mji wa mimba (ectopic preganancy). Mfano mimba kutungwa kwenye mirija ya uzazi(fallopian tube) hapo nafasi ya kulea mimba na mpaka miezi 9 ni ndogo, hiyo hali inamletea mama kupata damu kwa wingi. Ndio mana Wizara ya Afya inashauri mama unapopata mimba toa taarifa kituo cha afya usisubirie ikue miezi 4-5 ndio uanze clinic.
4. Kondo(placenta) kuwa na matatizo kwenye ukuta wa uzazi.
5. Mabadiliko ya mwili yanachochewa na homoni(hormonal changes), inasababisha mama kutokwa damu matone madogo madogo (spotting).
6. Kushiriki tendo la ndoa uume akigonga kwenye mlango wa uzazi kunaweza msababisha mama kutokwa damu kidogo (matone). Mama akiona iyo hali ni vizuri kuacha kushiriki tendo la ndoa muda kwanza.
7. Maambukizi yanapompata kupitia ukeni au cervix k**a U.T.I, PID, kaswende, gonorea n.k ni rahisi kutokwa damu kipindi cha miezi 3 ya kwanza (first trimester). Mama mwenye infections anatakiwa kuwahi hospital ili kuokoa maisha yake na mtoto, infetions husababisha watoto kuzaliwa na ulemavu (kuona,kusikia n.k)
8. Mama anapofanyiwa vipimo na mkunga au daktari na kuwekea kidole ndani ya uke kunaweza msababishia kutokwa damu matone.
9. Mama anapojifungua kabla ya week 37(preterm labor) atasikia kutanuka kwa uke kunakoweza ambatana na damu, kuhara, maumivu ya mgongo na mvuto kwenye nyonga.
Muhimu:
Unapoona damu inakutoka haijalishi kidogo au nyingi, wahi hospital